Tunawaunganisha wanunuzi na wauzaji Tanzania tangu 2009!
 

Kuhusu Sisi

Kuhusu Sisi
Kuwa Salama
Maswali Yanyoulizwa Mara kw Mara
Tangaza na Sisi

Kuhusu Sisi

ZoomTanzania ni jukwaa la mtandaoni la matangazo linalotoa fursa pekee kwa wanunuaji na wauzaji kuwafikia walengwa kwa ufanisi.

ZoomTanzania inajali usalama wa wote, wauzaji na wannunuaji. Mifumo yetu ya uchunguzi inatuwezesha kutambua watumiaji walaghai mapema. Na muhimu zaidi, tunahakikisha kila kitu kwenye ZoomTanzania kinapitiwa kwa umakini na timu yetu na kufaulu viwango vyetu vya ubora wa juu.

Tunatoa matangazo ya BURE kwa watangazaji kuwawezesha kufikia masoko yao bila kikomo na bila vikwazo. ZoomTanzania inafanya kazi ya kuhakikisha matangazo yako yanafikia walengwa wengi kupitia mitandao yetu na tovuti shirikishi hivyo kurahisiha kazi kwako.

Wasiliana nasi leo ugundue ni jinsi gani ZoomTanzania inaweza kukusaidia kukuza biashara yako.

Kuwa Salama

Tunajumuisha teknolojia ya ZoomTanzania ya kisasa na timu yenye kuwajibika ili kukupatia nafasi salama ya kuuza na kununua. Lakini, tunadhibiti sehemu moja tu ya utaratibu wa kununua. Wewe unaweza kufanya yafuatayo:

Dondoo za Usalama kwa Wanunuzi:

 1. Hakikisha umekagua bidhaa kabla ya kuinunua
 2. Kutana na muuzaji kwenye eneo la umma.
 3. Uliza kuhusu utaratibu wa kufikishiwa bidhaa kabla hujanunua
 4. Ni salama zaidi kuwasiliana na muuzaji kupitia sehemu ya barua pepe iliyopo ZoomTanzania. Kwa njia hii tunapata taarifa zako za mawasiliano ili tuweze kukujulisha pale tutakapo gundua tabia za kilaghai.
 5. Toa malipo pale tu utakapopata bidhaa

Dondoo za usalama kwa wauzaji:

 1. Hakikisha umeweka picha sahihi ya bidhaa
 2. Hakikisha umeweka namba ya simu au barua pepe inayofanya kazi
 3. Hakikisha simu yako haijazimwa ili uweze kupokea simu kutoka kwa wateja
 4. Kuwa makini na ujumbe bandia.
 5. Hakikisha unakutana na mnunuaji kwenye eneo la umma.
 6. Hakikisha umepata malipo yako kabla hujatoa bidhaa au huduma.

Jinsi ya kugundua walaghai

 1. Angalia bidhaa na bei-je ni bei ya busara au inaonekana nzuri mno kuwa kweli?
 2. Unaambiwa ulipe kupitia mifumo isiyojulikana, malipo ya kielektroniki au unaambiwa ulipe kwanza ndio upewe bidhaa?
 3. Muuzaji anajaribu kutoa uhakiki bila kuulizwa?
 4. Muuzaji hataki kujibi maswali ya muhimu, au hapokei simu yake?
 5. Muuzaji hataki kutumia njia za usafirishaji zinzowezwa kufuatiliwa?

Kila kitu kipo sawa?

Kama sio sawa, wasiliana na timu yetu kupitia:

Kama kila kitu kipo sawa, basi endelea kutafuta bidhaa unayohitaji au ingia utangaze bidhaa yako hapa

Maswali Yanyoulizwa Mara kw Mara:

ZoomTanzania inahusu nini?
ZoomTanzania ni jukwaa la mtandaoni la matangazo linalotoa fursa pekee kwa wanunuaji na wauzaji kuwafikia walengwa kwa ufanisi.
Wauzaji wanatangaza bidhaa zao kwenye tovuti yetu, wewe una peruzi kupata unachohitaji na kuwasiliana na muuzaji moja kwa moja kupanga jinsi ya kufanya biashara.

Nawezaje kuuza bidhaa zangu kupitia ZoomTanzania?
Tangaza bidhaa zako bure kwenye tovuti yetu na utafikia maelfu ya wateja.
Anza na akaunti ya bure hapa
Baada ya kufanya hiyo utaweza kutengeneza tangazo lako na kuanza kupata pesa.

Inachukua muda gani kwa tangazo lako kuhakikiwa?
Muda wa kuhakiki kwa masaa ya kazi hauzidi masaa 2 na nje ya masaa ya kazi hauzidi masaa 8, hii haihusishi siku za mapumziko.

Nawezaje kuwasiliana na muuzaji wa bidhaa?
Unaweza kuwasiliana na muuzaji kwa kufungua tangazo na kumfikia kupitia njia hizi 2:

 • Simu: bonyeza kitufe cha "Show Number/Onyesha Namba" na umpigie muuzaji kupitia namba itakayotokea hapo
 • Barua Pepe: tumia sanduku la maelezo lililopo chini ya "Taarifa za Mtumiaji/User Information" za muuzaji na utume barua pepe

Nimesahau nenosiri langu, nawezaje kuingia?
Kwenye ukurasa wa kuingia unaweza kubadilisha nenosiri kwa kuingiza barua pepe ya akaunti yako kwenye kisanduku cha maelezo cha "Forgot Password/Nimesahau Nenosiri"

Nawezaje kuomba kazi iliyowekwa ZoomTanzania?
Unaweza kuomba kazi moja kwa moja kupitia maelezo ya kuomba yaliowekwa kwenye tangazo la kazi. Pia kumbuka baadhi ya kazo zinahotaji utengeneze akaunti ya ZoomTanzania (Ya Bure) na uwe umeingia.
Anza na akaunti ya bure hapa

Ningependa kuweka tangazo kwenye gazeti lenu, Nifanyaje?
Gazeti letu bado halijaanza kutolewa, lakini unaweza kutumia jukwaa letu la mtandaoni kutangaza bidhaa na huduma zako.
Ongeza nguvu ya tangazo lako zaidi ya mara 10 kwa kuliweka kama Premium Listing/Tangazo la Premium au biashara yako kwa kuiweka kama Premium Business Account/Akaunti ya Biashara ya Premium. Wasiliana na sisi kujua zaidi

Natoa vipi taarifa kuhusu ulaghai/vitu bandia/matangazo yenye mashaka?
Kila tangazo lina kitufe cha "Report Suspicious Ad/Ripoti Tangazo lenye mashaka". Bonyeza kitufe hicho na andika sababu zilizokufanya uripoti tangazo hilo kwenye kisanduku cha maelezo. Tutapokea ripoti yako na kuchukua hatua haraka iwezekanavyo. Pia unaweza kututumia tangao hilo kwenye kurasa yetu ya Facebook au kupitia barua pepe info@zoomtanzania.com au tupigie kupitia +255 655 140 602 na timu yetu itakusikiliza.

Nawezaje kuwasiliana na nyinyi kwa msaada?
Kwa maswali zaidi- Wasiliana na sisi kupitia


Tangaza bidhaa au huduma zako kwenye jukwaa kubwa zaidi la matangazo mtandaoni Tanzania kwa kuweka tangazo lako au kusajili biashara yako na sisi. Kutangaza na sisi ni BURE.

Ongeza hadhi ya bidhaa au biashara yako zaidi kwa kufanya yafuatayo:

 1. Kodisha Bango la matangazo la mtandaoni kwenye tovuti yetu
  zoomtanzania.com inatembelewa na maelfu ya watu kila siku. Fikia walengwa unaohitaji na kwa wingi zaidi: Kama unatafuta wafanyakazi au wanunuzi wa samani-tutakufikisha kwa walengwa unaohitaji. Pia pata ufahamu wa kiundani kuhusu walengwa wako na jinsi ya kuwafikia.
 2. Tangaza kwenye jarida letu la mtandaoni
  Tunachagua ofa nzuri na za kisasa kwa watumiaji wetu. Usambazaji wa kila wiki unakuwezesha kufikisha ujumbe wako kwa jamii ya wanunuzi unaohitaji.

Kama unataka kutangaza biashara yako, Wasiliana na sisi leo!

Jiunge na jarida letu

Tunachagua tunavyovipenda na tunakutumia bidhaa moto moto kila wiki!!