26. Jul '20, 09:52
Ad ID: 1995004
TSh 290,000

Furahia Kukaa Siku Tatu ndani ya Zanzibar.

Other Zanzibar District Zanzibar
Details
Valid until
2022-03-31
Description

Je unahitaji kufika Zanzibar na Kutembea sehemu mbali mabli za utalii?

Saving Tour inakupatia fursa wewe mtanzania kuja kutembea sehemu mbali mbali ndani ya Zanzibar na kukaa makaazi ya Hoteli mbali mbali ndani ya Zanzibar kwa kupitia Booking.com kwa Bei za Mtanzania .

Pakage hii ni kwaajili ya Familia ambayo inahitaji kuja kutembea Zanzibar au Marafiki wanahitaji kutembea Zanzibar au Hata mtu pekeyake anahitaji kutembea Zanzibar anaweza kupata huduma hii na Siku tatu hizi atapata kutembea kama ifuatavyo:
Gharama za Hoteli Hazitakuemo kwenye Pesa ya Matembezi ila Tutakushauri kutokana na Bajeti yako hoteli gani Ukae. Chakula cha Asubuhi na Usiku ndio Kitakuemo kwenye Bajeti ya Matembezi.

Siku ya Kwanza
Tutakuchukua kwa gari yetu kutoka eidha Bandarini au Airport Bure ( gharama imo ndani ya bajeti)
Utafikia Hoteli ya mjini kama:

 1. Tembo Hotel
 2. Lost and Found
 3. Park Hyatt Hotel
 4. Serena Hotel
  Bei ya Hoteli ya makaazi Tutakushauri kutokana na kupatikana (Availability) kwa chumba ndani ya mtandao wa booking, Pesa yako na mandhari unayoyapenda ya Hoteli.

Kwahio kwenye Hoteli tutakupa fursa ya kutuambia bajeti yako na mapendekezo ya mazingira ya hotel na sisi tutakushauri wapi ukae.

Baada ya kukaa kwenye Hoteli sisi tutakuacha upumzike siku nzima na usiku utapata fursa ya kuenda Forodhani Garden kwaajili ya Kula chakula cha usiku kama Pweza, Mishakaki, Ngizi, Zanzibar Pizza nakadhalika.Kisha kurudi katika Hoteli na kuagana kwa siku ya pili.

Siku ya Pili
Tutakuja kwenye hoteli yako baada ya kumaliza Chakula cha Asubuhi, kisha utapata nafasi ya kuenda kutembea sehemu mbili na itachukua siku nzima kuanzia asubuhi hadi jioni, Kwanza Tutaenda Sehemu ya Historia na Kisiwa kinachoitwa " Prison Island" ambako tutaenda kuona makobe na majengo ya kizamani na kupata historia kwanini kisiwa hicho kimeitwa Prison Island na Kuitwa Quarantine Island. Pia tutaenda kutembea Fungu linaloitwa"Nakupend Island" Nalo ni maarufu na watalii wengi wanapenda kwenda kwaajili ya kuogelea, kufanya sorkeling, kula vyakula vya baharini kama Pweza, Ngisi, Kaa, Samaki
navyenginevyo. Kisha Tunategemea Kurudi Safari hii jioni ya saa kumi na kurudi Hotelini kwa Mapumziko.

Usiku tutakupeleka Lukmaan Restaurant kupata Chakula cha Usiku na kurudisha Hotelini kwa kuonana siku ya Tatu.

Siku ya Tatu
Asubuhi na Mapema baada ya kumaliza chakula cha Asubuhi tutaenda Nungwi Kukaa huko ambayo usafiri ni Bure.
Utafikia Hoteli Za Nungwi kama

 1. Z Hotel
 2. Aluna
 3. Kasa Beach Villa
  Hoteli zitakua hazipo kwenye Bajeti. Sisi tutakuchagulia kutokana na mapendekezo yako na Bajeti yako kupitia mtandao wa booking

Nungwi ni sehemu nzuri saana na inapendwa saana na watalii, asilimia 70% ya watalii zanzibar wanapenda kufikia Nungwi na kuna Shughuli tofauti tofauti za michezo ya baharini kama Parasailng, Jetski, Snorkeling, Diving na mengineo.
Ukifika Nungwi Tutakuzungusha Nungwi Village, Tutakupeleka Kuogelea na Kasa ambako utakutana na wageni tofauti tofauti na kuenda kupumzika beach. Usiku tutakupeleka Nungwi Inn ambako utapata nafasi ya kula chakula cha usiku hapo na kuagana.

Siku ya Nne
Baada ya chakula cha asubuhi na usalimiana. Itakua ni safari ya kukusindikiza Airpot au Bandarini kwaajili ya kurudi nyumbani.

Natumai utafarijika na Matembezi yetu ndani ya siku tatu.

Katika Matembezi haya Gharama ambazo zimo ndani ya Bajeti ni kama ifuatavyo:

 1. Usafiri wa Kukupeleka kukupokea, kukupeleka nungwi na Kukurudisha siku ya mwisho
 2. Chakula cha Asubuhi na Usiku isipokua siku ya pili imo chakula cha Mchana
 3. Mtembezi (Tour Guide)
 4. Viingilio kama Prison Island, Kuogelea na Kasa Nungwi.
  5 Ushauri.

Vitu Havimo kwenye Matembezi haya ni kama:

 1. Makaazi ya Hoteli
 2. Tiketi ya Ndege au Boti
  3 Chakula cha Mchana isipokua siku ya pili tu.

Pia Bei iliokuepo hapo ni kwa mtu mmoja, kama mutakua wengi unaweza kuwasiliana nasi kwa email kutuambia muko wangapi na lini munahitaji huduma yenu.

Kwa maelezo zaidi tupigie simu au tuma barua pepe kwa email yetu.

Saving Tour
Member Since 17. Sep '17
Verified via:
Email Mobile Number

Contact Seller
Contact via Phone
Contact via Chat
Report This Ad
Cancel
Join our weekly Newsletter

Learn about new items, custom picked just for you.