Vitu 7 Vyakufanya Dar Es Salaam

  | 3 min read
0
Comments
1040

Dar es Salaam ni  mji uliyochangamka ikiwa na utamaduni, fukwe, migahawa, baa na mengineyo. Sasa, ukijikuta Dar kwa muda mfupi (kama siku 2 au 3) inaweza ikawa ngumu kuamua ufanye nini na uache nini.

Wasafiri wanatofautiana kwa vitu tunavyopenda kufanya na kuona. Wengi wanapenda mitoko ya usiku wakati starehe ya wengine ni kulala fukweni wakiwa na kitabu na kinywaji. Pia kuna wengine wanaotaka kujifunza utamaduni na historia ya nchi au mji waliyotembelea.

Chochote utakachoishia kufanya, usikose vivutio 7 vifuatayo ambazo zitafanya uikumbuke Dar es Salaam kiukweli.

1. Soko la Samaki Kivukoni

Kwa kuwa Dar es Salaam iko pwani mwa Tanzania, ina vyakula vingi kutoka baharini. Ila, ingawa sehemu nying zinauza chakula kutoka baharini, haitakuwa kama Soko la Samaki Kivukoni. Kwenye soko hii utaweza kuchagua ngizi, pweza, kamba na zaidi; alafu zitapikwa hapohapo mbele yako. Soko la Samaki Kivukoni ina umaarufu mpaka ili tajwa kama “moja ya sehemu za kula kabla ya kufa” na Buzzfeed.com.

2. Makumbusho ya Taifa na Nyumba ya Utamaduni

Kama unapenda historia na unataka kujua zaidi kuhusu historia na utamaduni ya Tanzania, Makumbusho ya Taifa na Nyumba ya Utamaduni ndio sehemu ya kutembelea. Makumbusho haya yanaonyesha mengi yakiwemo urithi wa kikabili, ufundi wa kitamaduni, vifaa vya muziki, sanaa ya kitanzania, historia ya kikolony na ya kisiasa na zaidi. Pia, utaweza kufurahia mazingira mazuri kabisa ya bustani ya makumbusho haya – ambayo pia hutumika kama ukumbi wa harusi.

3. Kijiji cha Makumbusho

Makumbusho, kama inavyoitwa kwa kifupi, itakupeleka ndani ya Tanzania vijijini kwa kuonyesha tofauti ya vijiji vya Tanzania, kabila kwa kabila. Wanabaadhi za nyumba za kiasili ambazo unaruhusiwa kuingia. Jifunze kuhusu ujenzi wao na utamaduni wa watu hao. Pia, unaweza kuangalia wasanii wakifanya uchoraji wa kiutamaduni, michezo ya kiasili pamoja na shughuli zingine za kitamaduni. Kwa kifupi, Kijiji cha Makumbusho itakupa uzoefu wa utamaduni ya Tanzania.

4. Kariakoo Market

Soko la Kariakoo ni soko yenye uhai kuliko zote Dar es Salaam, Kariakoo ni sehemu bora kuliko zote mjini kununua vitu kwa bei nafuu. Wakazi wa Dar es Salaam wanenda kariakoo kununua vyakula, nguo, spea za magari na zaidi. Watalii wanaenda kutafuta zawadi, vitambaa vya kiafrika, nguo za kiasili, viatu na vitu vingine vya kiasili.

Dokezo: Usiogope kujaribu kushusha bei!

5. Kisiwa ya Mbudya

Kama unataka kupumzika fukweni ukiwa Dar, Kisiwa ya Mbudya ndio pakwenda. Kisiwa hii iliyojaa urembo ina mchanga mweupe, maji safi na chakula safi kutoka baharini. Njia rahisi kufika mbudya ni kwa kupanda boti kutoka Jangwani Sea Breeze Resort iliyopo Mbezi Beach, na kawaida hakujai. Kwa hiyo, unaweza kutulia hapo kwa raha zako.

6. Coco Beach

Ukijikuta Dar kwenye wikiendi, hakikisha unafika kwenye fukwe ya Coco ambayo ipo Msasani Peninsula, na onja chakula cha mtaani. Jaribu kula mishkaki na muhogo wa kuchoma. Fukwe ya Coco inapendwa sana na familia au marafiki wa aina zote. Ni sehemu nzuri sana kuangalia jinsi gani jamii ya kitanzania inapenda kujiachia.

7. Kijiji ya Wamakonde, Mwenge

Kama unatafuta sanaa, nguo, viatu, begi, vifaa vya jikoni, chochote kile, utavikuta kwenye Kijiji ya Wamakonde. Eneo lote limetengwa kwa ajili ya kukuza sanaa ya kitanzania. Zaidi ya hapo, mara nyingi wauzaji ndio wasanii wenyewe kwa hiyo wanaweza wakakutengezea kitu cha

kipekee pamoja na kukufundisha juu ya sanaa yao. Kwa kweli, kunafurahisha sana na utaondoka hapo ukithaminikazi ngumu na ujuzi unayohitajika kuwa msanii.

Tafuta sehemu zingine za kutembelea Dar Es Salaam

Kama unapenda shughuli zingine za kufanya ukiwa Dar, tembelea orodha yetu ya biashara kujua migahawa, burudani, matukio na zaidi zilizopo Dar.

Iman Lipumba
A digital storyteller, experienced in creating content that improves website visibility on search engines, enhances the user experience, and nurtures brand loyalty. With a background in the social sciences, an expert in researching complex ideas, and communicating them in engaging language to multiple audiences.