Usalama Barabarani – Vitu vya Kufanya Baada ya Ajali

  | 2 min read
0
Comments
4980

Waendesha magari, bodaboda, bajaj na daladala wengi wanaendesha kwa kasi na kutozingatia usalama barabarani. Na hivyo, ajali nyingi zinatokea.

Ila, unaweza ukawa dereva mzuri anayefuata sheria za barabarani na bado ukapata ajali. Kwa hiyo ni muhimu kujua chakufanya ukihusika kwenye ajali.

1. Simama

Haijalishi kama wewe ndio aliyesababisha ajali, inabidi usimame. Ukitoa gari lako kutoka kwenye eneo ya ajali unapoteza ushaidi atakaotumia polisi akiwa anafanya tathmini. Pia, usijaribu kukimbia kwa kuwa unaweza ukafukuzwa au kupatikana baadaye kwa kutumia namba ya gari na adhabu yako ikawa kali zaidi.

Ila, ni kawaida kwa watanzania kufurika kwenye eneo la ajali na kuleta fujo kwa hiyo, hapo ukiamua kukimbia kitaeleweka. Alafu, bora ukimbilie polisi au uwaite hapohapo baada ya ajali kutokea.

2. Jua hali ya watu wote waliohusika kwenye ajali

Hali ya wote waliohusika kwenye ajali ndio swala muhimu kuliko zote.

Kama kuna majeruhi, wapigie polisi mara moja na pia, gari la kubeba wagonjwa iitwe. Kama gari la kubeba wagonjwa inachelewa, bora uwapeleke wote walioumia hospitalini.

3. Toa maelezo kwa trafiki

Msubiri trafiki polisi kufika. Akifika, mueleze kilichotokea kwa undani. Toa gari lako katika eneo la ajali pale tu atakapo kuruhusu. Pia, piga picha za ajali. Unaweza ukazihitaji baadaye kwenye maswala ya kisheria au na bima.

Pia, mwache polisi aamua nani aliyesababisha ajali. Ndio kazi yake. We usichukue lawama kabla. Unaweza ukafikiri makosa yalikuwa ya kwako na ukakuta dereva wa hiyo gar lingine alikuwa amelewa, kwa mfano.

4. Ipigie kampuni yako ya Bima

Toa taarifa kwa kampuni yako ya bima hapohapo ukiwa kwenye eneo la ajali. Watakujulisha mahitaji yao kutoka kwako na polisi ili kuanza mchakato wao wa kukulipa.

Hakikisha una:

  • Jina kamili la dereva wa gari la pili, annuani yake, namba ya simu pamoja na jina ya kampuni yake ya bima na akaunti namba.
  • Namba ya usajili na aina ya gari ya hiyo gari la pili.

Mwanasheria anaweza akasaidia

Ajali huwa zinaleta wakati mgumu kwa namna moja au nyingine. Ila, ukifuata maelekeo yetu, zitakusaidia. Ila, ni vizuri pia ukiwa na mtu wakupa ushauri wa kisheria baada ya ajali. Bahati nzuri, tuna orodha bora ya wanasheria Tanzania wanoweza kukusaidia.

Ila, kujikinga ni bora zaidi ya kuwa na tiba. Kuwa makini barabarani.

Iman Lipumba
A digital storyteller, experienced in creating content that improves website visibility on search engines, enhances the user experience, and nurtures brand loyalty. With a background in the social sciences, an expert in researching complex ideas, and communicating them in engaging language to multiple audiences.