Unaijua Tanzania Vizuri? Ukweli 10 za kukufurahisha kuhusu Tanzania

  | 2 min read
0
Comments
784

Ndio, tunajua kwamba Kilimanjaro iko Tanzania na tuna wanyama wengi nakadhalika, nakadhalika.

Ila, ni vitu gani ambavyo hatujui kuhusu Tanzania? Hivi hapa:

1.

Mbao kutoka kwa mti wa Mpingo unaopatikana Tanzania ni mbao ghali kuliko zote Tanzania.

2.

Wimbo wa taifa wa Tanzania ni sawa na nyimbo za taifa za Afrika Kusini na Zimbabwe. Zilitungwa na Enock Sontonga, aliyetoka Afrika Kusini.

3.

Lake Manyara ni sehemu pekee duniani ambapo utaona simba zinazo panda miti.

Panga safari ukawaone!

4.

Watanzania wengi hawamjui Freddie Mercury, ambaye alikuwa kiongozi wa bendi ya Queen. Zaidi ya hapo, hawajui kwamba alizaliwa Zanzibar na jina lake halisi ni Farrokh Bulsara.

5.

Rais Julius K Nyerere alikuwa mtanzania wa kwanza kusoma Uingereza na wa pili kupata shahada kutoka chuo cha nje.

6.

Mwaka 2015 ni mwaka ambao Tanzania ilikuwa nchi ya kwanza chini ya Sahara kuweka Swahili kama lugha kuu mashuleni.

Kwa kuwa Tanzania ina zaidi ya kabila 120 na lugha asili 130, Kiswahli kimechangia sana kwenye kujenga umoja kati ya wananchi. Lugha hii imeundwa na maneno ya Kiarabu, Bantu, Kiingereza na Kijerumani.

7.

Mgombea urais mwaka 2015, Edward Lowassa, alikuwa mtanzania aliyetafutwa zaidi kwenye Google mwaka huo.

8.

Tanzania ina msongamano mkubwa wa wanyamwa kwa kilometa za mraba duniani.

9.

Kito johari ya Tanzanite inapatikana Tanzania tu! Ni kati ya vito johari 3 duniani zinazopatikana ndani ya nchi moja tu.

10.

Fuvu ya binadamu ya zamani kuliko zote ilipatikana Olduvai Gorge, Tanzania.

Kwisha habari!

Iman Lipumba
A digital storyteller, experienced in creating content that improves website visibility on search engines, enhances the user experience, and nurtures brand loyalty. With a background in the social sciences, an expert in researching complex ideas, and communicating them in engaging language to multiple audiences.