Vidokezo vya Kutafuta Kazi kwa Waliomaliza Chuo Kikuu hivi karibuni

  | 3 min read
0
Comments
819

Kama umemaliza Chuo Kikuu hivi karibuni, na huna uzoefu wa kufanya kazi, ajira yako ya kwanza ni ngumu sana kupata. Bahati nzuri, unaweza kufanya vitu mbalimbali kuboresha nafasi yako kuajiriwa.

1. Tafuta nafasi za kazi zinazowalenga watu waliomaliza chuo kikuu hivi karibuni

Njia bora ya kuboresha nafasi yako ya kupata ajira ni kuomba ajira kwenye nafasi ya kazi inayohitaji mtu mwenye sifa zako. Kwa kifupi, usipoteze muda wako kwa kuomba ajira kwenye nafasi za kazi ambazo sifa zake huna.

2. Field, mafunzo na mengineyo yanahesabika kama uzoefu  

Kama ulishawahi kufanya kazi field na ndio uzoefu pekee uliyonayo ya kufanya kazi, basi tafuta njia yakuhusisha uzoefu hiyo na kazi unayoomba. Waajiri wanajali zaidi unachojua na ulichojifunza kadri miaka yalivoenda na namna gani zinaweza kusaidia ofisini.

3. Jisajili na Shirika la Kuajiri

Shirika za kuajiri ni rasilimali nzuri za kuwatafuta waliyomaliza chuo kikuu hivi karibuni. Na ukiwa umefaulu vizuri sana pamoja na kuwa na ujuzi wa kuwasiliana, inasaidia zaidi.

Wana uwezo mkubwa wa kukusaidia kupata ajira unayotaka, kuliko idara za rasilimali watu ambazo zinaweza zikasahau ombi lako la ajira.

4. Tumia mitandao yako

Hakikisha familia yako na marafiki wako wanajua kwamba unatafuta ajira. Waombe wakusaidia kukutaarifu wakiona kazi itakayokufaa au wakiona kampuni inatafuta wafanyakazi.

5. Jaribu kujitolea kufanyakazi kwa kujitolea

Kujitolea kufanyakazi kwa kujitolea ni njia nzuri sana ya kuongeza uzoefu wa kazi. Kitakuongezea sifa na hivyo kufanya uwejuu ya watu wengine wanaotafuta ajira.Pia, itakuuza mtandao wako.

Pamoja na hayo, ukimwambia mwajiri kwamba umewahi kufanya kazi kwa kujitolea inamuonyesha mwajiri kwamba unahamu kufanya kazi, hata pale pasipo kuwa na mshaara au maslahi kwako. Pia, unaweza kusisitiza mambo maalum uliyoyafanya yanayohusika na kazi unayoomba. Kwa mfano, kama ulifanya kazi kubwa ndani ya kundi unaweza kuongelea hili kwa kuwa makampuni mengi yanahitaji mtu anyeweza kufanyakazi mwenyewe na kwenye pia.

6. Ulizia kazi za field

Makampuni mengi yako tayari kumuanzisha mtu kwenye nafasi za field wakiamini kwamba unaakili, una muelekeo na utaongeza thamani kwenye kampuni.

Chagua makampuni utakayopenda kuajiriwa nao alafu ulizia nafasi za kufanya kazi ya field. Kufanya kazi za field itakufundisha mengi kuhusu kazi hiyo, pia kukufanya uwe na soko zaidi kwenye sekta hiyo kwa kupata uzoefu.

Ubora juu ya wingi

Ukitafuta kazi kwa umakini na unaweka juhudi zako zote kwenye maombi ya kazi, pamoja na kufuata vidokezo tulivyoeleza hapo juu pamoja na kutafuta taarifa zaidi, utaanzwa kuitwa kwenye interview hivi karibuni.

Pia, ni muhimu kukumbuka kuomba kazi kwenye nafasi zinazolingana na uwezo na sifa zako. Ombi moja ya uhakika ni bora kuliko ombi nyingi za kawaida na inaongeza nafasi yako kuitwa kwenye interview.

 

Iman Lipumba
A digital storyteller, experienced in creating content that improves website visibility on search engines, enhances the user experience, and nurtures brand loyalty. With a background in the social sciences, an expert in researching complex ideas, and communicating them in engaging language to multiple audiences.