Tabia 7 za Kila Siku za Mabosi wenye mafanikio

  | 5 min read
0
Comments
3113

Hapa Tanzania biashara, kubwa na ndogo, zinafunga kila siku. Wakati huo huo, biashara zingine zinaendelea kwa miaka na miaka. Watafiti wamethibitisha kwamba 50% ya makampuni zinashindwa ndani ya miaka 5 ya kuanzia. Pia, 33% za biashara zinadumu kwa miaka 10 au zaidi.

Kunasababu nyingi sana zinazochangia kufanikiwa au kushindwa kwa kampuni/biashara. Sababu moja kuu ni mmiliki. Iwapo ni mwanzilishi, mkurugenza mtendaji au bosi mwenyewe, yule anayesimamia uendeshaji wa kampuni na hivyo, hutazamwa kama kiongozi na wafanyakazi ana mchango muhimu:

 • Yeye ndio mfano kuu kwa wafanyakazi kuhusu maadili ya kampuni na ya kazi
 • Wanawezesha wafanyakazi kuongelea bidhaa na huduma zinazotelewa na kampuni hiyo kwa wateja.
 • Anafanya wafanyakazi wajisikie vizuri kuhusu kufanya kazi hapo
 • Anawaajiri wafanyakazi bora wenye uwezo wa kusimamia idara zao.

Hizi ni sababu chache zinazonyesha umuhimu wa bosi kwenye mafanikio ya kampuni.

Sasa, swali linakuja: Ni jinsi gani wewe unaweza ukawa bosi/mwajiri/kiongozi mzuri kwenye kampuni yako? Tunatumaini kwamba hizi tabia 7 za mabosi wenye mafanikio yatakusaidia:

1. Wanaamka mapema

Hapa Tanzania, kuna mtazamo wa kwamba bosi anaweza kuingia na kuondoka kazini muda wowote ule. Labda hii ni ukweli kwenye makampuni mengi, ila, kama kampuni inatakufanikiwa, na kama ndio kwanza imeanza, bosi inabidi awe mchapa kazi nambari moja.

Kwa ujumla, watu wengi wenye mafanikio wanaamka mapema kwa vile:

 • Inawapa muda wa kufanya kazi zadi
 • Asubuhi ni muda mzuri wa kufanya mazoezi. Hii inakuwezesha uwe na nguvu zaidi katika siku yako.
 • Wanaweza kutumia asubuhi kufanya vitu vingine wanvyopenda, ambazo ziko nje ya kazi.
 • Wanapata muda wa kula vizuri na kiafya zaidi asubuhi
 • Kujiongezea nidhamu. Kuamka mapema, kama kuongoza kampuni, inahitaji nidhamu ya hali ya juu.

Hutuamini?

Basi, Business Insider inatuonyesha watu 10 maarufu wenye mafanikio na muda wao wakuamka:

 1. Mkurugenzi mtendaji wa Apple Tim Cook anaamka saa kumi kasorobo asubuhi, kila siku.
 2. Michelle Obama anaamka saa kumi na nusua asubuhi kila siku.
 3. Mkurugenzi mtendaji wa Twitter Jack Dorsey anaamka saa kumi na mjoa asubuhi, kila siku.
 4. Richard Branson, mwanzilishi wa Virgin anaamka saa kumi na mbili kasorobo asubuhi, kila siku.
 5. Mkurugenzi mtendaji wa PepsiCo Indra Nooyi anafika ofisini saa moja asubuhi, na hapo ni akiwa amechelewa.
 6. Mkurugenzi mtendaji wa General Motors Mary Barra anafika ofisini saa kumi na mbili asubuhi.
 7. Mkurugenzi mtendaji wa Starbucks Howard Schultz anaamka saa kumi na nusu asubuhi.
 8. Michelle Gass, rais wa Starbucks anaamka saa kumi na nusu asubuhi.
 9. Rais wa zamani wa Marekani George HW Bush anaamka 4am.
 10. Mhariri mkuu wa Vogue, Anna Wintour anaamka saa kumi na mbili kasorobo asubuhi.

2. Wanaweka malengo yao kwenye kufanya kazi ya maana kuliko kuwa ‘busy’

Kunatofauti kati ya kuonekana kama una kazi nyingi na kufanya kazi ya maana. Tofauti kati ya hizi mbili ni vipaumbele.

Bosi anayeelewa mahitaji ya kukuza kampuni atafanya kazi za maana. Bosi asiyeelewa haya atajaribu kufanya kai nyingi bila mwelekeo.

Kazi zenye malengo kamili yanawapa wafanyakazi matokeo ya maana, wakati ukiwa una tembeatembea kwenda hapa na pale haitakuwezesha kumaliza kazi muhimu. Watu wenye mafanikio wanaelewa uwekaji wa vipaumbele na hii inawasaidia kufanikiwa zaidi.

Kwa mfano, mtu mwenye kazi nyingi atakubali kupewa kazi wakati hana muda huo. Ila mfanyakazi anyezingatia kufanya kazi ya maana anathamini muda wake. Kwa hiyo, kabla ya kukubali kazi atafikiria kama kweli ana muda wa kufanya kazi hiyo.

Kwa kifupi, hawaogopi kusema, ‘hapana, sina muda wa kufanya kazi hiyo’.

3. Wanakundi nzuri ya wafanyakazi wanaowaamini

Wanaajiri watu bora. Ndio bosi ni muhimu, ila wafanyakazi wote ndio wanaijenga kampuni.

Utafiti uliofanyiwa na Chuo Kikuu cha Kentucky iligunduwa kwamba wafanyakazi wakiwa ndani ya kundi maalum, badala ya kufanyakazi wenyewe, huwa wanafanikiwa kumaliza kazi kwa haraka na kwa usahihi zaidi. Pia wanaridhishwa zaidi na kazi walizopewa ndani ya hiyo kundi.

4. Wanasikiliza wafanyakazi wao

Mwanzilishi na mbunifu wa Apple, Steve Jobs, aliwahi kusema kwamba ‘Kumwajiri mtu mwenye akili na kumwambia cha kufanya haina maana. Tunaajiri watu wenye akili ili watuambie chakufanya”

Kinachotofautisha bosi wa kawaida na bosi bora ni kwam bosi bora haongei tu, anasikilizi maoni na maswali ya wafanyakazi wake. Mwajiri mzuru anaelewa kwamba maoni ya wafanyakazi wake yana umuhimu kubwa na kuyasikiliza inaweka nafasi nzuri katika kampuni ya wafanyakazi kutoa maoni yao.

Richard branson alisema, ‘kuna tofauti kati ya kumsikia mtu na kumsikiliza’. Ukimsikiliza mtu inamaanisha kwamba unajaribu kumuelewa badala ya kumsikiliza tu na kumpotezea baada ya hapo. Branson anaendelea kusema kwamba mtu anayesikiliza anajifungulia kupata ubunifu zaidi kwa kutumia masikio yake badala yam domo waka kila mara!

5. Wanatunza miili na akili zao

Kwa kupanga muda wa kufanya mazoezi, unapewa nafasi ya kujenga tabia ya kuweka na kufuata ratiba.

Pia, mazoezi yanawasaidia mabosi kwa kuwa:

 • Yanaongeza furaha; ukifanya mazoezi mwili wako hutoa kemikali, kwa mfano (endorphins, zinazosabibisha furaha)
 • Zinamsaidia mtu kujiamni zaidi.
 • Mazoezi ni njia nzuri ya kujihusisha na kitu zaidi ya kazi kinachochangia afya yako na kuhakikisha kwamba hujichoshi kazini.
 • Mazoezi yanakuongeza nguvu, nguvu itakayotumika kukumbana na matatizo mbali mbali ya ofisini.

6. Kuwa na marafiki wenye sifa nzuri

Marafiki wa mabosi walifanikiwa wamefanikiwa pia. Wakiwa pamoja, wanajadiliana kuhusu biashara na sekta yao. Watu wako wa karibu wakiwa na malengo yao yakufanikiwa watukufanya na wewe uchape kazi zaidi ili wote mfanikiwe.

Ukiona mafanikio ya wenzako inabidi ujisikie kwamba, ‘na mi naweza’.

7. Hawaachi kujifunza

Kwa kuwa wewe ni bosi haimaanishi kwamba unajua kila kitu. Watu wote wenye akili zaidi wanaendelea kujifunza. Bosi bora anajifunza kutoka kwa:

 • Washauri. Watu wenye uzoefu zaidi yao
 • Wafanyakazi wao. Wanaufahamu ambayo huwezi ukawa nao.
 • Vitabu. Wanasoma vitabu kuhusu sekta yao pamoja na vitabu kuhusu kuishi vizuru maishani, vitabu vya tawasifu n.k
 • Kupitia intaneti. Kuna rasilimali nyingi sana za bure kama Coursera, Open University na Udemy
 • Uzoefu. Wanajifunza wakishindwa pamoja na wakifanikiwa.

Ubora unafanyiwa mazoezi na haikamiliki

Hii sio dokezi, bali ni kitu cha kukumbuka maishani. Kwenye zoezi ya kuwa bosi bora, inabidi uzifanyie mazoezi vidokezo 7 zilizoelezwa hapo juu mpaka pale zitakapo kuwa tabia yako ya kila siku.

Ila, hautakamilika. Bosi bora anajaribu kujiboresha kila mara. Ni muhimu kutoruhusu mafanikio yako yakufanye uwe na kiburi kwa kuwa watu wenye kiburi wanafikiri wanajua kila kitu. Badala yake, kumbuka kwamba unaweza ukajiboresha zaidi. Waajiri wenye mafanikio wanajua hili na ndio maana makampuni yao yanadumu kwa vizazi.

 

Iman Lipumba
A digital storyteller, experienced in creating content that improves website visibility on search engines, enhances the user experience, and nurtures brand loyalty. With a background in the social sciences, an expert in researching complex ideas, and communicating them in engaging language to multiple audiences.