Nukuu 10 Zitakazo Kufanya Utake Kusafiri Zaidi

  | 2 min read
0
Comments
13978

Kusafiri ni moja kati vitu bora vya kufanya maishani. Iwapo kusafiri inatupa furaha pamoja na kutusaidia kuwa wafanyakazi bora zaidi, tunajiongezea busara kwa kuwa tunapata fahamu mpya za sehemu mbalimbali duniani.

Aidha, ukisafiri kwenda sehemu ambayo ni tofauti kabisa na ulichozoea, inakufanya uheshimu zaidi mila, destuli na utamaduni tofauti. Pia, inaweza ikaongeza ubunifu wako na kupanua  fikra zako.

Kama bado hatujakushawishi kusafiri, basi nukuu 10 zifuatayo zitakufanya utake kusafiri zaidi:

  1. “Hatusafiri kutoroka maisha, tunasafiri ili maisha yasitutoroke” – Bila Jana
  2. “Mimi sio mtu yule yule, baada ya kuona mwezi ukiandama kwenye upade mwingine wa dunia” – Mary Anne Radmache
  3. “Travelling – inakufanya ukose maneno alafu inakupa hadithi za kuwaambia watu” – Ibn Battuta
  4. “Matumizi ya kusafairi ni kupatanisha ubunifu na ukweli, na badala ya kufikiria jinsi gani vitu vitakavyo kuwa, tutaon jinsi zilivyo” – Samuel Johnson
  5. “Kusafiri ni kugundua kwamba kila mtu amekosea kwenye fikra zake za nchi zingine” – Aldous Huxley
  6. “Labda kusafiri haiwezi kuzuia ubaguzi, ila kwa kuonyesha kwamba watu wote wanalia, wanacheka, wanakula wanapata wasiwasi na wanakufa, inaweza ikaanzisha wazo wa kwamba tukijaribu kuelewana, hata marafiki tunaweza kuwa.” – Maya Angelou
  7. “Sio wote wanaotembea tembea wamepotea – J.R.R Tolkien
  8. “Usiniambie ulivyojielimisha, niambie ulivyosafiri’ – Mohammed
  9. “Dunia ni kitabu na yule asiyesafiri anasoma ukurasa mmoja tu” – St. Augustine
  10. “Kusogea, kupumua, kupaa, kuelea; kupata wakati una gawa; kutembelea barabara za vijijini; kusafiri ni kuishi” – Hans Christian Andersen

Haya! Nukuu 10 safi kabisa zinazoelezea uzuri wa kusafiri!. Kila mtu ana sehemu anayotaka kutembelea. Na kama hukujua unapotaka kwenda, labda unajua sasa hivi.

Kusafiri ni fundisho ambayo huwezi kupata darasani au kwenye intaneti. Kuna vingi vya kuona, anza!

Tafuta wakala wa usafiri alafu anza kupanga safari yako leo!

Iman Lipumba
A digital storyteller, experienced in creating content that improves website visibility on search engines, enhances the user experience, and nurtures brand loyalty. With a background in the social sciences, an expert in researching complex ideas, and communicating them in engaging language to multiple audiences.