Eneo Ekari 20 Chalinze

TSh 4,000,000 / Acres
Ad ID
780566
Posted at
27. Jul, 09:00
Details
Price negotiable
Yes
Price per square unit
Yes
Unit of measure
Acres
Square units
20
Location
Kibaha Vijijini Pwani Chalinze pembeni ya Kiwanda cha Vigae cha Twyford
Description

ENEO LINAUZWA
Eneo lenye ukubwa wa ekari ishirini linauzwa Pingo, Chalinze. Eneo linapakana na Chuo cha Ualimu Chalinze kwa mbele na kwa upande wa kulia ni kiwanda kipya cha vigae kinachojengwa hapo Pingo.Kama ambavyo baadhi watakuwa wanajua, kiwanda cha vigae kitaajiri wafanyakazi wa kudumu 6,000 achilia mbali madereva na makonda  wa malori watakaokuja kupakia mizigo wenye kukadiriwa kufikia 2,000 kila siku ambao watalazimika kutafuta malazi. Kwa ujumla eneo hili linategemewa kuhudumia watu elfu kumi kwa makazi na malazi. Pamoja na hayo, ujenzi wa bandari kavu unaoendelea eneo la Kwala unaliongezea eneo hili matumizi mengine muhimu sana katika biashara. Mizigo yote inayoingia au kutoka bandarini ni lazima
ikaguliwe na maofisa wa serikali ambao kimsingi ni waajiriwa wa mamlaka ya Mji Mdogo na Wilaya mpya ya Chalinze. Eneo linatoa fursa kwa makampuni ya usafirishaji, uwakala wa forodha na uwakala wa meli kuweka yadi kwa ajili ya kuhifadhia, kukagulia, kupakilia na kupakulia mizigo inayoingia au kutoka bandarini yakiwemo makontena yenye shehena na matupu. Pamoja na hayo, uwepo wa shughuli za kibandari jirani na eneo hili unavutia uwekezaji wa nyumba za kulala wageni na sehemu za biashara. Kwa mfano watu watano walipakia mizigo yao ndani ya kontena moja, siku ya kulitoa bandarini ni lazima wote wawepo kwa ajili ya kupokea mizigo yao. Siku ya kupokea mzigo ikaangukia Ijumaa na bahati mbaya mashine
ya kupakilia mzigo ikaharibika au ikawepo sababu nyingine yoyote, basi wote watano watakuwa wageni eneo hili kwa siku 3. Watahitaji kula, kulala, kunywa na kupumzika. Kwa ujumla eneo lote la Chalinze, Pingo mpaka Vigwaza-mizani linatoa fursa ya Dar es Salaam mpya ya siku za usoni. Wakati wa kuwekeza ni sasa ambapo ekari moja ni TShs. 4,000,000 (milioni nne tu) na maelewano yapo. Unapimiwa kulingana na mahitaji yako na pia tunafanya upimaji (surveying) na kulifanya eneo lako litambulike kisheria kwa gharama nafuu sana. Wasiliana nami David Kilenga 0655 571 552 au 0675571452    Email:david.kilenga@gmail.com

ZoomTanzania Disclaimer:
WE VALUE YOUR SAFETY ABOVE EVERYTHING. NEVER PAY MONEY BEFORE VIEWING A PROPERTY, PLEASE REPORT ANY USER REQUESTING UPFRONT PAYMENT USING THE REPORT ABUSE BUTTON ON THIS PAGE. FOR MORE TOP TIPS ON KEEPING SAFE, SEE OUR SAFETY PAGES.
Kilenga Shipping Services Ltd.
Member Since 16. Sep '12 4 Active Ads Active Ads 4 Published Ads
Verified info
Contact Seller
Phone Seller
Email Seller
Report This Ad
Cancel
Join our Mailshot

Notification for member sales, events and promotions.