Sehemu Kumi za Kimapenzi za kutembelea kwa ajili ya Fungate Tanzania

  | 5 min read
0
Comments
6134

Ni nini kinachofanya sehemu iwe nzuri kwa ajili ya Fungate?

Kwa kweli inategemea utu na nia ya wachumba. Wengine wanpenda sehemu iliyotulia na kuna wengine wanapenda kukaa mjini na kujifunza historia ya mji.

Kwa bahati nzuri, karibia chochote unachokitaka utakipata Tanzania. Kwa kuwa kuna ufukwe vya kutosha, mbuga za wanyama, hoteli za nyota 5 na watu wazuri, ni nchi nzuri ya kuanza maisha mapya na mpenzi wako.

Kukuanzisha, pitia orodha yetu ya sehemu kumi za kimapenzi za kutembelea kwa ajili ya fungate Tanzania. Zitafanya wewe na mpenzi wako muendeleze hisia zenu za kimapenzi zaidi na zaidi.

1. Lazy Lagoon Island Lodge, Bagamoyo

Lazy Lagoon iko kusini mwa Bagamoyo na ni sehemu nzuri sana kwa wachumba wanaopenda kuwa kwenye fukwe binafsi pamoja na huduma ya kipekee.

Tovuti ya Lazy Lagoon inaeleza kwamba ina banda 12 zenye vitanda vyakulala watu wawili au moja. Banda zote zina choo na bafu, na zinatazama bahari.

Bagamoyo inaumbali wa lisaa limoja kutoka Dar es Salaam na inachukua dakika 15 kufika Lazy Lagoon kutoka Bagamoyo mjini.

Soma maoni ya watu kupitia Tripadvisor

2. Nungwi, Zanzibar

Kama unataka fungate ufukweni na yenye huduma ya hali ya juu kabisa, basi Nungwi iliyopo kaskazini mashariki ya Zanzibar, ndio pakwenda.

Kuna malazi mengi mazuri Nungwi na Hideaway of Nungwi Resort & Spa ni mojawapo. Ina vyumba ambazo zinamfaa mfalme (zipitie hapa), spa, huduma za kuchua na za urembo, gym na mengineyo. Hii ni sehemu ya kwenda kama unataka kupumzika kama wafalme.

Kujua zaidi pitia tovuti yao.

Pia, soma maoni kupitia Tripadvisor

3. Mullers Mountain Lodge, Usambara

Kama hamtaki kwenda kwenye fungate ufukweni ila bado mnataka kufurahia mazingira ya kimapenzi, basi malazi yaliopo ndani ya milima ya Usambara yatakuwa suluhisho.

Mullers Mountain Lodge ina banda zilizojengwa kwa mitindo ya zamani lakini zenye vifaa vya kisasa. Pia, unaweza kutembea kwenye milima hizo na zipo karibu na mporomoko wa maji. Zinaleta mazingira za kinyumbani zaidi na zimekuwepo kwa zaidi ya miaka 10. Wanajua namna ya kukusaida kupumzika na vilevile kuhakikisha unaondoka na kumbukumbu safi.

Kujua zaidi, pitia tovuti yao.

Pia, soma maoni ya wageni waliowahi kwenda kupitia Tripadvisor

4. Uroa, Zanzibar

Hotelihii ya gharama nafuu ina huduma za kuvutia ambazo sio gali sana. Huduma maalum zinazotolewa ni pamoja na:

 • Mlo wa jioni ya kibinafsi karibu na bwawa la kuogelea likitazama Bahari wa Hinfi
 • Matembezi ya bahari kwa kutumia boti. Utakuwa na wavuvi watakao kupeleka kwenye ziada ya aina yake baharini mpaka kwenye miamba ya matumbawe
 • Michezo ya majo kama scuba diving, snorkeling na kite surfing.

Kujua zaidi, pitia tovuti ya Uroa

Soma maoni ya wengeni waliowahi kwenda kupitia tripadvisor

5. Bushtops Camp, Serengeti

Hakuna mtu aliyesema kwamba mapenzi hayawezi kuchangamshwa. Tembelea mbuga ya wanyama bora duniani na mpenzi wako.

Kati ya kambi zote zilizopo Serengeti, Bushtop Camps ndio bora kwa wachumba. Chakula chao ni cha kufurahia sana, ina vifaa vya kisasa na wanyama bora. Inasemekana kuwa ni eneo bora ya mbuga za wanyama duniani.

Tovuti yao ina ukurasa maalumu kwa wachumba.

Soma maoni ya wageni waliowahi kulala hapo kupitia Tripadvisor

6. The Palms, Bwejuu

Gazeti maarufu ya Travel + Leisure iliichaguwa The Palms kama moja kati ya hoteli za mapumziko bora duniani. Kama unataka kuishi kifahari na pesa sio tatitizo, hapa patakufaa.

The Palms ina villa 6 tu za kipekee zeilizopambwa na rangi na fenicha za kisasa za kizanzibari. Pia, zina:

 • Bwawa la kuogelea
 • Dstv na DVD player
 • Bar ndogo
 • Bar inayotoa huduma za chain a kahawa
 • Sehemu ya kuhifadhi vitu muhimu
 • Simu
 • AC

Zaidi ya hapo, kuna migahawa, bar, spa, michezo ya maji na vinginevyo vya kufurahia. We na mchumba wako hamtaboreka kabisa.

Kujua zaidi, pitia tovuti ya The Palms

Soma maoni ya wageni waliowahi kulala hapo kupitia Tripadvisor

7. Mount Meru Game Lodge na Sanctuary, Arusha

Hoteli iliyopo kati ya mto na eneo ya wanyamapori, imetulia. Mandhari yake ni kitulivu na unaweza ukakutana na pundamlia, mbuni, nyani na mengineyo. Ni sehemu nzuri sana kwa wachumba wanaotaka kupata uzoefu wa kuona wanyama pamoja na utamaduni.

Kuna vyumba 15, 2 zikiwa Suite za kifahari amabazo zina sebule, chumba cha kulala pamoja na sehemu ya kuota moto. Suite hizi pia zina bustani na baraza zao.

Mambo mengine yakufanya ni:

 • Kwenda kwenye ziada ya kahawa
 • Kwenda kwenye matembezi ya utamaduni na elimu
 • Kucheza Golf
 • Kwenda kununua shanga.

Soma maoni ya wageni waliowahi kulala hapo kupitia Tripadvisor

8. Malaika Beach Resort, Mwanza

Ukifikiria mtazamo wa kuvutia wa maji kwenye sehemu ya kwenda kwenye Fungate, wengi wetu tutafikiria Zanzibar. Ila Mwanza, ambapo Ziwa Victoria ilipo, pia ina mengi ya kuvutia. Pia, ni masaa mawili kutoka upande wa Magharibi ya Serengeti na pia kuna Rubondo Island National Park. Kwa hiyo, unaweza kufurahia mitazamo mizuri ya Ziwa Victoria pamoja na kuangalia wanyama.

Kujua zaidi, pitia tovuti ya Malaika Beach Resort, Mwanza.

Soma maoni ya waliowahi kulala hapo kupitia Tripadvisor

9. Pole Pole Bungalows, Visiwa vya Mafia

Kama unataka kwenda sehemu ya kuwa na mchumba wako kwa muda maalum bila kusumbuliwa, Visiwa vya Mafia zina mchanganyiko mzuri wa utulivu na uzuri wa ajabu zitakazo kusaidia kufurahia muda wako na mpenzi wako.

Pole Pole Bungalows zinatumia asili ya Visiwa vya Mafia kutengeneza mazingira ambayo hutakuja kusahau.

Kujua zaidia, pitia tovuti ya Pole Pole Bungalows.

Soma maoni ya waliowahi kulala hapo kupitia Tripadvisor

10. Protea Hotel Courtyard, Dar es Salaam

Kama unataka fungate ya mjini zaidi iliyojaa na mitoko mbalimbali, basi Dar es Salaam ndio pakwenda. Kuna mamia ya migahawa vyenye vyakula vya nyumbani/kiasili, pamoja na vya nje vikiwemo vya Ethopia, Italia na China. Pia, kuna baa nyingi zenye bendi, utalii wa kitamaduni, hoteli zilizopo ufukweni pamoja na visiwa vya kutembelea. Kwa kifupi, huweza ukaboreka.

Protea Hotel Courtyard ni hotel safi ya kupumzika baada ya kuzunguka Dar.

Soma maoni ya waliowahi kulala hapo kupitia Tripadvisor.

Chaguo mingi. Mapenzi mingi.

Tanzania nia moja kati ya nchi chache duniani ambazo unaweza kupata sehemu ya kwenda kwa ajili ya fungate itakayofaa mtu yoyote. Iwapo unatako mitoko mbalimbali, kumpumzika peke yenu au kupumzika kifahari, fungate yako itakuridhisha haswa.

Kupitia sehemu zingine za kwenda, pitia kipengele cha Hoteli na Malazi zilizopo nchini, kwenye Orodha ya Biashara yetu.

Iman Lipumba
A digital storyteller, experienced in creating content that improves website visibility on search engines, enhances the user experience, and nurtures brand loyalty. With a background in the social sciences, an expert in researching complex ideas, and communicating them in engaging language to multiple audiences.