Wednesday, 18:31
Ad ID 3505699

VIDONDA VYA TUMBO NA TIBA YAKE.

Kinondoni, Mikocheni Dar Es Salaam
Description

Vidonda vya tumbo ni tatizo linalotokea baada ya kuta za tumbo au utumbo mdogo kuwa na vidonda, hii hutokea ni baada ya kuharibika kwa ukuta wenye ute unaozuia kemikali za kuyeyusha chakula unaoitwa mucus.

Kemikali ambayo ni acidi inayozalishwa mwilini kiasili husaidia kuyeyusha chakula na kuua wadudu tumboni, kama ukuta wenye ute ukiharibiwa na kushindwa kufanya kazi basi kemikali (acid) itaathiri tumbo au utumbo na kuruhusu bakteria kuendelea kusababisha vidonda vya tumbo.

Vidonda vya tumbo vinatibika kirahisi ila vikicheleweshwa bila kutibiwa huweza kusababisha tatizo kubwa. Ni tatizo linalotesa sana na kuwanyima raha watu wengi, linahitaji umakini na pia husababisha magonjwa mengine kama kansa, amoeba (amiba), homa, kupungua uzito.

AINA ZA VIDONDA VYA TUMBO

Kuna aina zipatazo mbili za Vidonda vya Tumbo (Peptic Ulcers)

Vidonda vya tumbo kubwa (Gastric ulcers) – Hivi ni vidonda vya tumbo vinavyotokea ndani kwenye tumbo kubwa

  1. Vidonda vya utumbo mdogo (Duodenal ulcers) – Hivi ni vidonda ambavyo hutokea kwenye utumbo mdogo (hasa juu)

CHANZO CHA VIDONDA VYA TUMBO

Vidonda vya tumbo vina vyanzo tofauti ili vyote ni vile vinavyohusiana na mmeng’enyo, vyanzo hivyo ni;

Bakteria waitwao Helicobacter pylori (H. pylori)
Matumizi ya dawa za kupunguza maumivu kama asprin, (NSAIDs), (Advil, Aleve, na zingine)
Kuwa na mawazo mengi
Kula vyakula vinavyozalisha acid kwa wingi
Kunywa pombe na vinywaji vikali
Uvutaji wa sigara
Kuto kula mlo kwa mpangilio

DALILI ZA VIDONDA VYA TUMBO

Dalili za vidonda vya tumbo hujitokeza baada ya kula au kabla ya kula, ila mara nyingi wengi huwa wanazipuuzia na endelea kukuza tatizo, vidonda vya tumbo vinadalili kama;

1.Kupata maumivu ya tumbo yanayokuwa
kama ya moto (kuunguza) baada na kabla ya kula

2.Kupatwa na kiungulia karibu na chembe ya moyo

3.Tumbo kujaa gesi na kuvimbiwa

4.Kichefuchefu na kutapika tena yawezekana kutapika damu

5.Kupata haja kubwa ya rangi kahawia au nyeusi yenye harufu mbaya sana, pia haja yaweza kuchanganyikana na damu

6.Kupoteza hamu ya kula na kupungua uzito

7.Kushindwa kupumua vizuri

JINSI YA KUEPUKANA NA VIDONDA VYA TUMBO

*Kunywa maji mengi

*Punguza mawazo, fanya mazoezi yatakupunguza na mawazo

*Punguza (balansi) kiwango cha halemu (choresterol)

*Usivute sigara

*Punguza au acha kunywa pombe

*Kula vizuri vyakula bora hasa asilia na sio vyakula vyenye kemikali

*Lala vizuri kwa muda mzuri – masaa 7 hadi 9

MADHARA YA VIDONDA TUMBO

Saratan ya utumbo

Kupungua kwa kinga ya mwili

Kupungua uzito

Kupungua kuvu za kiume

Kupoteza viini lishe muhimu mwilin

Wasiliana Nasi Kwa Msaada Zaidi.

DrMgonda
DrMgonda
Member Since 18. Nov '20
Verified via:
Mobile Number
Contact Seller
Contact via Phone
Contact via Chat
Report This Ad
Cancel
Join our weekly Newsletter

Learn about new items, custom picked just for you.