Vidokezo 10 vya Kukusaidia Kudumisha Gari Yako Zaidi

  | 3 min read
0
Comments
4905

Tofauti ya mtu mwenye gari inayotembea kwa zaidi ya miaka 10 na mtu mwenye gari iliyoharibika baada ya miaka 2 ni utunzaji.

Ila watu wengi wanafikiri kwamba kuifanyia servisi ndio kianchohitajika tu kudumisha gari yako. Hii sio kweli.

Kuna vitu ambavyo unaweza kufanya mara kwa mara ili gari yako idumu zaidi.

1. Badilisha mafuta ya injini

Mtu yoyote mwenye gari anajua kwamba kubadilisha mafuta ya injini ni muhimu; inachangia sana kudumu kwa injini.

Faida za kubadilisha mafuta ya injini ni:

 • Inapungusa msuguano kati ya vifaa tofauti vya gari.
 • Inanyonya joto linalotolewa na injini
 • Inapunguza kutu

2. Tunza mfumo wa kuhifadhi baridi

Kwa nchi yenye joto kama Tanzania, mfumo wa kuhifadhi baridi ni muhimu sana kupunguza joto kwenye injini na vifaa vingine.

Hakikisha una:

 • Una fanya chunguzi wa mfumo huo injini ikiwa baridi, tu!
 • Tumia maji ya kupunguza joto ya gari yako, yaliopendekezwa.
 • Changa maji ya kupunguza joto na maji masafi, kupunguza kutu na mengineyo.

3. Usisahau mafuta ya transmisheni

Zaidi ya mafuta ya injini, mafuta ya transmisheni ni muhimu pia na ni vizuri kuichunguza mara kwa mara. Ila, ni bora fundi wako aiangalie. Akiwa anaiangalia, hakikisha ana:

 • Weka kiwango cha mafuta ya transmisheni kinachohitajika. Asizidishe!
 • Angalia kama haijaungua au rangi yake imebadilika
 • Tumia aina ya mafuta iliyopendekezwa na mwongozo wa gari yako.

4. Badilisha maji ya breki

Kubadilisha maji ya breki mara moja kwa mwaka ni vizuri kuzitunza na hivyo, kujipa usalama zaidi ukiwa unaendesha. Kama huna uzoefu na magari sana, mwachie fundi wako kazi hii.

5. Grisi ni bora

Kifaa chochote cha gari yako kinachotembea au yenye vitu vinavyotembea inabidi iwe na grisi ya kutosha.

6. Usafi

Zaidi ya kuweka umuhimu kwenyeusafi wa sehemu zinazonekana kiurahisi, tunasahau kusafisha chini ya gari. Kwa kuwa kuna vumbi, mchanga na udongo mwingi Tanzania, hii ni muhimu sana. Ipeleke gari yako kuoshwa kwa chini mara moja kwa mwezi au zaidi.

7. Tunza rangi ya gari

Kubadilisha rangi ya gari yako ni ghali, ila kuipiga laka ni gharama nafuu zaidi. Hii italinda na kudumisha rangi ya gari yako kwa muda mrefu zaidi, pamoja na kuipa mng’ao.

8. Ilinde na jua

Joto na mionzi ya jua yanachangia kuharibika kwa rangi na muonekano wa gari yako kwa nje. Pia, zina uwezo wakuharibu plastiki ndani ya gari. Ilinde gari yako na jua popote panapowezekana kufanya hivyo.

9. Ukubwa wa matairi yako ni muhimu

Pata ushauri kutoka kwa mwongozo wa gari yako kuhakikisha matairi yako yana ukubwa unaohitajika na presha sahihi. Hii itaisaidia kutembea kwa usalama zaidi na kupunguza gharama za mafuta. Pia, itazisaidia kudumu zaidi.

10. Endesha vizuri

Hakikisha una:

 • Tunza breki zako kwa kutosimama haraka na ghafla
 • Usiendeshe kwa kasi sana kama huna gari yenye nguvu nyingi
 • Usiweka mafuta yasio sahihi kwa gari yako
 • Panda matuta polepole. Ukiyapanda kwa kasi unaweza kuharibu vifaa vya ndani ya injini.

Jifunze kutoka kwa mtaalam

Mwombe fundi wako awe anakufundisha jinsi ya kuangalia hivi vitu vidogo vidogo tulivyoelezea.

Usihofu, kama huna fundi maalum, kuna chaguo nyingi za fundi hapa.

Iman Lipumba
A digital storyteller, experienced in creating content that improves website visibility on search engines, enhances the user experience, and nurtures brand loyalty. With a background in the social sciences, an expert in researching complex ideas, and communicating them in engaging language to multiple audiences.