Njia 5 za Kuwa Salama Wakati wa Kuuza Bidhaa Mtandaoni

  | 4 min read
0
Comments
2477
uza bidhaa mtandaoni sell online

Changamoto za biashara za mtandaoni haziwakumbi wanunuzi tu. Wauzaji wa bidhaa kupitia mitandao wanakumbana na changamoto nyingi pia. Kuna kupoteza muda mwingi wakati wa kukutana na mteja ili kukamilisha mauzo, hasa kwa wauzaji wanaosafirisha bidhaa wenyewe. Kuna wateja wanaoahidi kununua bidhaa lakini dakika ya mwisho wanasema hawahitaji. Wakati mwingine hata hawajibu simu wakati muuzaji kashaleta bidhaa kwenye eneo alilopo mnunuzi. Kuna hofu ya kutapeliwa na wateja ambao wanatumia nafasi hii kujinifaisha. Ukweli ni kwamba kuna changamoto nyingi zinazowakuta wauazaji mitandaoni.

Ukiwa makini, unaweza kufanya biashara yenye faida kubwa sana mtandaoni bila kupata adha hizi na nyingine. Hivyo kabla ya kuuza bidhaa mtandaoni, chukua tahadhari hizi ili uwe salama wewe na biashara yako.

1. Kuwa Makini Wakati wa Kukutana Uso kwa Uso na Mteja

uza bidhaa mtandaoni kuwa makini wakati wa kukutana uso kwa uso

Mfano unauza makochi yako nyumbani. Umeyatangaza kwenye mtandao kama ZoomTanzania. Mteja anakupigia anataka kuja kuyaona, humjui wala hakujui, na wewe ni muuzaji mwanamke na unakaa mwenyewe, unafanyeje? Wakati unauza vitu vyako vya nyumbani ambavyo huvitumii, kuwa nakini na ni unamualika nyumbani kuja kuvikagua. Ni kweli unahitaji kuuza  lakini usalama wako ni kipaumbele. Tafuta sehemu ambayo kuna watu, na kama ni muhimu sana aje nyumbani basi ni vyema usiwe peke yako. . Na kama ni kiwango kikubwa cha pesa anakuja kulipa, ni bora mkafanyia malipo kupitia huduma za simu za pesa au benki.

2. Kuwa Makini na Hundi na Huduma za Kifedha za Simu

Kama umeuza bidhaa za bei ndogo, kufanya malipo inaweza ikawa si tatizo sana. Mnunuzi anaweza akalipa kwa fedha taslim na mkamalizana hapo hapo. Lakini fikiria kama unauza bidhaa zenye  gharama kubwa na mnunuzi anataka kulipa kwa kutumia hundi au miamala ya simu. Mfano, hundi za watu binafsi zinaweza kuwa tatizo kwani huwezi kujua iwapo akaunti ya mnunuzi ina salio la kutosha au la. Kuna wauzaji wamepata changamoto na wanunuzi wanaolipa kupita benki na kutuma nyaraka za uthibitisho ambazo ni feki, na muuzaji bila kucheki kama hela imeingia, anatuma bidhaa.  Pia kuna wizi ambao uliingia kwa kutumia huduma za kipesa za simu. Mnunuzi anakulipa kupitia huduma kama Tigo Pesa, Airtel Money au Mpesa. Mkimalizana anakwenda kuripoti kuwa pesa aliyokulipa alikosema kufanya muhamala, hivyo inarudishwa. Usipokuwa makini na miamala ya pesa ambayo si taslim, unaweza kujikuta umetoa bidhaa zako bure..

3. Hakikisha Bidhaa Inamfikia Mnunuzi

uza bidhaa mtandaoni hakikisha bidhaa zinamfikia mnunuzi

Kwa wateja wa mikoani ambao inabidi utumie huduma ya mabasi ya abiria kusafirisha mzigo wako, inabidi kuwa makini sana. Fikiria umetuma mzigo na mnunuzi anasema hajapata bidhaa yake? Unafanyaje?

Moja ya wizi wa mtandaoni hutokana na wanunuzi wasio waaminifu wanaosema  hawajapokea mzigo wakati wameshapokea. Hivyo ni muhimu sana kuhakikisha umeandaa mfumo mzuri wa ufatiliaji wa bidhaa uliyotuma (tracking system), unaojumuisha uwekaji saini kwa kila hatua mzigo unapopita hadi unapomfikia mnunuzi. Pia unaweza kutumia mfumo wa namba ya siri ambapo mnunuzi lazima aziwasilishe namba hizo kabla ya kukabidhiwa mzigo. Unaweza kuwa na mtu husika katika vituo vya mabasi ambaye kazi yake ni kukabidhi mizigo yako badala ya kuwaachia makondakta wa mabasi.

4. Kuwa Makini na Wale Wanaobadilisha Bidhaa

Moja ya tatizo ambalo limewakumba wauzaji wengi wa mtandaoni ni ubadilishwaji wa bidhaa mbovu na nzima. Mteja anaweza kununua bidhaa nzima kabisa kutoka katika duka lako, ambayo inafanana kila kitu na bidhaa ambayo anayo nyumbani. Akipata bidhaa aliyokuagiza, anabadilisha (anachukua mpya kisha mbovu anakuwekea kwenye boksi lako) na kukupigia akisema bidhaa ni mbovu na anataka kuirudisha.

Kuepuka hili, hakikisha unakuwa na picha zenye maelezo ya kutosha na alama za bidhaa hiyo kabla ya kuitangaza mtandaoni. Baadhi ya wauzaji wakubwa huamua pia kuweka mhuri wa moto wa alama ya siri ili kuepuka kubadilishiwa bidhaa.  Ni tahadhari muhimu ambayo itakuhakikishia kuepuka kuuza TV nzima na kurudishiwa TV yenye kioo kilichopasuka.

5. Tengeneza Tangazo Salama

uza bidhaa mtandaoni tengeneza bidhaa mtandaoni

Mwisho, hakikisha wakati wa kutengeneza tangazo lako unatangaza bidhaa unayouza tu. Usiweke taarifa binafsi kama hakuna ulazima sana. Kumbuka kuwa, kila aina ya taarifa unayoitoa mtandaoni inaweza kuja kutumiwa kwa matumizi ambayo hutayapenda. Toa maelezo machache, muhimu na salama. Usiweke taarifa zinazohusu maisha yako binafsi kama anuani ya nyumba yako, n.k.

Angalia kwa makini picha unayoitumia kutangaza bidhaa zako. Hakikisha unaonyesha tu bidhaa unayouza. Na kama hakuna ulazima sana, basi usitumie namba au barua pepe binafsi katika matangazo ya biashara yako. Tumia mitandao salama mfano ZoomTanzania ambapo baada ya kuuza bidhaa yako, namba yako ya simu na barua pepe havitaweza kuonekana mtandaoni tena, mpaka pale utakapokuwa tayari kuuza kitu kingine.

Mustapha Mosha
Mustapha Ally is a Community Marketing Manager at Zoom Tanzania and BrighterMonday Tanzania. He loves digital marketing social media