Uzima – Jinsi ya Kuanza Kufanya Mazoezi Ukiwa Mvivu

  | 2 min read
0
Comments
4757

Watu wengi wenye mafanikio huwa wanafanya mazoezi. Unajua kwa nini?

Kwa vile, uzima wa akili na uzima wa mwili zinaendana.

Kiukweli, kufanya mazoezi kwa daka 30 kila siku sio nyingi lakini wengi tunashindwa kufanya hivyo. Kwa hiyo, tutakupa vidokezo vya kuwasaidia kuanza na kuacha kusema ‘nimechoka’ au ‘siwezi’.

1. Punguzu mategemeo yako

Usitegemee kwamba baada ya muda kadhaa utakuwa kama The Rock. Badala yake, kuwa na lengo la kuongeza pumzi. Jitahidi kufanya mazoezi kwa nguvu zote kwa dakika 30 na baada a hapo, ongeza mazoezi mengine ya kuongeza misuli n.k.

2. Tafuta namna ya kufanya mazoezi kwa furaha

Gym haimfaii kila mtu, ila hiyo sio sababu ya kutofanya mazoezi. Kucheza michezo ni mazoezi, kutembea kwa mwendo wa maana kwa dakika 30 ni mazoezi pia.

 

Kwa hiyo, badala ya kwenda gym, unaweza ukafanya yafuatayo:

  • Kutembea mtaani kwako
  • Dvd za mazoezi
  • Kucheza muziki
  • Kuendesha baisikeli
  • Kuruka kamba
  • Kukimbia kwenye ngazi

3. Jipatie mwalimu

Kuomba msaada sio kitu kibaya! Kwa hiyo, kama utaamua kujiunga na gym, mwombe moja wa wasidizi awe mwalimu wako. Kama utafanya mazoezi nyumbani, tumia dvd za mazoezi au video za mazoezi kwenye intaneti zenye waalimu.

4. Jizawadishe

Kama umeweza kufanya mazoezi siku ambayo hukujisikia kufanya mazoezi kabisa, jizawadishe na kitu kidogo.

Kwa kifupi, kujizawadisha kadri unavyoendelea kufanya mazoezi kutakusaidia.

5. Ondoa vizuizi vyote

Jiandae kufanya mazoezi masaa kadhaa kabla kufanya mazoezi. Kwa mfano, kama utafanya mazoezi asubuhi, hakikisha nguo zako ziko tayari kabla ya kwenda kulala.

Pia, jiulize:

  • Kama unapenda kufanya mazoezi asubuhi au mchana
  • Ni muda gani ambayo una nguvu sana?
  • Ungependa kufanya mazoezi na mwenzako?

6. Tengeneza ratiba yenye vichochezi

Usitegemee tu kuwa na motisha siku zote. Ila, jiwekee vichochezi vya kufanya mazoezi. Kwa mfano, kabla ya kwenda kulala weka nguo zako za mazoezi sehemu ambazo zinaonekana kukukumbusha kwamba inabidi ufanye mazoezi kesho na pia, ili usizisahau.

7. Kumbuka lengo kuu ya mazoezi

Lengo la kufanya mazoezi si kutunisha misuli mbele ya watu ukiwa fukweni, ni kujenga afya yako. Hii ndio lengo kuu na si yakusahau. Faida zote zingine zitakuja baadaye.

Jiandae kushinda.

Usitegemee kuona mabadiliko ghafla baada ya kufanya mazoezi kwa siku moja, wiki au hata mwezi. Mabadiliko yatachukua muda ila yatakuja. Ila, we weka malengo yako kwenye kuwa na ratiba ya mazoezi na kuifuata.

Iman Lipumba
A digital storyteller, experienced in creating content that improves website visibility on search engines, enhances the user experience, and nurtures brand loyalty. With a background in the social sciences, an expert in researching complex ideas, and communicating them in engaging language to multiple audiences.