Wakala wa Nyumba na Malazi: Faida za Kuwatumia

  | 3 min read
0
Comments
506

Kwa maisha ya kisasa, kwa kuwa karibia kila kitu kinapatikana kwenye intaneti, hii inaturahisishia sisi kujihudumia wenyewe. Kwa mfano, ukiingia YouTube tunadhani kwamba unaweza ukafundishwa namba ya kutengeneza kompyuta, kuremba keki na hata kununua nyumba.

Kwa hiyo, unahitaji wakala wa nyumba na malazi wa nini ukiwa una nunua au unauza mali?

1. Okoa muda yako

Pengine we ni mwajiriwa wa kudumu na kutafuta au kuuza nyumba ni kazi ziada. Ila, kazi ya wakala wa nyumba na malazi ndio hiyo.

Hii ina maanisha kwamba kazi zote za shughuli hii zikiwemo kuwasiliana na wanunuaji na wauzaji, kuwauliza maswali, kulinganisha bei n.k wanzifanya wao. Kazi yako itakuwa kuangali nyumba na kuamua untaka ipi.

2. Wana maarifa ya soko

Japokuwa unaweza kutembelea tovuti kama ZoomTanzania na kupata wastani wa bei za nyumba zinazouzwa maeneo mbalimbali, huwezi ukamzidi mtu/kampuni yenye ujuzi huu kwa muda mrefu kama wakala wa nyumba na malazi. Pia, nyumba zinazotangazwa kwenye maeneo ambayo sio maarufu sana huwa hazipo kwenye tovuti za matangazo, kwa hiyo kupata wastani wa bei zaoni ngumu.

Bahati nzuri, wakala wa nyumba na malazi atakuwa ana mtandao wa nyumba nyingi sana kwenye maeneo mengi zaidi. Kwa hiyo, wataweza kukwambia kwa nini bei zinatofautiana kati ya eneo na eneo. Pia, wataweza kutabiri kama bei/kodi zitapanda au zitashuka kadri maendeleo yanavyokuja. Utathamini maelezo yao sana hasa ukiwa unaamua kununua, kodi au kuuza.

3. Fanya makubaliano kwa kujiweka kwanza

Watanzania wengia wamezoea kufanya manunuzi kwa makubaliano ya bei na muuzaji. Sasa, ikija kwenye swala la sehemu ya kuishi, inabidi ufikirie zaidi ya bei ukija kwenye makubaliano.

Wakala wa nyumba na malazi mwenye uzoefu atajua namna ya kukubaliana bei pamoja na kukubaliana juu ya vitu vingine kama umeme na maji (kwa wanaokodi), gharma za uhamiaji, parking, ulinzi, matengenezo – chochote kile!

Ila, watu wanaotaka kununua nyumba wanabidi wachague wakala wao kwa umakini, asije akakubali bei/kodi inayomfaidi yeye zaidi yako.

4. Jilinde kisheria

Watapeli wapo na wapo wengi.

Wote tumeshawahi kuambiwa kuhusu mtu aliyeuziwa kiwanja lakini akajakujua kwamba kiwanja hiyo ni ya mtu mwingine, au ni mali ya umma au kwamba huruhusiwi kujenga hapo.

Wakala wa nyumba na malazi watakusaidia kuandaa hati zotezinazohusika na manunuzi au mauzo ya mali, malipo ya kodi, mkataba wa nyumba n.k Hii ni Baraka kwa kuwa kusoma hati yoyote ya kisheria ni ngumu kwa wengi.

5. Wanajali kile unachojali

Iwe bwawa la kuogelea, baraza au bustani, wengi wetu tuna vitu maalum tunavyotaka tukiwa tunataka kununua au kukodi nyumba/apartment. Wakala wa nyumba na malazi atakupatia sehemu nyingi za kuchagua, mradi mahitaji yako zinaendana na bei/kodi zilizopo.

Mwisho wa siku, wakala bora atakujali na atakuwa makini na vitu unavyotaka (iwe kutumia pesa kutangaza mali yako au kwenye kufanya makubaliano), ili akupatia dili bora.

Maelezo ya undani ndio muhimu

Inawezekana kwamba ukapenda nyumba mara moja, ila wakala wako atakuwa makini na mahitaji yako. Rangi imebabuka? Kuna kutu? Kuna mwanga wa kutosha? Vitu vyote hivi vinaweza vikafanya nyumba yako iwe nzuri au mbaya sana.

Kwa hiyo, iwapo unaweza kutafuta nyumba peke yako, kuwa mtaalamu pembeni yako itarahisisha mchakato mzima na matokeo yatakuwa bora zaidi.

Tafuta wakala wa nyumba na malazi atakaye kufaa kupitia ZoomTanzania

Iman Lipumba
A digital storyteller, experienced in creating content that improves website visibility on search engines, enhances the user experience, and nurtures brand loyalty. With a background in the social sciences, an expert in researching complex ideas, and communicating them in engaging language to multiple audiences.