Miji: Vitu vya kujua kuhusu Kilimanjaro

  | 4 min read
0
Comments
2423

Jiografia

Kilimajaro ina idadi ya watu chini kidogo ya 2m. Ni nyumbani kwa Mlima Kilimanjaro na iko mpakani na Tanga (kusini), Manyara (kusini magharibi), Arusha (magharibi) na Kenya kaskazini.

Ni moja kati ya mikoa mikubwa nchini. Ina wilaya 7 – Siha, Hai, Rombo, Moshi Mjini, Moshi kijijini, Mwanga na Same. Makau makuu yake yako Moshi Mjini.

Wachagga na Wapare

Wachagga na Wapare ni kabila kuu za Kilimanjaro. Wachagga wengi wapo Hai, Moshi, Rombo na Siha. Hii ni kwa vile wachagga waliweka makazi yao katika maeneo haya. Mwanga na Same ni sehemu za wapare zaidi.

Wachagga ni kabila ya tatu Tanzania kwa ukubwa. Waliweka makazi yao kwenye mteremko wa mlima Kilimanjaro na sehemu za jirani. Wachagga wanajulikana kwa uwezo wao wa kufanya biashara. Hii ndio imewapeleka kote nchini na kuwapa umaarufu.

Zaidi ya hapo, kwa kuwa hali ya hewa ya Kilimanjaro imependekeza kilimo kwa vizazi. Wachagga wametumia hali ya hewa hiyo kuweka mifumo ya umwagiliaji, uwekaji mbolea na matuta kwenye juhudi zao za kilimo. Ila, kwa kuwa walikuwa moja kati ya kabila za kwanza kuwa wakristu, walipendelewa kwa kuwa na elimu na huduma za afya bora zilizokuja na wamishonari.

Kama 90% ya kabila za kitanzania, kabila ya wachagga ni mfumo dume. Ila, siku hizi wanawake wamekuja juu na kujiendeleza sana. Katika familia vingi siku hizi, wanawake ndio wenye mchango mkubwa kwa mapato ya kifamilia.

Haya, twende kwa Wapare

Wapare walikuwa wazalishaji wazuri wa chuma, ambayo yalihitajika na majirani yao wachagga. Wakawa wahunzi bora katika maeneo hayo.

Pia, walijihusisha na siasa mapema kuliko kabila nyingi sana. Umoja wa Wapare uliundwa 1946 na ulikuwa moja kati ya harakati za kizalendo Tanganyika dhidi ya ukoloni wa Waingereza. Kadri ilivyokuwa, ikajiunga na Tanganyika African National Union (TANU)

Kiuchumi, chai, kahawa na mkonga zinazalishwa kwa wingi na wapare. Kilimo ya bidhaa hizi imechangia maenedeleo ya eneo hii kwa sana. Ukiwalinganisha na wilaya zingine, Wapare wamejiendeleza kimiundombinu ukiangalia barabara, upatikanaji wa umeme, uunganishaji wa simu na upatikanaji wa maji.

Chakula na Vinywaji vya Kila Siku

Ndizi. Ndizi. Ndizi! Ziwe zimepikwa na mchuzi, za kukaanga, za kuponda (mtori) au za kuchoma, wachagga wanakula ndizi. Nyama, hasa ya ng’ombe na mbuzi, ni muhimu sana. Zadi ya hapo, wachagga wanapombe ya iitwayo Mbege.  Inatengenezwa na ndizi kwa siku 5 au 7 na inapendwa sana.

Mlo kuu ya wapare ni Makande kiungo kikuu ni mahindi na ina maharage nyekundu, vitunguu, nyanya, kitunguu saumu na supu ya kuku zikipikwa kwa pamoja. Siku hizi, Makande inajulikana na kupatikana kote nchini.

Zaidi ya vyakula hivi utakuta, wali, chips na ugali. Pia, Mutura, ambayo ni nyama ya kusaga iliyowekwa ndani ya utumbo na kuandaliwa na kuchomwa kama soseji, imepata umaarufu hivi karibuni. Inapatikana kwa wingi zaidi Moshi mjini.

Moshi

Ofisi zote kuu za kiserikali za Kilimanjaro zipo Moshi mjini. Pia, rais ana nyumba yake ya kulala akiwa amefikia huko. Zaidi ya hapo, biashara zote na maeneo bora ya burudani yapo Moshi mjini. Zaidi ya hapo, ni nusu saa kutoka uwanja wa ndege wa Kilimanjaro (KIA) na lisaa limoja kutoka Arusha.

Moshi kumeendelea zaidi ya maeneo mengine Tanzania kwenye swala za ujuzi wa kusoma na kuandika, na elimu. Kila wilaya ina shule iliyoanzishwa na jamii yake. Pia kuna vyuo vingi vya elimu ya juu.

Huduma ya afya nayo iko katika hali nzuri. Kilimanjaro Christian Medical Centre (ikiwa na shule ya Kilimanjaro Clinical Research Institute) pamoja na Mawenzi Regional Hospital ni hospitali kuu, zote zikiwa ndani ya manispaa ya moshi.

Pia, utalii ulioletwa na Mlima Kilimanjaro umechangia sana kwenye uchumi wa wilaya hii.

Kitu kingine wakazi wa Moshi wanacho jivunia ni usafi wake. Moshi ni moja kati ya miji misafi Tanzania na wenyeji wake wanajitahidi kuendeleza usafi huo, wakiendelea kupanda miti na kutotupa matakataka hovyo hovyo.

Sehemu yenye uwezo

Kilimanjaro bado unakuwa lakini ni moja kati ya mikoa yanayoongoza kwa maendeleo Tanzania. Ilipata manufaa ya kihistoria na ikazitumia. Moshi ilipaswa iwe imejiendeleza zaidi, ila, inaanza kuamka. Hata hivyo, Kilimanjaro kunafaa kutembelewa.

Iman Lipumba
A digital storyteller, experienced in creating content that improves website visibility on search engines, enhances the user experience, and nurtures brand loyalty. With a background in the social sciences, an expert in researching complex ideas, and communicating them in engaging language to multiple audiences.