Vidokezo 10 vya Kusafiri Kwa Gharama Nafuu

  | 4 min read
0
Comments
1179

Kwa bahati mbaya, wengi wetu tunaona kwamba kusafiri na fahari ambayo watu wachache wanaiweza.

Kiukweli, kuna vitu kama kodi ya nyumba, ada ya shule na gharama za hospitalini ambazo ni muhimu zaidi ya kusafiri. Ila, kutembelea sehemu tofauti inaweza ikakupa faida nyingi sana. Kwa mfano:

  • Kusafiri inatupanua kimawazo na inatusaidia kujua mapungufu yetu na hata kupata suluhisho zao.
  • Kusafiri inapumzisha akili zetu
  • Kusafiri inatusaidia kukutana pamoja na kupanua mitandao yetu.
  • Kusafiri inasaidia kuhamasisha ubunifu

Kwa hiyo, ni vizuri kutazama kusafiri kama njia muhimu ya kujielimisha na kujijua. Badala ya kulenga fahari, tuwe makini kwa vyote tutakavyo vikuta tukisafiri. Ukiwa na mtazamo huu, huhitaji pesa nyingi kusafiri.

Alafu, tunavidokezo kuthibitisha hii.

1. Iweke kama kipaumbele

Kwa kifupi, kama hutaiweka kama kipaumbele, hautakuwa na pesa ya kutosha kusafiri.

Haya, sasa kazi ngumu ya tenga pesa kwa ajili ya kusafiri ndio kinachofuata.

2. Orodhesha matumizi yako yote alafu toa zote zisizokuwa za lazima

Kuna vitu vingi maishani tunavyofikiri ni za muhimu wakati sio. Tukibadilisha maisha yetu ya kila siku, tunaweza kuhifadhi pesa nyingi. Kwa mfano:

  • Acha kununua chakula cha mchana. Anza kupika nyumbani alafu ibebe.
  • Badala ya kunywa kwenye baa, nunua vinywaji dukani alafu kunywa nyumbani
  • Endesha kwa umakini
  • Kama unatumia pesa kwenda saluni, anza kurekebisha nywele zako mwenyewe nyumbani.
  • Kuwa makini na vitu vidogovidogo vinavyo toa pesa kwako kama vyakula vidogovidogo, soda, kahawa n.k

3. Chagua sehemu ya kwenda yenye gharama nafuu

Kuna nchi kama Ireland, Ufaransa na Ubelgiji ambazo zinahitaji pesa nyingi kuzitembelea. Ila, unaweza kwenda India, Malaysia au South Africa kwa gharama nafuu zaidi:

Hata ndani ya nchi, kuna miji zenye gharama zaidi ya miji mingine. Kwa hiyo, fanya utafiti wako kujua wapi pakutembelea kutegemeana na bajeti yako.

4. Jifunze zaidi kubook ndege kwa bei nafuu

Soma zaidi kuhusu hii, hapa.

5. Tumia AirBnb au mengine kutafuta malazi ya gharama nafuu

Kama bajeti hairuhusu, usilale kwenye hoteli la kifahari. Badala yake, tafuta malazi ya kawaida au kama hosteli au nyumbani kwa mtu. Uzuri wake ni kwamba utajipunguzia gharama pamoja na kujifunza zaidi kuhusu watu na utamaduni wa huko.

6. Tumia usafiri wa kawaida

Kama taxi siyo njia ya usafiri inayotumika zaidi na umma, usizitumie. Badala yake, tumiia usafiri wa umma (mradi ina usalama) au Uber na mengineyo kama yapo.

Kwa mfano, watalii wengi Dar es Salaam wanatumia Bajaji kwa usafiri wa kila siku, kwa kuwa hazina gharama kubwa na unaweza ukazitegemea.

7. Kula chakula cha mtaani

Chakula ni kitu kimoja kikubwa kinachotofautisha utamaduni mbalimbali. Na hakuna chakula cha kiasili kama chakula cha mtaani au chakula kilichopikwa na bibi wa jirani wako. Jaribu kula chakula cha mtaani ya kutosha, ni gharama nafuu kwelikweli!

Kiukweli, ukija Tanzania alafu huli chips maya pamoja na vyakula hivi vya kiasili, utakuwa umekosea sana.

8. Achana na sehemu za kitalii. Nenda kwa wenyeji

Sehemu zilizojaa watalii, huwa zinagharama kubwa zaidi ya sehemu za wenyeji.

Pia, kusafiri kwenda nchi nyingine na kuishia kuwa na watalii wenzako haina maana. Badala ya kuwa na watu kama wewe, wauliza wenyeji sehemu za kwenda.

Note: Ukimuliza mwenyeji, ‘niende wapi?’ atakuelekeza kwenye sehemu za kitalii. Ila, ukimuuliza ‘we unaendaga wapi?’ tunadhani watakuelekeza kwenye sehemu yenye chakula nzuri, bia za ndani na muziki.

9. Pata ajira ukiwa una safari: Fundisha fanya kazi kupitia kompyuta

Kusafiri sio lazima iwe kitu unachofanya mara mojamoja. Unaweza ukaiingiza katika maisha yako ya kila siku kwa kupata ajiri ukiwa umesafiri. Teknolojia imetuwezesha kufanya kazi popote pale tulip mradi tuna kompyuta mpakato (laptop) na intaneti. Kwa hiyo, angalia jinsi ya kutengeneza pesa ukiwa unasafiri.

Njia nyingine ya kutengeza pesa ukiwa umesafiri, ni kufundisha. Jua zaidi hapa.

10. Jifunze lugha ya kiasili

Ukijua misemo na maneno muhimu kwa lugha ya kiasili utaweza kujenga uhusiano na wenyeji kwa kiurahisi zaidi. Hii itakusaidia kukubaliana bei ya baadhi ya vitu pamoja na kupata mapendekezo ya sehemu nzuri za gharama nafuu za kutembelea.

Kwa mfano, ukiongea kiingereza Tanzania, mwenyeji atafikiri kwamba umetoka nje na mapato ya ziada. Kwa hiyo, ukiweza kuongea Kiswahili kidogo itakusaidia sana.

Maisha mazuri ni yale ya kawaida

“Kusafiri inamfanya mtu awe mpole. Unaona kwamba katika dunia nzima, wewe unachukua nafasi ndogo sana” – Gustave Flaubert

Kuna faida nyingi ya kusafiri. Usikate tamaa, utaweza tu!

Pia, unaweza ukakuta kwamba kusafiri kwa bajeti ndogo ina raha zaidi kwa kuwa inabidi ujiingize katika maisha ya kiasili ya huko utakapokwenda, badala na kujihusisha na shughuli za kitalii zaidi ambazo zinaweza zikakupa picha isiyokuwa sahihi ya sehemu uliyotembelea.

Iman Lipumba
A digital storyteller, experienced in creating content that improves website visibility on search engines, enhances the user experience, and nurtures brand loyalty. With a background in the social sciences, an expert in researching complex ideas, and communicating them in engaging language to multiple audiences.