Vitu vya Kubeba Ukienda kwenye Mbuga ya Wanyama Tanzania

  | 3 min read
0
Comments
1090

Maandalizi yanaweza yakafanikisha au yakaharibu safari yako ya kwenda kwenye mbuga za wanyama. Hutaweza kufurahia uzuri wa wanyawa kama unamaumivu makali ya kichwa kisa, ulisahau kubeba kofia. Pia, hutaweza kuangalia nyota zilizopo angani kama una fukuza mbu kila mara.

Kama vitu vingi maishani, inabidi ufanya maandalizi sahihi ili safari yako iende vizuri. Kumbuka, unaenda kwenye sehemu ambapo sio tu hali ya hewa ni tofauti, lakini pia maisha ni tofauti.

Kwa kifupi, utachobeba kitachangia sana safari yako kuwa nzuri au mbaya.

Mizigo na malazi

 • Sanduku kubwa – litabeba kila kitu utakachotumi kwenye safari
 • Begi nyepisi ya matumizi ya kila siku. Unaweza ukaitumia kubeba maji, glovu, sweta, darubini n.k Kama utakuwa unatembea kwa muda mrefu sana, fikiria kujipatia begi isiyoingia maji
 • Begi la kulala (sleeping bag); Kama utaitumia wakati wa kupanda mlima kilimanjaro, iwe na uwezo wa  -10C mpaka -15C. Kama utaitumia kwenye safari tu, -5C inatosha.

Nguo

 • Sweta
 • Viatu vyepesi vya kutembea
 • Sandal zisizoharibika na maji
 • T-sheti 2 au 3
 • Mashati ya mikono mirefu 2
 • Bukta 2 au 3
 • Suruali 2
 • Mavazi ya kuogolea
 • Chupi na soksi; wanawake wanaweza wakafikiria kubeba sidiria ya michezo
 • Mavazi ya kulala
 • Chupi zenye joto (kwa miezi ya baridi ya Mei mpaka Septemba)
 • Koti nzito (kwa miezi ya baridi ya Mei mpaka Septemba)
 • Skafu/glovu
 • Mavazi ya mvua (kwa msimu wa mvua; Novemba mpaka Mei)

Vitu vya Bafuni

 • Mswaki, dawa ya mswaki na
 • Tissue za Famasi
 • Toilet Pepa
 • Chanuo
 • Pedi
 • Mafuta yam domo
 • Vaseline

Afya

 • Vidonge vya Malaria; hii sio lazima ila inapendekezwa
 • Mafuta ya kuzuia makali ya mionzi ya jua
 • Begi ndogo ya huduma ya kwanza
 • Vidoge vya kupunguza maumivu
 • Diamox (Acetazolamide) kama unapanda mlima Kilimanjaro – Paracetamol
 • Zinc oxide tape na mikasi midogo
 • Pedi za jipu
 • Vidonge vya kuzuia kuharisha
 • Dawa yoyote unayotumia kwa kawaida
 • Paketi zakurejesha hidrati

Hati

 • Pasipoti
 • Visa ya kuingia Tanzania
 • Hati za kusafiri
 • Fedha za kitanzania
 • Credit Kadi (Visa na MasterCard ndio zinazokubaliwa karibia sehemu zote)
 • Hundi za kusafiri hazipendekezwi
 • Hati za bima ya usafiri
 • Vyeti vya chanjo (kama zinahitajika)

Vitu vya Ziada

 • Kamera. Kumbuka kubeba memory kadi za kutosh pamoja na betri na chaja
 • Miwani ya kuzuia jua
 • Vyakula vidogo vya kuongeza nguvu
 • Contact lense za akiba
 • Tochi ya kuvalia kichwani na betri akiba
 • Vyupa vya maji
 • Vidonge vya kusafisha maji
 • Plug za masikioni
 • Begi za plastiki (kwa ajili ya nguo chafu, takataka n.k)
 • Simu ya mkononi – nunua sim card ya kitanzania kupunguza gharama zako za simu.

Tukio lolote nzuri linaanza na maandalizi

Orodha inaonekana kama inavitu vingi lakini wala. Ushaamua kwenda safirini, ni bora kuanza mapema kupanga vitu vya kubeba.

Kumbuka, safari yako ni muda wa kufurahi ni si muda wa kuwa na wasiwasi na ubora wa sleeping bag yako. Kwa hiyo, hakikisha unajiandaa kabla. Tumia orodha yetu na pia fanya utafiti zaidi kama unafikiri utahitaji vitu vingine.

Safari Njema!

Iman Lipumba
A digital storyteller, experienced in creating content that improves website visibility on search engines, enhances the user experience, and nurtures brand loyalty. With a background in the social sciences, an expert in researching complex ideas, and communicating them in engaging language to multiple audiences.