Connecting buyers and sellers in Tanzania since 2009!
 
15. Jul, 15:39
Ad ID: 1458582

Mafunzo ya Wiki 6 ya 3D Character Animation

Kinondoni, Mikocheni Dar Es Salaam
Description

Ujuzi katika 3D Animation una mahitaji makubwa hapa duniani. Unaweza kuajiriwa katika makampuni ya Video Games, film au television. Pia unaweza pia kujiajiri mwenyewe ukafanya kazi kama freelancer. Soko la watu wenye ujuzi huu ni kubwa sana.

Karibu katika mafunzo mapya ya 3D Animation yatakayoanza Jumatatu 8 July, 2019, Mikocheni, Dar es Salaam.

Katika mafunzo haya utajifunza kila kitu kinachohusiana na Character Animation kuanzia Modeling, Rigging, Texturing hadi Animation. Mafunzo haya yatakuwa ya vitendo yatakayomuwezesha mwanafunzi aweze kwenda kutumia ujuzi alioupata mara moja.

Mafunzo haya yataendeshwa na mtaalamu wa Post-Production, 3D Animation na Visual Effects, Paschal Ruta kutoka kampuni ya Animation na Visual Effects, Natron Studios.

Baada ya mafunzo haya utaingizwa kuwa member wa PUGU Project ambayo ni Lifetime Mentorship Program iliyoanzishwa na inayosimamiwa na kampuni ya Natron Studios kwa ajili ya kukuza wataalamu wa baadae.

Software zitakazotumika ni Autodesk Maya, ZBrush na Adobe Photoshop.

Hakuna vigezo vyovyote ili kushiriki. Sifa kuu ni uwe na nia ya kujifunza, jitihada na ufahamu wa utumiaji wa computer. Wasichana wanapewa motisha sana wa kuhudhuria.

Gharama za mafunzo haya ni Tsh. 200,000/= na mafunzo haya yatakuwa kwa muda wa wiki 6. Mwisho wa kujiandikisha ni Ijumaa 5 July, 2019. Usichelewe, nafasi zilizotengwa ni chache.

Ili kujiandikisha au kupata maelezo zaidi, wasiliana na sisi kwa simu au email.

Natron Studios
Member Since 6. Nov '15 2 Total Ads / 2 Active Ads
Verified via:
Email Mobile Number

Contact Seller
Contact via Phone
Contact via Email
Report This Ad
Cancel
Join our weekly Newsletter

Learn about new items, custom picked just for you.