Sifa 5 za Kisiri Zinazotafutwa na Waajiri

  | 3 min read
0
Comments
1763

Unahitaji kufanya nini kupata ajira?

Ndio, kila mwajiri anamtafuta mfanyakazi mwenye ujuzi maalum ila kufanya kazi maalum, ila wengi wanaoitwa kwenye interview wana sifa zinazohitajika. Kwa hiyo, mwajiri anajuaje amchague yupi?

Watafuta ajira huwa hawatambui kwamba zaidi ya kuwa na sifa za kufanya kazi hiyo, kuna sifa zingine zinazotafutwa na mwajiri.

Sifa hizi ndio zinaweza kuwa sababu ya mtu mmoja achaguliwe juu ya mwingine.

Kwa hiyo, ukiwa unaomba kazi kuna sifa 5 unazobidi kuonyesha kwenye CV, barua ya kuomba kazi pamoja na lugha utakayo tumia kwenye interview, ili ujiongezee nafasi ya kupata kazi hiyo.

  1. Uwezo wa kuwasiliani kwa Kiingereza (kuandika, kuongea na kusikiliza)

Tatizo kubwa kwa ukuaji wa biashara Tanzani ni kwamba watu wengi walioajiriwa wanshindwa kuwasiliana vizuri kwa Kiingereza.

Inasikitisha kwa watafuta ajira wenye utaalamu hawapati nafasi ya kushindania nafasi za kazi nyingi kwa kuwa hawawezi kuandika na kusoma Kiingereza kwa kiwango kinachohitajika.

Ila, unataka kuboresha uwezo wako wakuwasiliana kwa Kiingereza?

Tafuta kozi kwa kupitia ZoomTanzania.

  1. Uwezo wakukabiliana na vitu vingi

Waajiri wanapenda watu wenye uwezi wa kukabiliana na kazi nyingi kwa wakati mmoja.Kuwezi kufanya hivi ni kuweza kuweka vipaumbele na kukabiliana na mabadiliko ya kikazi na kwenye sekta hiyo. Kama unataka kufanya kazi kwenye sekta za Masoko, Matangazi, Vyombo vya Habari, Tehama au Digitali, inabidi uwe na uwezo wa kufanya hivi.

Kwa mfano, kama unataka kufanya kazi kwenye kampuni inayohusika kwenye masoko kupitia intaneti, utaweza kushughulikia mahitaji ya wateja wako pamoja na kuendelea na kazi zako za kila siku?

  1. Kuwa na fikra za kiundani

Usipokee habari kwa juujuu. Fikiria umeipokea kutoka wapi, kwanini umeambiwa na jinsi gani inaweza kukusaidia.

Watu wenye fikra za kiundani na sio za juujuu tu wanaweza kutoa suluhisho kwa matatizo mbali mbali kwa kutumia ubunifu, ujuzi pamoja rasilimali mengine.

  1. Kujituma

Kuna tatizo nyingine inayokumba waajiri wa Tanzania, kwamba wafanyakazi hawajitumi. Wengi wetu tumefundishwa kufanya kile tunachoambiwa. Ni mara chache sana kwamba tunajituma kufanya zaidi ya tulichoambiwa.

Waajiri huwa wanatafuta wafanyakazi wanaopenda kazi yao na wana fikra na mbinu zao za kusaidia biashara ikue. Hawataki wafanyakazi wanaofanya kazi ili walipwe mwisho wa mwezi, tu.

  1. Kuonyesha nia ya Kujifunza

Siku hizi, wafanyakazi wengi wanajikuta wakiombwa kufanya kazi ambazo kwa kawaida zilikuwa hazihusiani na nafasi zao.

Ila, kutokana na mabadiliko ya kiteknolojia, kazi zinabadilika na watafuta ajira inabidi waonyesha nia ya kukua na kujifunza, pamoja na kubadilika. Usipoweza kufanya hivyo, mwingine ataajiriwa.

Kumbuka, kabla ya kuomba kazi, kama unajua kwamba kuna sifa maalum ambazo ni muhimu mtu awe nazo kwenye sekta ya hiyo kazi unayoomba, jiwekee muda wa kujifunza. Hii itakuongezea nafasi ya kuajiriwa.

Wekeza kwenye maisha yako ya baadaye. Fanya mtihani kujua nguvu na mapungufu yako

Mara kwa mara, watafuta ajirawanakuwa wamelenga kuthibitisha kwamba wanaweza kazi fulani, mpaka wanasahau sifa zitakazo wavutia waajra kwao kuliko watafuta ajira wengine.

Mtu yoyote mwenye mafanikio anaelewa kwamba kuna uwezo wa kujiboresha. Kwa hiyo, badala ya kuupotezea nafasi nzuri, fanya utafiti na jipe muda wakujifunza kitu kipya kitakacho kufaidi katika utafutaji kazi

Uzuri ni kwamba ujuzi wote ulioelezwa hapa inaweza kufundishwa.

Sehemu moja ya kuanzia ni kujua nguvu na mapungufu yako. Kuzijua, fanya mtihani wa AMCAT. Itakusaidia kujua:

  • Kiwango chako cha Kiingereza na mawasiliano kwa ujumla
  • Kiwango chako cha kufikri
  • Ujuzi wa kazi unayoomba
  • Kama tabia yako inaendana na kazi unayoomba.

Fanya mtihani wa AMCAT

 

Iman Lipumba
A digital storyteller, experienced in creating content that improves website visibility on search engines, enhances the user experience, and nurtures brand loyalty. With a background in the social sciences, an expert in researching complex ideas, and communicating them in engaging language to multiple audiences.