12. Aug, 11:06
Ad ID 3206473
TSh 37,500

SIKU ZA KUPATA UJAUZITO

Arusha Mjini Arusha
Seller offers delivery

Uwe ndani ya Arusha Mjini tu .Tofauti na apo utachangia gharama zitakazo husika

Details
Price negotiable
No
Description

SIKU ZA MWANAMKE KUPATA UJAUZITO

Kutungwa kwa mimba kunahitaji mambo kadhaa lakini ya msingi sana ni kukutana kwa yai la uzazi la mwanamke na mbegu ya kiume ndani ya muda hai katika mzunguko wa hedhi.

Mzunguko wa hedhi wa kawaida kwa wanawake ni kati ya siku 21 - 35. Lakini asilimia kubwa ya wanawake wana mzunguko wa hedhi wa siku 28.

Kwenye mzunguko wa hedhi kuna siku ambayo yai la uzazi lililopevuka linadondoshwa na linapokutana na mbegu ya kiume mimba uweza kutungwa. Kwahiyo ni muhimu sana kwa mwanamke kufahamu mzunguko wa hedhi yake una siku ngapi ili kuweza kujua siku za kufanya tendo la ndoa na kuweza kupata mimba.

Kwa kawaida wanawake wote wenye mizunguko ya hedhi yenye urefu wa siku tofauti, siku za baada ya yai la uzazi kudondoshwa hadi kuanza hedhi nyingine huwa ni sawa ambazo huwa ni siku 14. Siku zinazobadilika ni zile katika matayarisho ya yai la uzazi kukomaa na kudondoshwa. Ili kuweza kujua siku yako ya kuweza kupata ujauzito unachukua siku za mzunguko wa hedhi unatoa siku 14.

Nitazungumzia mifano tofauti kuelezea siku ambayo yai la uzazi linadondoshwa kuingia kwenye mirija ya uzazi.

Mfano wa kwanza ni kwa mwanamke mwenye mzunguko wa hedhi wa siku 28.

Siku za mzunguko wa hedhi uanza kuhesabiwa kuanzia siku ya kwanza kuona damu inatoka ukeni. Katika siku 28 toa siku 14 ambapo zinabakia siku 14. Kwahiyo, yai la uzazi lililopevuka linadondoshwa siku ya 14 kwa mwanamke mwenye mzunguko wa siku 28. Ili kutunga mimba, yai la uzazi linatakiwa kurutubishwa na mbegu ya kiume ndani ya muda usiozidi masaa 24 baada ya kudondoshwa kuingia kwenye mirija ya uzazi. Pia mbegu za kiume zikishaingia ndani ya viungo vya uzazi zinaweza kuwa hai kwa muda hadi siku 5.

Wengi wa wanawake wanapata mimba wanapofanya tendo la ndoa ndani ya siku 2 kabla ya yai la uzazi kudondoshwa au siku ya yai la uzazi kudondoshwa kwenye mirija.

Mfano wa pili kwa mwanamke mwenye mzunguko wa siku 35. Siku ya yai la uzazi kudondoshwa ni: siku 35 toa siku 14 unapata siku 21. Kwahiyo yai la uzazi linadondoshwa siku ya 21 kwa mwanamke mwenye mzunguko wa hedhi wa siku 35.

Tuangalie mfano mwingine wa mwanamke mwenye mzunguko wa hedhi wa siku 21. Siku yake ya yai la uzazi kudondoshwa kuingia kwenye mirija ni: siku 21 toa siku 14 unapata siku 7. Kwahiyo yai la uzazi linadondoshwa siku ya 7.

Kwa maana hiyo siku za kupata mimba zinatofautiana kulingana na mzunguko wa hedhi!

By Good Afya

Kama unatafuta mtoto na hujapata wasiliana nasi kwa msaada zaidi

Tupo
Arusha
Dar
Morogor
Dodoma
Mbeya
Mwanza na no

Bf suma
Member Since 26. Feb '20
Verified via:
Email Facebook Google Mobile Number
Contact Seller
Contact via Phone
Contact via Chat
Report This Ad
Cancel
Join our weekly Newsletter

Learn about new items, custom picked just for you.