Vifaa vya umeme 10 unavyohitaji nyumbani

  | 3 min read
0
Comments
4362

Ni ngumu sana kujua mahitaji yako wakati kuna vifaa vingi vya umeme siku hizi. Vilevile, kama unawatoto wanaotaka gemu mpya au iPad, inaweza ikawa ngumu zaidi.

Kwa hiyo, inabidi ujiulize, ‘hivi, ninahitaji nini?’

Tumejaribu kukusaidia na hili kwa kuorodhesha vifaa vya umeme 10 unavyohitaji nyumbani:

1. Kompyuta ya familia

Kompyuta ya familia itakusaidia sana na watoto na wageni.

Kwa mfano, wageni wakija nyumbani na watoto wao, watoto wanaweza wakajiburudisha na michezo kwenye kompyuta. Pia, kompyuta si rahisi kuvunja kama iPad au laptop.

Tafuta kompyuta bora hapa.

2. Laptop

Ingawa ofisi nyingi zinawapa wafanyakazi wao laptop yakutumia, kuwa na laptop yako ni nzuri kwa ajili ya kazi zako za binafsi.

Pia, watu wengi siku hizi wanatumia laptop kuliko tv kuangalia series na sinema.

Tafuta laptop bora hapa.

3. TV

TV ni nzuri wakati familia nzima inataka kuangalia kipindi au sinema maalum, au habari kwa pamoja.

Pia, kama unataka kuwaalika marafiki kuangalia fainali ya mpira kwa mfano, TV itakuwa suluhisho.

Tafuta TV itakayokufaa hapa.

4. Spika

Kwa kifupi, ukitaka kufanya sherehe ya maana nyumbani, spika zenye ubora na za nguvu zitahitajika.

Angalia spika bora zinazouzwa hapa.

5. Taa ya LED ya kubeba

Kwa kuwa umeme wetu unatabia wa kukatika katika, sio wote wenye uwezo wa kununua jenereta au kuweka mifumo ya nguvu ya jua.

Kwa hiyo, taa za LED za kubeba zitakufaa, hasa kwa kuwa zina betri ya kudumu.

6. Microwave

Microwave ina matumiza mengi zaidi ya kupasha chakua. Pia, inauwezo wa kupasha maji, kudefrost nyama na mboga za majani,kupika mayai na mengineyo.

Pitia microwave na vifaa vingine vya jiko.

7. Kamera ya Ulinzi Nyumbani

Kwa ulinzi wa familia, vifaa yako vya umeme na nyumba yako kwa ujumla, usalama wa nyumbani ni muhimu.

Pia itakusaidia kujua kinachoendelea ukiwa haupo.

Tafuta kamera za ulinzi na mifumo yao kwa bei nafuu hapa.

8. Jokofu

Ukizingatia joto la Tanzania, jokofu inaumuhimu sana hasa kwa kuhakikisha chakula hakiozi haraka.

Pitia jokofu za kisasa hapa.

9. Power Bank

Kama taa ya LED hii ni muhimu kwa kuwa umeme sio wakuamini sana. Pia, ni vizuri kuwa nayo ukisafiri.

Jipatie power bank yako hapa.

10. Simu ya mkononi ya ziada

Zaidi ya kuwa na simu yako mwenyewe, ni vizuri ukawa nayo moja ya nyumbani kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na dharura.

Tafuta simu mpya na zilizotumika zenye ubora, hapa.

11. Mfumo wa gemu (X-Box, PS4 n.k)

Siku hizi, hizi sio za watoto tu. Wakubwa nao wanazicheza vilevile na zinauweza wa kuwaburudisha kwa muda mrefu ukiwa na mgeni.

Tafuta mifumo mpya na zilizotumika za gemu, hapa.

Nunua vitu vya kudumu

Kabla ya kununua kifaa chochote cha umeme, fikiria thamani yake kwa maisha yako ya baadaye.

Kumbuka, huna haja yakununua kitu ambacho haitakuwa na faida kwako baaday ya miezi michache.

Tafuta vifaa vya umeme vitakavyo rahisisha maisha yako.

Iman Lipumba
A digital storyteller, experienced in creating content that improves website visibility on search engines, enhances the user experience, and nurtures brand loyalty. With a background in the social sciences, an expert in researching complex ideas, and communicating them in engaging language to multiple audiences.