Wakala wa Usafiri: Sababu za Wasafiri Wenye Ujuzi Kuwatumia

  | 3 min read
0
Comments
564

Siku hizi, unaweza ukapanga safari yako kupitia simu. Kuna tovuti nyingi zitakazokuwezesha kununua na kulipia tiketi yako; kuna tovuti zinazotoa maoni kuhusu kusafiri kwenda sehemu mbalimbali pamoja na chaguo za hoteli na migahawa. Pia, kuna blog nyingi zinazohusiana na usafiri.

Sasa, kuna haja ya kutumia wakala wa usafiri tena?

Kwa kweli, inategemea wewe ni msafiri wa aina gani.

Kwenye biashara ya usafiri wa ndege, kuna aina mbili za wasafiri; wasafiri wa kibiashara na wasafiri wa burudani.   Wasafiri wa kibiashara wanasafiri kikazi na hivyo, hawajali gharama sana (kampuni inalipa) ila wanajali muda. Wasafiri hawa hawahitaji wakala wa usafiri.

Ila, kama mwajiri wao anataka kupunguza gharama, wanaweza wakatumia waka wa usafiri.

Msafiri wa burudani anasafiri kwa ajili ya kwenda likizo. Wanajali gharama, furaha na muda sio muhimu sana kwao. Hawa ndio wanaweza wakahitaji msaada wa kitaalamu kupanga safari.

Kwa nini?

Kuna sababu 3 kuu:

1. Uzoefu wa Soko

Kuwa na bei ya chini sio kitu pekee kinachofanya wakala wa usafiri kuvutia wateja. Sana sana, wanavutia wateja kwa maarifa walionao.

Kwa mfano, unaweza ukapata taarifa kupitia intaneti kuhusu madili mazuri ya kwenda kwenye mbuga za wanyama, ila, wakala wako wa usafiri atajua na kukushauri msimu mzuri wa kwenda. Pia ataweza kukwambia kama wana ofa maalum, hoteli bora huko na mengineyo. Maarifa ya wakala wa usafiri itakuongezea starehe.

Pia, tumia wakala wa usafiri mwenye ujuzi maalum ya usafiri unayotaka kufanya wewe. Kwa mfano, kama una mpango wa kwenda kwenye mbuga za wanyama, tumia wakala wa usafiri mwenye ujuzi maalum ya mbuga za wanyama. Zaidi ya kukuchagulia mbuga ya wanyama bora, tayari watakuwa na uhusiano mzuri na wa muda na makampuni ya tours na hoteli. Hivyo, watakusaidia kupata madili mazuri zaidi pamoja na nyongeza nyingine.

2. Unaokoa muda

Pesa ni kitu unachoweza kuongeza, muda sio. Iwapo wakala wa usafiri atakulipisha kwa huduma yake, wanachokurudishia ni muda wako.

Kuna vitu vingi vya kufiria ukipanga safari. Zaidi ya kutumia masaa kadhaa kutafuta tiketi ya ndege kwa gharama nafuu, itabidi:

  • Utafute malazi kwa kila mji/eneo utakalo tembelea
  • Utafute usafiri
  • Ufanye utafiti juu ya vitu vya kubebe vikiwemo hati za usafiri, nguo, fedha na vinginevyo.
  • Ufanye utafiti na upange sehemu za kwenda na kubook mapema, kama unahitaji kufanya hivyo

Kwa hiyo, kwa wengi kupanga safari ndio kinacholeta bugudha kwenye kusafiri. Ila, kazi ya wakala wa usafiri ndio hiyo, kupanga safari yako. Unachohitaji kufanya wewe ni kumueleza wakala wa usafiri wako ni nini unachotaka, alafu umwachie.

3. Okoa Pesa

Kamatulivyosema, wakala wa usafiri wanaijua soko vizuri na wanaweza kukusaidia kupunguza gharama. Wanajua lini ni muda mzuri wa kusafiri na pia, wanaweza wakakupatia dili nzuri kupitia mtandao wao. Vilevile, wanaweza wakakusaidia kupata chumba bora zaidi au kukupatia tiketi za matukio maalum.

Ila, njia kuu ambay wakala wa usafiri anakusaidia kuokoa pesa ni kwa kukupangia safari yenye thamani bora kwa bajeti ulionayo. Unaweza ukapanga safari peke yako na ikawa nzuri au mwachie wakala wa usafiri hiyo kazi alafu upate starehe ya hali ya juu.

Kumbuka kwamba wakala wa usafiri wanataka uwatumie tena na tena na pia wanataka uwapendekeze kwa familia na rafiki zako – kwa hiyo, watajitahidi kuhakikisha wanakusaidia kukupatia safari bora kwa bajeti yako.

Kusafiri bila kuwa na wasiwasi wowote ndio vizuri

Wasafiri wa burudani wanataka starehe. Ukitumia pesa yako binafsi na hutaki kupoteza muda ukiwa hujaridhika na chaguo ya malazi au usafiri au chochote kile.

Kwa hiyo, kwa nini usimuachie mtu mwingine wasiwasi huo aifanyie kazi? Tumia wakala wa usafiri alafu safiri kwa raha kamili.

Tafuta wakala wa usafiri atakayekufaa hapa!

Iman Lipumba
A digital storyteller, experienced in creating content that improves website visibility on search engines, enhances the user experience, and nurtures brand loyalty. With a background in the social sciences, an expert in researching complex ideas, and communicating them in engaging language to multiple audiences.