Nyumba 6 Zenye Bustani Zinazofaa Kupanga

  | 4 min read
0
Comments
10538

Unapotaka kupanga nyumba kuna vitu kadhaa inabidi uangalie kwanza. Vitu kama kodi, uwepo wa maji, usalama, idadi ya vyumba na hata majirani zako. Lakini watu wengi husahau bustani. Nyumba zenye bustani zinakuwa nzuri na zenye mvuto, lakini hii sio sababu pekee ya kukufanya upange nyumba yenye bustani. Kuna faida kubwa za kuwa na nyumba yenye bustani. Bustani ni nzuri kwa afya yako, mchakato wa kutunza bustani ni mazoezi mazuri kwa mwili wako. Tafiti zinaonyesha kuwa bustani inasaidia kuleta utulivu na furaha kwa nafsi. Bustani ni eneo zuri kwa kufanya shughuli au sherehe ndogo kwa familia na marafiki. Pata faida hizi kwa kupanga nyumba kati ya hizi zilizopo Dar es salaam.

Mikocheni         

 Nyumba Zenye Bustani                                

Unaweza kupanga nyumba nzuri ya chumba kimoja ambayo ina bustani, ipo eneo la Mikocheni. Kodi inaanzia dola 350 za kimarekani, lakini unaweza kupunguziwa kulingana na makubaliano ili kufikia bajeti yako. Nyumba hii inakuja na fanicha na huduma muhimu kama kiyoyozi, ulinzi na sehemu ya kupaki gari.

Kinondoni         

  Nyumba Zenye Bustani                              

Kama una familia, Kinondoni kuna nyumba kubwa nyingi zenye bustani. Nyumba hii ya kifahari ina bustani na vyumba vitatu, kimoja ambacho kinafaa kwa wazazi kina choo na bafu lake. Nyumba imezungukwa na bustani nzuri zinazotunzwa na zenye maua ya kuvutia. Nyumba hii pia inakuja na fanicha na huduma zote za muhimu kama maji, ulinzi saa 24, sehemu ya kupaki gari na sehemu ya kufanyia mazoezi. Kodi inaanzia dola 500 za kimarekani.

Oysterbay     

 Nyumba Zenye Bustani                                     

Oysterbay ni moja ya mitaa ya kifahari zaidi Dar es salaam. Nyumba ya vyumba 4 hufikia hadi kodi ya dola 3000 za kimarekani na inakua na huduma za kutosha kukufanya uishi raha mustarehe.Hii inakuja na mabafu 3 na bwawa la kuogelea la ndani kwa ajili ya familia. Ina uwanja wa kutosha bustani kubwa ambayo unaweza kutembea kila asubuhi kwa ajili ya kujiburudisha. Pia unapata nyumba ndogo ya watumishi na jenereta.

Masaki   

 Nyumba Zenye Bustani                                    

Masaki ni eneo lingine la kifahari lenye nyumba kadhaa zenye bustani. Nyumba hii ya vyumba 4 ya dola 4000 za kimarekani inakuja na uwanja mkubwa wenye eneo la kutosha. Ina bustani na sehemu ya kucheza watoto na kufanya starehe za familia. Nyumba inaweza kuwa na fanicha au la kulingana na unachotaka. Huduma zilizopo ni bwawa la kuogelea, sehemu ya kupaki magari yenye kivuli na nyumba ndogo kwa ajili ya watumishi.

Nyumba ya kifahari zaidi inakuwa na kodi ya dola 4200 za kimarekani. Hii ina  bwawa la kuogelea na bustani ya kisasa zaidi. Pia ina fanicha, vyumba vikubwa na huduma zote za muhimu kama kiyoyozi, nyumba ndogo kwa ajili ya watumishi na sehemu ya kupaki magari yenye kivuli. Hii inafaa kwa familia kubwa.

Goba

 Nyumba Zenye Bustani

                                       

Katika eneo la Goba, kodi ya nyumba kubwa za kifahari inaanzia dola 532 za kimarekani. Nyumba za gharama hii zinaweza kushangaza matarajio yako. Hii ina eneo kubwa na bwawa kubwa la kuogelea lenye sehemu ya wakubwa na ya watoto. Pia ina vyumba 4 vyenye choo na bafu ndani na vyumba 2 vya wageni. Bwawa la kuogelea limezungukwa na bustani yenye mandhari nzuri. Njia za ndani zimesakafiwa na nyumba ya watumishi ni ya kisasa.

Kigamboni

  Nyumba Zenye Bustani                             

Eneo la Kigamboni lina nyumba za vyumba 4 za kutosha zinazoanzia dola 800 za kimarekani. Nyumba hii ina fanicha na mapambo yake ya ndani ni yenye kuvutia. Pia inakuja na vifaa vya jikoni na mashine ya kufulia nguo. Nyumba nzima ina kiyoyozi na nje ina bustani ya kuvutia. Huduma nyingine zilizopo ni tanki la maji, sehemu ya kufanyia mazoezi na sehemu ya kupaki magari.

Chagua Nyumba (Nyingi Zaidi) Hapa

Kama ungependa kuona nyumba nyingi zaidi zinazopangishwa na zinazouzwa, pakua app ya ZoomTanzania na tembelea ukurasa wa nyumba au tembelea ukurasa huo kwenye tovuti yetu.

Neema Ngelime
A Content Creator who paints with light.