Uko Tayari Kuhama Nyumbani kwa Wazazi Wako?

  | 3 min read
0
Comments
1821

Je, wewe ni mtu mzima ambaye bado anaishi na wazazi wake?

Usijali. Kuishi nyumbani ni njia ya kuokoa pesa na kwa watanzania wengi, hatuna jinsi. Kwa kuwa imani za kiutamaduni na za kijamii hazipendekezi watoto waondoke nyumbani kabla ya ndoa (hasa wanawake), hali ya kiuchumi nayo ina mchango mkubwa kwa wengi wetu kubaki nyumbani.

Ukosefu wa ajira kwa vijana ni 13% and kukodi nyumba au apartment ni gharama kubwa – hasa kwa miji mikubwa kama Dar es Salaam.

Ila, ingawa kuishi nyumbani inafaida nyingi kama vyakula vya bure, hamna kodi na mengineyo, changamoto za kuishi na wazazi zinaongezeka kadri unavyokuwa. Hasa ukiwa na wale wazazi wanaokusubiri urudi nyumbani ukiwa umetoka usiku au wasio ruhusu wageni wa jinisia tofauti.

Kwa hiyo, muda itafika ambapo utaanza kuwaza kuhama nyumbani kwa kiundani. Kama umeshafikia hapa, jiulize maswali yafuatayo:

1. Unaweza kugharamia kuhama?

Huwa tukipiga mahesabu ya kuhama nyumbani, tunafikiria kodi tu. Lakini kuna mambo mengine ya kufikiria kama:

  • Karibia wenye nyumba wote watataka ulipe miezi 6 kabla ya kuhamia
  • Itabidi ununue fenicha kama sehemu unayohamia haina
  • Chakula na vifaa vya usafishaji vitakugharamia shs ngapi kila wiki?
  • Utahitaji mfanyakazi wa nyumbani?
  • Maji na umeme yanahesabiwa ndani ya kodi au itabidi uzilipie peke yao?
  • Utahitaji kuleta mlinzi/walinzi?

2. Itakuwa matumizi mazuri ya pesa yako?

Usingekuwa unahama, ungetumiaje pesa ya kodi?

Unawaza kuanzisha biashara? Umeweka akiba kufanya Uzamili? Kama kuna kitu kingine cha kuwekeza pesa yako ambayo itakuletea faida kubwa zaidi, labda huu sio muda wa kuhama nyumbani.

3. Faida kubwa za kuhama ni nini?

Unataka kuhama kwa kuwa sheria za wazazi wako zimekuchosha? Au unawafuata marafiki zako kwa kuwa wao wamehama nyumbani? Ni muhimu kutathmini sababu zako za kuhama.

Kwa hiyo, andika orodha ya faida kubwa za kuhama na gharama za kuhama.Hii itakupa picha nzuri ya maamuzi yakufanya.

Kwa mfano, kama faida ni kwamba:

  • Utaishi karibu zaidi na kazini na kupunguza muda wa kukaa kwenye foleni
  • Utakuwa na nafasi yako pekee
  • Unataka kujitegemea na kuwa na wajibu wa kulipa bill zako

Wakati gharama ni:

  • Matumizi yataongezeka kidogo, ila bajeti ipo

Basi bora uhame.

4. Rafiki zako wanaishi nyumbani?

Iwapo kujilinganisha na wengine ni ufunguo wa huzuni, ukiangalia jinsi wenzako unaowapenda wanaishi, itakusaidia kujua ni mabadiliko gani katika maisha yako unayobidi kufanya.

Kwa mfano, kama una miaka 34 na bado unaishi nyumbani, wakati rafiki zako wamesha hamia kwao au wameanza kujenga nyumba zao wenyewe, jiulize: Ninaishi nyumbani kwa sababu zinazoeleweka?

Labda kuisihi nyumbani inakupa muundo na mipaka unayohitaji ili kuendesha biashara yako, wakati rafiki zako wanapenda starehe na burudani sana. Ila, sababu inaweza ikawa kwamba kuweka akiba ya pesa ni ngumu kwako. Au hujamuliza bosi wako kuhusu kupandishwa cheo.

5. Ongea na watu wengine wazima

Ongea na wazazi wako. Iwapo wanaweza wakawa na upendeleo wao wa kuhama au kutokuhama, wanaweza wakakushauri vizuri na wakakusaidia kujiandaa kwa hilo.

Kwa mfano, wanaweza wakakuambia kwamba inabidi uanze kuweka akiba kwa ajilia ya wakati mgumu. Kwa hiyo, kila mwezi weka akiba ya 10% ya mshaara wako ili kama utapoteza ajira, unahitaji matibabu maalum au unapata majukumu ya kifedha usiyotegemea, utakuwa na akiba ya pesa kukusaidia.

Pia, kwa kujiandaa na maisha mapya yanayokusubiri, anza kuchangia gharama za umeme na kuwalipa kodi wazazi wako. Kwa kujizoesha kuwa na majukumu wakati bado uko nyumbani, utakuwa unajizoesha kwa maisha yako baada ya kuhama.

Uko tayari kuhama?

Kuhama kutoka nyumbani ina mahitaji zaidi ya kulipa kodi ya kununua nyumba. Inabidi ubadilishe fikra zako, ziwe fikra za mtu mzima anayejitegemea. Kwa hiyo, fanya maamuzi ya busara kwa kuwa ukishaahama, hakuna kurudi.

Usiwe na wasiwasi, tuko hapa kukusaidia. Ukiamua kuhama nyumbani unaweza kuanza tafuta sehemu ya kuishi kwa kupitia kipengele yetu ya nyumba na malazi.

Iman Lipumba
A digital storyteller, experienced in creating content that improves website visibility on search engines, enhances the user experience, and nurtures brand loyalty. With a background in the social sciences, an expert in researching complex ideas, and communicating them in engaging language to multiple audiences.