Viatu – Aina ya Viatu Wanawake Wanavyohitaji

  | 2 min read
0
Comments
8056

Sana sana, wanawake wananunua viatu kulingana na mitindo,  kwa kuwa wanazipenda tu au kwa ajili ya mavazi maalum. Ila, wengi hawanunui viatu kulingana na mahitaji yao.

Kwa ujumla, wanawake wanahitaji viatu vya aina 9 kwa tukio lolote lile, zikiwemo yafuatayo:

1. Flat pumps/ballet flats:

Viatu hivi vina faraja sana na zinapendeza. Zinafaa kwa matumizi ya kila siku, kazini, sherehe n.k

2. Black kitten heels:

Viatu hivi vinafanya miguu yako yaonekane mirefu zaidi bila kushangaza.Zinafaa kuvaliwa kwenye mazingira ya kikazi au kwenye mtoko wa usiku.

3. Malapa

Unahitaji malapa kwa ajili ya kwenda ufukweni, ukienda kumtembelea rafiki yako na sehemu zingine zisizokuwa na shamra shamra.

4. Casual bootie

Buti hazivaliwa kwenye maeneo yenye baridi tu. Bootie ya kawaida au ya anka inaongeza kitu fulani kwenye mavazi kama jinzi kwa mfano.

5. Wedges za rangi ya Tan or Brauni

Kama unataka kuvaa viatu vya juu vinavyoongeza urefu wa miguu yako lakini pia, zinazofaa kuvaliwa fukweni, wedges ndio zenyewe. Zinapendeza na hazina muonekano kwa kirasmi zaidi.

6. Oxford Shoes:

Kama unataka viatu vya kukufanya uonekane kama fashionista, viatu hivi vitasaidia. Zinafaa kuvaliwa kazini na kwenye sherehe za hapa na pale.

7. Raba

Hapa hatumaanisha raba za kufanyia mazoezi, lakini yale yakuvaa na mavazi ya kawaida kama jinzi na t-shirt au ukiwa unapumzika na wenzako kwenye baa ya kawaida

8. Statement Heels

Iwe zinang’aa, zenye rangi tofauti n.k. kili mwanamke anahitaji pea moja ya viatu visivyo vya kawaida kabisa! Zisiwe chini ya inchi 4. Zinafaa kwa ajili ya mtoko maalum au sherehe ambayo unataka macho yote yame yanakuangalia wewe.

9. Nude heels

Hizi zinaendana na vazi lolote ile na aina pekee ya viatu virefu vinayofaa mazingira yalirasmi na yasiorasmi.

Usinunue kiatu isiyokuwa na ubora

Bora uwe na viatu chache vya ubora wa hali ya juu kuliko kuwa na viatu vingi vyenye ubora wa chini utakazo ishia kutupu kila baada ya miezi mitatu.

Kutupa na hivyo kulazimika kununua viatu mara kwa mara itakuwa gharama kubwa kwako pia.

Anza kutafuta viatu sasa hivi kupitia ZoomTanzania!

Iman Lipumba
A digital storyteller, experienced in creating content that improves website visibility on search engines, enhances the user experience, and nurtures brand loyalty. With a background in the social sciences, an expert in researching complex ideas, and communicating them in engaging language to multiple audiences.