19. Sep, 20:04
Utambulisho wa Tangazo 3385405
TSh 1

BAWASIRI,CHANZO CHAKE ,DALILI ZAKE NA MATIBABU KWA DAWA ASILI

Ilala, Ilala Dar Es Salaam
Seller offers delivery

Free delivery

Maelezo ya Bidhaa
Bei Maelewano
Ndiyo
Hali
Mpya
Maelezo

UFAHAMU UGONJWA WA BAWASIRI, AINA ZAKE, DALILI ZAKE NA MATIBABU YAKE MEPESI.

Bawasiri ni nini
-Bawasiri ni Ugonjwa unaotokana na kuvimba/kupasuka kwa mishipa ya damu sehemu ya haja kubwa na kupelekea kuota kwa kinyama amcho ndio huitwa Bawasiri/mgoro/mgongo nk
▶️Sababu kubwa ya mtu kupata Bawasiri ni Mgandamizo sehemu ya haja kubwa ambapo mgandamizo huo hupelekea kupasuka/kuvimba kwa mishipa midogo midogo ya damu aina ya veins sehemu ya haja kubwa hivyo hupelekea kuota kwa kinyama,miwasho,maumivu .

DALILI ZA MTU MWENYE BAWASIRI

1.?kupata muwasho mkali katika eneo la juu la haja kubwa
2.?kujitokeza kwa kinyama/vinyama eneo la haja kubwa
3.?kutokewa na kiuvimbe katika tundu ya haja kubwa
4.?kupata kinyesi chenye damu
5.?kupata maumivu makali wakati wa kujisaidia
6.? Kupata maumivu ya tumbo/kiuno hasa Bawasiri inapofikia hatua mbaya

MAMBO YANAYOWEZA KUSABABISHA MTU KUPATA BAWASIRI

▶️ Uzito kupita kiasi(Overweight)
▶️ Ujauzito
▶️ Unywaji pombe
▶️ Kukaa sana sehemu ngumu
▶️ Kuingiliwa sehemu ya haja kubwa( tendo la ndoa kinyume).
▶️ Kujisaidia Choo Kigumu. Sababu za kujisaidia choo Kigumu ni:
-Vidonda vya TUMBO
-Ngiri/Hernia
-Ulaji duni
▶️ Kula sana nyama nyekundu
▶️ Presha ya kupanda
▶️ Kula sana pilipili
▶️ Kula udongo(Wajawazito na watoto wadogo)

AINA ZA BAWASIRI⤵️
-Kuna aina 2 za Bawasiri kama ifuatavyo⤵⤵⤵⤵

1⃣. BAWASIRI YA NJE
Ni kuota kinyama sehemu ya nje ya haja kubwa ambapo kinyama huwa nje hata kama hujaenda kujisaidia haja kubwa.

2️⃣.BAWASIRI YA NDANI
Ni kuota kinyama sehemu ya ndani ya haja kubwa mara nyingi huambatana na maumivu makali na damu na kinyama hutoka wakati wa kujisaidia haja kubwa.

Bawasiri ya dani ina hatua NNE ambazo ni:⤵⤵⤵⤵

HATUA YA KWANZA
Katika hatua hii mtu hujihisi maumivu makali,miwasho pamoja na kutokwa damu wakati wa kujisaidia na kinyama hakionekani wakati wa kujisaidia.

HATUA YA PILI
Hii hutokea wakati wa haja kubwa na kurudi yenyewe punde baada ya kujisaidia

HATUA YA TATU
Hii hutokea wakati wa haja kubwa na mtu kuweza kurudisha ndani yeye mwenywe ama inaweza kurudi yenyewe baada ya muda

HATUA YA NNE
Hii ni bawasiri inayotoka na huwa ngumu kurudi baada ya kujisaidia.

ATHARI ZA BAWASIRI
1.?Upungufu wa damu mwilini
2.?Kutokwa na kinyesi bila kujitambua
3.?kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa
4.?kupungukiwa nguvu za kiume
5.?kupungukiwa na uwezo wa kufanya kazi kutokana na maumivu
6.?Kupata tatizo la kisaikolojia
7.?Kutopata ujauzito
8.? Mimba kuharibika
10.? Kupata kansa ya utumbo ( Colorectal cancer)
11.? Mwili kudhoofika

NJIA ZA KUJIKINGA DHIDI YA BAWASIRI
1.?Kula mboga za majani na nafaka zisizo kobolewa kwa wingi
2.?kunywa maji mengi lita sita hadi kumi na mbili kwa siku
3.?Acha kufanya mapenzi kwa kutumia tundu la haja kubwa (kulawitiwa)
4.?Punguza kukaa chooni kwa muda mrefu, kunaweza kuongeza shinikizo katika njia ya haja kubwa.
5.? Acha kunywa pombe
6.?Punguza kula nyama nyekundu
7.?Punguza matumizi ya pili pili.
8.?Jitibie vidonda vya tumbo
9.? Jitibie Ngiri
10.? Dhibiti uzito wako
11.? Jiepushe/punguza kunyanyua vitu vizito mara kwa marafiki.

ZIJUE SABABU ZINAZOWAFANYA WAGONJWA WENGI WA BAWASIRI KUTUMIA DAWA NYINGI BILA MAFANIKIO

Kwanza Mgonjwa wa Bawasiri anatakiwa kufahamu ya kwamba,matibabu si dawa pekee.Watu wengi wa naamini kwamba matibabu ni dawa pekee na jambo hili limepelekea wengi kuteseka na matatzo kwa muda mrefu sana bila mafanikio na kupelekea kukata tamaa ya kutafuta tiba na badala yake humuona kila mtoa huduma ni tapeli

Zifuatazo ni sababu zinazowafanya wagonjwa wengi kuteseka na Bawasiri kwa muda mrefu licha ya kutumia dawa mbali mbali:

1.? Kutopata dawa sahihi
-Si kila dawa inayotangazwa kutibu Bawasiri inaweza kutibu Bawasiri bali dawa yenye ufanisi wa kutibu ndio inaweza kutibu Bawasiri.

2.? Kutofuata ushaur wa daktari.
-Usipofuata yale ambayo daktari anakuelekeza ili kupata suluhisho la Tatizo lako ni ngumu kupona tatzo lako.

3.? Kutoziacha sababu zilizopelekea upate Bawasiri. Katika hili wengi wamefeli kwani haiwezekani ukapona Bawasiri ikiwa sababu zilizopelekea upate Bawasiri hutaki kuziacha mfano;
-Pombe
-Uzito mkubwa
-Ulaji mbovu
-Kuingiliwa kinyume
-Kula sana pilipili
-Kukaa sana chini
-Kunyanyua vitu vizito
-Kutotibu Magonjwa kama Ngiri na Vidonda vya TUMBO
-Kutokula vyakula vya kulainisha choo kama vile Mboga za majani & matunda
-Kula udongo(wajawazito)
-Kujisaidia kwenye vyoo vya kukaa.
-Kuharisha mara kwa mara
-Kujisaidia choo Kigumu

Hata utumie dawa zaid ya 100,usipoziacha sababu hizo ni ngumu sana kupona Bawasiri na matokea yake kila mtoa tiba utamuona Tapeli kumbe sababu ni wewe mwenyewe kutofuata miongozo,maelekezo na USHAURI kutoka kwa daktar.

⚫ Ukizingatia hayo utapona Bawasiri kwa muda mfupi sana(wiki 1 mpaka 3) Nakuhakikishia wapo wanaopona kwa siku 5 licha ya kukaa na Bawasiri kwa miaka kadhaa.

? KWANINI UZITO KUPITA KIASI NI SABABU YA MTU KUPATA BAWASIRI???

⤵⤵⤵⤵⤵⤵⤵⤵
-Uzito kupita kiasi ni katika sababu ya kupata Bawasiri kwasababau uzito mkubwa hupelekea mgandamizo katika mishipa ya damu(Veins) sehemu ya haja kubwa na puru hivyo husababisha kupasuka/kuvimba kwa mishipa ya damu eneo hilo kisha husababisha kutoa kwa kinyama/uvimbe ikiambatana na damu,maumivu na miwasho.

Hivyo kuwa na uzito kupita kias ni kuwa hatarini kupata Bawasiri

: MAMBO YA KUFANYA KWA MWENYE BAWASIRI ILI KUPATA AHUENI NA MAUMIVU YA BAWASIRI
1?Epuka matumizi ya vilevi/pombe.
2? Epuka matumizi ya pilipili.

3? Epuka kukaa sana sehemu ngumu kwa muda mrefu.

4?Epuka matumizi ya nyama nyekundu kama vile nyama ya mbuzi,ng’ombe na Kondoo

5? Epuka Kuingiliwa/kufanya mapenzi sehemu ya haja kubwa.

6?Punguza vyakula vya mafuta

7?Epuka/punguza unyanyuaji wa vitu vizito.

8? Punguza matumizi ya vyakula vya ngano.

9? Epuka kula vyakula vyenye kusababisha choo kuwa kigumu.

10? Jitibie magonjwa ya ngiri,vidonda vya tumbo nk.

11.?Jitahid kula Mboga Mboga na matunda katika mlo wako wa kila siku

*Jitahid kutumia juice ya matunda kama vile parachichi,passion na maembe angalau mara 3/5 kwa siku

? KWANINI POMBE NI KATIKA VISABABISHI VYA BAWASIRI/MGORO(Hemorrhoids)

Pombe husababisha Bawasiri kwa namba kubwa mbili kama ifuatavyo⤵⤵

1⃣ Pombe husababisha UPUNGUFU wa maji mwilini.
-Pombe ina Kemikali Lupolin ambayo huathiri mfumo wa Hormone katika Ubongo,huathiri homoni inayodhibiti upotevu wa maji mwilini ( Anti-diuretic Hormone) hivyo kusababisha mwili kupoteza maji mengi (Diuretic) na kusababisha Mnywaji kujisaidia choo Kigumu na choo Kigumu hupelekea mgandamizo sehemu ya haja kubwa/puru na kusababisha mishipa ya damu (Veins) eneo hilo kupasuka/kuvimba na kusababisha Bawasiri.

2️⃣ Pombe Husababisha Presha ya damu.
-Pombe husababisha mwili kuzalisha hormone iitwayo Endothilin 1 ambayo huingia kwenye damu na kusababisha kusinyaa kwa mishipa ya damu ( Vasoconstriction of blood vessels).Kusinyaa kwa mishipa ya damu hupelekea presha kupanda na baadae husababisha mishipa ya damu sehemu ya haja kubwa kupata stress/straining na kupelekea kuvimba/kupasuka kwasababu ipo eneo LA haja kubwa ambalo huwa na Mgandamizo mtu anapokaa ama kujisaidia nk hivyo hali hii hupelekea mtu kupata Bawasiri ambayo huambatana na Miwasho mikali,maumivu makali,kutoa damu na kuota kinyama eneo la haja kubwa/puru

—Hivyo ndivyo pombe husababisha Bawasiri kwahyo kama una Bawasiri halafu unakunywa pombe kupona ni ngumu sana unaweza kutumia dawa za kila aina bila mafanikio.
.? KWANINI KUKAA SANA SEHEMU NGUMU NI KATIKA SABABU YA MTU KUPATA BAWASIRI

MAJIBU
⤵⤵⤵⤵⤵
-Kukaa sawa sehemu ngumu ni katika sababu za watu kupata Bawasiri kwasababau kukaa sana sehemu ngumu hupelekea kutokea mgandamizo mkubwa sehemu ya haja kubwa /puru hali hii husababisha mishipa ya damu (Veins) eneo la haja kubwa kuvimba/kupasuka na hii hupelekea mtu kupata Bawasiri na kupeleka kuota kinyama,kupata miwasho,kutokwa damu wakati wa kujisaidia,kupata maumivu makali ama yote kwa pamoja.

USHAURI
Kama kazi unazozifanya hupelekea kukaa kwa muda mrefu basi jitahid kusimama kwa muda wa dakika 10 mpaka 15 kila baada ya kukaa masaa mawili,hii itakusaidia kupunguza mgandamizo sehemu ya haja kubwa na kujiepusha na Bawasiri ama kupata Bawasiri.
? KWANN UJAUZITO HUWEZA KUPELEKEA MTU KUPATA BAWASIRI
⤵⤵⤵⤵⤵⤵

Wajawazito kupata Bawasiri Kutokana na sababu zifuatazo:

1⃣ UZITO KUZIDI & MGANDAMIZO
-Mwanamke mjamzito huongezeka uzito na Mgandamizo sehemu ya hajakubwa kwasababu ya uzito wa Mtoto na ukuaji wa mwili na Kizazi(Uterus) hali hii hupelekea mgandamizo sehemu ya haja kubwa na Puru na KUSABABISHA mishipa ya damu midogo midogo (Veins)sehemu ya haja kubwa huvimba /kupasuka na kupelekea kuota kwa vinyama/kinyama,kutoa damu ,maumivu makali na miwasho ambavyo ni viashiria vya Bawasiri.

2️⃣ KULA UDONGO
-Baadhi ya wajawazito hula sana Udongo, ukaji wa udongo hupelekea Mjamzito kupata choo Kigumu (Constipation).Choo Kigumu husababisha mgandamizo sehemu ya haja kubwa na kupelekea mishipa ya damu eneo la haja kubwa/puru kupasuka/kuvimba na kupelekea mtu kupata Bawasiri.

3️⃣ Kutokunywa maji Mengi
-Baadhi ya wajawazito hushindwa kabsa kunywa maji ingawa wakat huo maji huhitajika kwa wingi mawilin hali hii hupelekea kujisaidia choo Kigumu/Constipation na kupelekea mgandamizo kwenye mishipa ya damu eneo la haja kubwa na KUSABABISHA kuvimba/kupasuka kwa mishipa ya damu eneo la haja kubwa na kupelekea kutokea kwa bawasiri (piles)
MATIBABU YA UGONJWA WA BAWASIRI

⤵⤵⤵⤵⤵⤵⤵
Kuna matibabu aina mbili katika kutibu ugonjwa wa Bawasiri:

1.? MATIBABU YA KISASA
-Matibabu ya kisasa yanahusisha matibabu ya Hospital ambapo tiba kubwa ya Bawasiri kwa hospital ni kufanyiwa upasuaji mdogo ( minor surgery) kwaajili ya kuondoa kinyama. Changamoto kubwa ya matibabu haya ni kwamba asilimia kubwa ya wagonjwa wanaofanya upasuaji wa tatzo hili tatizo hujirudia kwasababu upasuaji huondoa athari ya tatzo na si mzizi wa tatizo yaani ni sawa na kukata mti kisha ukaacha mizizi bila shaka mti huo utachipua na kumea tena.Lakini pia Upasuaji wa Bawasiri huwa na maumivu makali sana na uponaji wa kidonda hufika mpaka miezi miwili,hali hii ya kukaa na kidonda kwa muda mrefu kunaweza kupelekea kupata Kansa ya utumbo ( Colorectal Cancer).

2.? MATIBABU KWA NJIA ASILI
-Matibabu haya yanahusisha utumiaji wa dawa zinazotokana na mimea dawa.Dawa hizi Hutibu Bawasiri bila kufanya upasuaji na huweza kuleta matokeo ya haraka kwa mgonjwa endapo atatumia dawa huku akijitahid kujiepusha na visababishi vyote vinavyopelekea mtu kupata Bawasiri. Zipo dawa asili nyingi na nzur sana katika kutibu Bawasiri, mfano wa dawa hizo ni Bawasiri Fluid na Bawasiri powder,dawa hizi zina ufanisi mkubwa katika kutibu Bawasiri endapo Mgonjwa atazingatia maelekezo.
? KWANINI KUINGILIWA SEHEMU YA HAJA KUBWA(kulawitiwa ) NI KATIKA SABABU ZA MTU KUPATA BAWASIRI

MAJIBU
⤵⤵⤵⤵⤵
-Kuingiliwa sehemu ya haja kubwa ni katika sababu za mtu kupata Bawasiri kwasababau sehemu ya haja kubwa ni sehemu maalumu kwaajili ya haja kubwa hivyo Kuingiliwa sehemu hiyo hupelekea mgandamizo na kupasuka kwa mishipa ya damu kwasababu ya ufinyu wa eneo hilo hivyo hupelekea kupata Bawasiri.

Huu ni mchezo mchafu sana na wengi ambao huufanya mchezo huu hufikia hatua ya kupata Kansa ya utumbo (Colorectal cancer) hivyo watu wajiepushe kabsa na huu Ushetani kwani ni hatari kwa afya yako na ni Madhambi Makubwa kwa Muumba.

? KWANINI KUJISAIDIA CHOO KIGUMU NI KATIKA SABABU ZA MTU KUPATA BAWASIRI??

MAJIBU
⤵⤵⤵⤵⤵
-Kujisaidia choo Kigumu/Constipation ni katika sababu za kupata Bawasiri kwasababau mtu hutumia nguvu nyingi wakat wa kujisaidia hivyo hupelekea mgandamizo wa mishipa ya damu sehemu ya haja kubwa/puru hali hii hupelekea kupasuka/kuvimba kwa mishipa ya damu na kusababisha Bawasiri

Miongoni mwa sababu za mtu kujisaidia choo Kigumu ni:⤵⤵⤵⤵⤵

▶️ Ulaji duni -Kutohusisha vyakula vyenye nyuzi nyuzi(fibres) katika mlo kama vile Mboga za majani na matunda pia kutokunywa maji ya kutosha.Pia kula vyakula vilivyokobolewa kama Sembe na Wali bila kuhusisha vyakula vya kusaidia mmeng’enyo wa chakula ni katika sababu ya kupata choo Kigumu.

▶️ Vidonda vya TUMBO
-Vidonda vya tumbo husababisha mtu kujisaidia choo Kigumu kwasababu vidonda huathiri mmeng’enyo wa chakula na kupelekea kupata choo Kigumu.

▶️ Ngiri/Hernia
–Ngiri/Hernia husababisha mtu kujisaidia choo Kigumu kwasababu Ngiri huathiri mmeng’enyo wa chakula na kupelekea kupata choo Kigumu hivyo husababisha Bawasiri.

MUHIMU
-Mtu mwenye Ngiri na Vidonda vya TUMBO ni ngumu sana kupona Bawasiri endapo hatotibu Ngiri na Vidonda vya TUMBO pia wakati anatibu Bawasiri.

-Usipojua chanzo cha Bawasiri yako na kutatua chanzo hicho basi unaweza kuhangaika na Bawasiri hata kwa miaka zaid ha 10.

-Bawasiri ni athari. ambayo inaashiria kuna tatzo hivyo tibu/Jiepushe na chanzo Bawasiri itakukimbia yenyewe .
Mwisho:
Kama umepanda makala hii; Karibu tutakusaidia zaidi.

Ilala Daresalaam Tanzania.

Dr.Magessa
Mwanachama tangu 19. Sep
Verified via:
Mobile Number
Wasiliana na Muuzaji
Contact via Phone
Contact via Chat
Ripoti Tangazo Hili
Kataa
Jiunge na jarida letu

Tunachagua tunavyovipenda na tunakutumia bidhaa moto moto kila wiki!!