Vitu 10 ambavyo hukujua kuhusu Zanzibar

  | 3 min read
0
Comments
1620

Zanzibar ni kisiwa iliyojaa urembo. Iko pwani mwa Tanzania na watu wengi kutoka sehemu mbalimbali wanaelekea kwenye kisiwa hii kufurahia fukwe, michezo ya maji na vyakula vya bahari vya kipekee.

Ila, watu wachache wanajua yafuatay kuhusu Zanzibar:

1.

Wahindi, waarabu na wa Persia walipagundua Zanzibar kwa kupitia upepo mkali wa Monsoon uliowapeleka hapo.

2.

Kwenye karne ya 19, Zanzibar ilikuwa eneo muhimu ya biashara kwa kuwa ilikuwa njia yakuingia barani Afrika Mashariki. Nchi nyingi zilitaka kuimiliki zikiwemo wapersia, wareno, waoman na waingereza.

Waoman ndio walifanikiwa kuimiliki kwanza na hivyo kuwa wakwanza wa kuendeshe biashara ya watumwa, karafuu na pembe za ndovu. Sultan (mkuu) wa Oman, aliamua kuhamisha nyumba makao yake yakifalme kutoka Muscat kwenda Zanzibar. Zanzibar ikawa nchi ya Kiarabu na muhimu wa biashara na siasa kwenye eneo hii.

Nyongeza: Zanzibar ilipata jina lake kutoka kwa waarabu na maana yake ni ‘pwani ya watu weusi’.

3.

Uislam ndio dini kuu Zanzibar na katika mwezi wa Ramadan, watu wanpendekezwa kuvaa ‘kistaarab’ zaidi.  Ila, makanisa na sehemu za kuabudu za dini zingine zipo.

Idadi ya watu Zanzibar ni 800,000. Ila, 700,000 wanaishi kwenye miji na vijiji vidogo zaidi.

4.

Wazanzibari wanategemea uvu na kilimo sana kwenye uchumi yao. Kuanzia mwanzoni wa karne ya 19, Zanzibar ilikuwa muuzaji wa wa nje mkubwa wa karafuu.

Katika muda hii, uchumi yao ilikuwa inategemea  karufuu kwa kiwango kikubwa. Bado ni hivyo ila siku hizi kuna bidhaa za nazi pamoja na viungo vingine vinavyochangia uchumi.

Ila kwa sasa hivi, utalii ndio kinachoingiza pesa na kuchangia uchumi wa Zanzibar kuliko vyote.

5.

Zanzibar imeunganishwa na visiwa kadhaa – vikubwa vikiwa Unguja na Pemba. Ila, wageni wengi (na wenyeji pia) wanakosea wakifikiri Unguja ndio Zanzibar.

6.

Zanzibar inashika rekodi ya vita vupi kuliko vyote duniani – dakika 38. Vita hiyo ilikuwa kati ya waingereza na wazanzibari na baada ya waingereza kuupiga Beit al Hukum Palace, mpigano yalisitishwa.

7.

Freddie Mercury, kiongozi wa bendi maarufu ya Queen alizaliwa Zanzibar mwaka 1946. Jina lake la kuzaliwa ni Farouk Bulsara.

8.

Zanzibar ilikuwa nchi ya kwanza Afrika kuwa na televisheni za rangi.

9.

Tukio la burudani  la Zanzibar linalojulikana duniani ni Zanzibar International Film Festival. Kila mwaka tukio hii linaonyesha sanaa bora ya utamaduni wa Swahili wa pwani.

10.

Ingawa Zanzibar ni kisiwa ndani ya Tanzania, ina serikali yake yenyewe, inayoongozwa na rais. Rais wake ni Dk. Ali Mohamed Shein.

Wageni wanakaribishwa

Sekta ya utalii Zanzibar umekuwa sana na nitegemeo kubwa ya uchumi wake. Ila, kwa kuangalia takwimu, Zanzibar inapata wageni 100,000 tu kwa mwaka. Ila, kwa kuwa Zanzibar ina vitu vingi vya kuvutia, umeanza kupanga safari yako sasa hivi, au sio?

 

Iman Lipumba
A digital storyteller, experienced in creating content that improves website visibility on search engines, enhances the user experience, and nurtures brand loyalty. With a background in the social sciences, an expert in researching complex ideas, and communicating them in engaging language to multiple audiences.