Vitu vya kubeba ukienda Ufukweni

  | 3 min read
0
Comments
1621

Kujipumzisha ufukweni ukiwa na kitabu kizuri na kinywaji baridi ni raha sana.

Kwa bahati nzuri, Tanzania ina fukwe nyingi sana ambazo ni mazuri kwa ajili ya kwenda likizo.

Ingawa joto, upepo pamoja na ubora wa huduma kwenye hoteli au malazi mengine utakayo kuwa umefikia zitaamua kama  utafurahia likizo yako, pia unachobeba inaweza ikachangia vilevile.

Uzuri na ubaya wa kwenda likizo ni kwamba unaachana na maisha yako ya kila siku, lakini kwa kufanya hivyo hautakuwa na vitu vyako vyote.

Kwa hiyo, kuhakikisha kwamba unabeba vitu vyote utakavyohitaji na kuacha vitu usivyohitaji ni muhimu sana.

Lakini, kabla ya sisi kupendekeza vitu vya kubeba, inabidi ujiulize: ninataka nijisikiaje baada ya likizo hii?

Ni vizuri kutumia likizo yako kupumzisha mwili na akili yako. Usifanye kazi yoyote ya kiofisi. Usibebe vifaa vya umeme kama kompyuta mpakato (laptop) yako, ambazo zinaweza kusababisha ufanye kazi. Ikiwezekana, usiwaze kazi za ofisini kabisa!

Haya, tumekubaliana. Likizo yako ni kumpumzika. Sasa, ubebe nini kukusaidia na hii?

1. Usafi

Kabla ya kuanza kufikiria nguo gani za kubeba, hakikisha kwamba unabeba vile vitu muhimu zitakazokusaidia kuwa msafi na kupendeza, zikiwemo:

 • Vitu vya bafuni (sabuni, mafuta ya ngozi, mswaki na dawa ya mswaki, n.k)
 • Vifaa vya usafi vya kike
 • Vifaa vya kunyoa ndevu kwa wanaume
 • Vipodozi
 • Dawa (paracetamol/panadol, vitamin c, dawa ya kikohozi na dawa yoyote ingine unayohitaji)
 • Mafuta yakukulinda na ukali wa jua
 • Taulo ndogo

2. Nguo

Wakati wengi wetu tunataka kupendeza kupita kiasi tukiwa kwenye likizo, angalia usipitilize. Badala yake, beba nguo zisizokuwa na mahitaji mengi na amabazo zinaweza kuvaliwa kwa mitindo mbalimbali, zikiwemo:

 • Nguo za kuogelea
 • Chupi
 • Nguo za kulalia
 • T-shirt na/au vesti
 • Bukta nyeupe au yenye rangi nyepesi (rangi nzito zinavutia makali ya jua)
 • Nguo za mitoko ya jioni
 • Shati/mashati (kwa wanaume)
 • Skirt nyepesi au maxi dress
 • Jeans
 • Nguo za kufanyia mazoezi
 • Skafu
 • Sweta nyepesi

Shoes

Usibebe viatu vyako vyote. Chagua viatu vya kuvalia fukweni, vya matumizi ya kila siku na vya kuvaa jioni. Kwa hiyo, 3 kwa ujumla:

 • Ndala
 • Viatu vya chini
 • Viatu vya michezo (kama utafanya mazoezi)
 • Viatu vya kuvaa kila siku
 • Boat shoes

3. Vifaa vya Nguo

Vifaa havitajaza sanduku lako lakini vita ongezea kupendeza kwako:

 • Shango
 • Ereni
 • Kofia
 • Miwani ya jua
 • Pochi
 • Begi la kwenda nalo fukweni

4. Burudani

Inabidi ufanye vitu mbalimbali kujipumzisha, zaidi ya kulala, zikiwemo:

 • Kitabu au Kindle
 • Kalamu na daftari
 • Karata na michezo mingine
 • Mpira (ya kuchezea fukweni)
 • Vyakula ndogo ndogo

5. Electronics

Usisahau kubeba hizi vifaa vya umeme muhimu:

 • Chaja ya simu, bettri n.k
 • Kamera

6. Mengineyo

Kama safari yako ya kwenda fukweni sio ya ndege, unaweza ukabeba vitu vingine kama:

 • Taulo za fukweni
 • Mwavuli na viti vya fukweni
 • Cooler Box (mradi inaruhusiwa na sehemu unapofikia)

Kubeba vitu utakavyohitaji ni inasaidia sana

Iwapo unachukua likizo ya kwenda ufukweni, au kutembelea mbuga za wanyama au kuwatembelea bibi na babu kijijini, kujua cha kubeba kitakusaidi sana maishani yako.

Kumbuka, kujua unachotaka kufanya katika likizo yako ndio itaamua ubebe nini na uache nini.

Sasa, kwa kuwa umeshajua nini cha kubeba kwenda ufukweni, tafuta fukwe bora ya kutembelea.

Iman Lipumba
A digital storyteller, experienced in creating content that improves website visibility on search engines, enhances the user experience, and nurtures brand loyalty. With a background in the social sciences, an expert in researching complex ideas, and communicating them in engaging language to multiple audiences.