Vifaa vya Kambi. Vitu 10 Unavyohitaji Ukienda Kambini

  | 5 min read
0
Comments
4756

Ukimuuliza watanzania anafanya nini akiwa likizoni, wengi watasema wanamtebelea familia/wazee kjijini, au wanaenda fukweni, labda wanakaa tu nyumbani na kupumzika au wanasafiri nje ya nchi kwenda Kenya au Afrika Kusini. Mara chache sana utamsikia mtu akisema kwamba anaenda kambini.

Kwa wengi, kwenda kambini ni kama adhabu. Kwa nini uamue kuachana na kitanda, bafu na tv ili uende kulala porini?. Watanzania wengi watakwambia kwamba hizi ni starehe za wazungu – “niache hotelini wakati we ukienda kambini”.

Ila, kwa bahati mbaya watanzania wengi hawafurahii mandhanri mazuri ya Tanzania kama inavyotakiwa. Miji mingi duniani zinaathirikwa na uchafuzi wa mwanga na gesi na kwa mfano, hawawezi kuangalia nyota angani kama unavyoweza kufanya Tanzania. Na hakuna muda mzuri wa kuangalia nyota angani kama ukiwa kambini.

Pia, kuna sababu zingine za kwenda kambini kaka:

 • Ni gharam nafuu: Huhitaji kwenda kwenye kambi ya Serengeti. Kuna kambi nyingi Tanzania za kwenda.
 • Inapunguza msongo: Ukiwa kambini, unalazimishwa kujitenga na maisha na vifaa vyako vyote vya umeme. Matokeo yake ni kwamba unapumzika haswa. Hii inapunguza uzalishaji wa Cortisol mwilini; Cortisol ni homoni inayozalisha msongo.
 • Inaleta furaha: Ukiweza kwenda kwenda kambini na kundi la marafiki na mkabeba vyakula na vinywaji, karata, mpira, vitabu n.k mtafurahia kuwa huko sana. Kwa kuwa mtakuwa umejitenga na mambo mengine, utaweza kufurahia muda wako na wenzako huko kambini, bila kusumbuliwa na vitu vingine.

Dokezo: Usiende kambini na watu usiowapenda.

Haya, si uko tayari kwenda kambini sasa?

Ila kwa kuwa kwenda kambini sio jambo linalofanyika sana Tanzania, watu wengi hawajui namna ya kujiandaa kwenda. Usihofu, tutakusaidia na hilo. Zifuatayo ni vitu 10 utakavyo hitaji kwenda kambini:

1. Hema

Labda uwe na uhakika kabisa kwamba haitanyesha mvua au una mnaenda kwenye kambi inayowapa mahema – ila, utahitaji hema ya kukuzuia na mvua, wanyama pori na wadudu (hasa mbu)

Ukiamua kununua hema, zingatia kwamba kwamba utakuwa unalala karibu na watu ambao utakuwa umeenda nao. Kwa hiyo, ukiwa unanunua hema yako hakikisha ina nafasi ya kutosha. Kama unanunua hema ya kulala watu watatu, bora ununue hema inayotosheleza watu wanne, ili

kuhakikisha kuna nafasi ya kutosha.

2. Begi ya kulalia

Hata kama hutawahi kwenda kambini, begi ya kulalia ni kitu kizuri ya kuwa nayo nyumbani. Inaweza ikasaidia ukienda kulala kwa rafiki yako au ukienda kwenye sherehe kijijini kwa wazee na ukakuta hakuna nafasi ya kutosha.

Ukiwa unanunua begi ya kulalia ya kwenda nayo kambini, zingatia joto au baridi la usiku kwenye kambi unayofikia. Kama joto linapungua sana usiku, hakkisha begi unalopata inhifadhi joto vizuri. Hii itakupunguzia haja ya kubeba mablanketi, ambazo zitakuongezea uzito ukiwa unatembea kuelekea kambini.

Pia, ukijipatia pedi la kulalia itakuongezea faraja ukilala, kama vile uko kitandani kabisa. Kama unataka kulala vizuri na uwe na faraja, hakikisha una begi ya kulali na pedi ya kulalia.

3. Dawa ya Mbu/Dawa za Wadudu

Hakuna kitu kibaya kama kuzungukiwa na mbu alafu huna dawa ya wazuia.

Zaidi ya hapo, fanya utafiti kujua kama kuna wadudu wenye sumu hatari huko kambini na namna ya kujilinda.

Iwapo utakwenda ufukweni au ndani ya Ngorongoro, mbu na wadudu watakwepo tu. Bora ujiandae.

4. Taa

Kutakuwa na giza kali usiku na taa itakusaidia kuona. Pia, kama kuna wanyama pori, itasaidia kuwaweka mbali.

Iwampo utawashamoto au la, utahitaji mwanga zaidi kwa kupitia taa. Taa za LED zinauzwa kwa bei nafuu, zina mwanga mwingi na ni rahisi kutumia. Pia, unaweza kubeba kamba ila uweze kuifunga kwenye mti ili itomwangaza zaidi.

5. Tochi ya kuvalia kichwani

Pamjoa na kuwa na taa, utahitaji chanzo cha mwanga  cha kutembea nacho usiku, hasa ukiwa unaenda kujisaidia, kupika, kupitia mizigo yako au kufanya vitu vingine usiku.

6. Appropriate Clothing

Usibebe jeans au bukta ambazo ni fupi sana. Badala yake, nguo ambazo unapaswa kubeba ni:

 • Mashati ya mikono mifupi nguo zozote za michezo
 • Bukta zenye mifuko mingi
 • Mashati a mikono mirefu
 • Sweta

Pia, kuwa makini sana na vitambaa vya nguo zako. Pamba na sanda ni bora.

7. Manukato

Kwa wengi, usafi ni muhimu wakifiria kwenda sehemu isiyokuwa na bafu au vyoo vya kawaida.

Wakati huwezi kuepukana na kunuka kama hujaoga kwa siku tatu, kuwa na manukato na breath mints itasaidia.

Pia, beba air freshner kwa ajili ya pale ambapo mtu kwenye kundi lenu anajamba. Itatokea tu!

8. Maji na Disinfectant

Hata kama mtapewa maji, hakikisha unabeba maji ya kutosha kwa ajili ya kunywa, kunawa mikono, na kupika. Unaweza ukaambiwa kwamba kunywa maji kutoka kwenye mkondo au maporomoko wa maji ni salama, ila, kama umezaliwa au umekulia mjini, ambapo maji ya chemshwa na kusafishwa, usijaribu kufanya hivyo.

Pia, ukiwa na dawa ya kuua wadudu waliyopo mikononi, hautatumia maji mengi. Ndio, nivizuri kunawa mikono kila unapoenda bafuni, ila kuna wakati chache ambazo unaweza ukatumia dawa ya kuua wadudu mkononi; kwa mfano ukitaka kusafisha mikono yako kabla ya kula.

9. Vifaa vya kutoa Huduma ya Kwanza

Ikiwa umejikwaruza kidogo umejikata vibaya sana, utashukuru kuwa na vifaa vya kutoa huduma ya kwanza.

Unaweza ukanunua vifaa hivi pamoja, ila, inaweza ikawa bora zaidi kuvinuna mojamoja kwa mahitaji yako. Kwa mfano, kama una pumu hakikisha umebeba pampu au dawa yoyote nyingine unayohitaji. Kama unafahamu kwamba unapoteza nguvu kwa haraka, beba glucose.

Vitu muhimu vya kutoa huduma ya kwanza ni:

 • Plasta
 • Tissue za kusafisha vidonda
 • Gauze
 • Gloovu safe
 • Mikasi
 • Vibano
 • Chochote cha kusafishia jicho.
 • Mafuta ya antiseptiki
 • Mafuta ya upele
 • Dawa ya wadudu
 • Dawa za maumivu kama panadol, paracetamol au asprin.
 • Dawa ya kikohozi
 • Maji masafi ya kusafisha vidonda.

10. Tabia Nzuri

Ukienda kwenda kambi unahitaji kushiriki kikamilifu kwenye chochote utakachokuwa umepanga  kufanya, ili muda wako uwe nzuri. Ukiishia kulalamikia wadudu, kutembea, hali ya hewa, ukosefu wa intaneti n.k utajizuia kufurahia na pia unaweza ukawaharibia wengine.

Kwa hiyo, ukiamua kwenda, fanya kweli. Jipatie msisimko. Haitakuwa kama kwenda hotelini ila utakuwa na marafiki wako kwenye mazingira tofauri kabisa – hiyo italeta raha ya aina nyingine kabisa.

Utaenda wapi?

Sasa, kwa kuwa umejua vya kwenda navyo kambini, anza kutafuta kambi bora ya kwenda. Anzia hapa kwa kupitia sehemu 10 bora Tanzania za kwenda kambini. Zaidi ya hapo, tafuta sehemu ya kwenda kambini kabisa kupitia ZoomTanzania.

Iman Lipumba
A digital storyteller, experienced in creating content that improves website visibility on search engines, enhances the user experience, and nurtures brand loyalty. With a background in the social sciences, an expert in researching complex ideas, and communicating them in engaging language to multiple audiences.