Viwanja – Namna ya kuzikagua Tanzania

  | 3 min read
0
Comments
687

Ukimiliki kiwanja, ikakaa ndani ya familia kizazi baada ya kizazi. Ni njia bora ya kuwekeza maishani.

Ubaya ni kwamba unaweza ukatapeliwa vilevile. Kuna changamoto zingine pia kama kujenga nyumba yako kwenye hifadhi ya barabara, kuuziwa kiwanja cha umma au kushindwa kufuata kanuni.

Ila, changamoto hizi zisiwe sababu ya wewe kutokuwekeza kwenye viwanja. Inabidi uwe makini kwenye ukakuzi kabla ya kununua.

Orodha hii itakusaidia kufanya hivyo

Usisahau gharama za ziada:

Kabla ya kuanza inabidi ujue kwamba kuna gharama zaidi ya ile ya kununua kiwanja. Inabidi ukumbuke:

 • Malipo ya wanasheria
 • Malipa ya ukaguzi
 • Malipo ya kuunganishiwa umeme, maji n.k
 • Uchimbuaji
 • Kodi za nyumba
 • Bima ya nyumba

Haya yote yatakusaidia kukulinda na utapeli na faini ukimiliki kiwanja. Kwa hiyo, usizisahau!

Msawala ya Kisheria:

Inawezekana kwamba hii ndio swala muhimu kuliko yote kwenye mchakato wa kununua kiwanja. Hakikisha kwamba maswala yote ya kisheria yamekamilika na kwamba umejilinda vya kutosha. Nenda na wakala wa nyumba na malazi kukagua kiwanja alafu hakikisha anauliza:

 • Mipaka ya kiwanja yanaonekana vizuri?
 • Unaweza kujenga ukuta wako kwa ukaribu gani na barabara?
 • Hati za nyumba zimekamilika?
 • Kisheria, unaruhusiwa kujenga aina ya nyumba/jengo unayotaka kujenga kwenye eneo hiyo?
 • Unaweza kujenga kwenye kiwanja hiyo?
 • Hiyo kiwanja ilikuwa inatumika kwa ajili gani?
 • Kunafurika?
 • Utapewa haki zote za maji na madini?
 • Kuna wanyama yoyote yanayolindwa kwenye kiwanja hiyo?

Maswala ya Ujenzi:

Kwa watu wengi, lengo la kununua kiwanja ni kujenga. Nenda na mtaalam wa ujenzi ukienda kukagua kiwanja. Ni muhimu wajue kama:

 • Kuna nafasi ya vifaa vya ujenzi
 • Udongo unamatatizo yoyote?
 • Eneo hiyo inapata mafuriko?
 • Kuna milima au mabonde?
 • Kuna sehemu za mmomonyoko zinazohitaji kusawazishwa?

Maswala ya Kuishi

Fikiria maisha yako yatakuwaje ukiishi hapo:

 • Majirani wakoje? Tabia zenu zinafanana?
 • Kuna umbali gani na ofisini/mjini/familia?
 • Kuna maduka, migahawa, shule, baa n.k ya karibu?
 • Kuna kelele sana au kuko kimya sana?
 • Kuna harufu mbaya kutoka kwa mashamba, maji taka n.k?

Hakikisha una watu unawahitaji karibu nawe

Kuna mambo mengi ya kuzingatia ukiwa unakagua kiwanja/viwanja. Na ni vizuri kuwa na mtaalam/wataalam pembeni yako kukusaidia na ukaguzi.

Wakala wa nyumba na malazi anaweza akawa na maarifa kuhusu kanuni na mikataba ila hatudhani kwamba watukuwa na ujuzi kujua kama udongo unamatatizo. Vilevile, mtaalam wa ujenzi anaweza akakuambia kinachoweza kujengwa kwenya kiwanja hiyo ila atashindwa kuandaa mkataba kitakacho kulinda na utapeli.

Kwa hiyo, kuhakikisha kwamba una wekeza vizuri, nenda na wakala wa nyumba na malazi, mtaalam wa ujenzi na orodha hii ukiwa unakagua kiwanja.

Iman Lipumba
A digital storyteller, experienced in creating content that improves website visibility on search engines, enhances the user experience, and nurtures brand loyalty. With a background in the social sciences, an expert in researching complex ideas, and communicating them in engaging language to multiple audiences.