Nguo za Uzazi – Jinsi ya kuvaa ukiwa mjauzito

  | 2 min read
0
Comments
23846

Utamaduni wa Tanzania inapendekeza wanawake kuvaa nguo kubwa, zilizopwaya wakati wa ujauzito. Kama vile hawana haja ya kupendeza wakiwa wajawazito. Bahati nzuri, kuna maduka mengi zenye mavazi mazuri za wakati wa ujauzito.

Ila bado kuna wanawake wengi wanaoamua kutojali muonekano wao wakiwa wajawazito. Sasa, kwa wao, vidokezo vifuatayo vitakusaidia kuvaa ukiwa mjauzito.

1. Kubali umbo lako

Hamna haja ya kuficha ujauzito wako. Ila hatusema kwamba uvae blauzi inayobana na kimini (ila, unaweza kuvaa hivyo ukipenda). Tunachopendekeza hapa ni kuvaa nguo zinazotosha umbo lako.Tumbo lako likianza kujitokeza, nunua nguo kama gauni, jinzi na topu zinazo ruhusu hewa kupita; hizi zitakuwezesha kuonyesha figure yako kwa kistaarabu.

2. Usibadilishe mtindo wako wa kawaida

Kwa kuwa we ni mjazmzito haimaanisha kwamba inabidi ubadilishe mtindo wako wa kipekee.

Kwa hiyo, kama ulikuwa unapenda gauni, endelea kuvaa gauni. Hakikisha inatosha umbo lako tu.

3. Tumia vifaa vya mitindo

Scafu, bangili, ereni n.k zitasaidia kuboresha vazi lako kwa ujumla na zitakusaidia kujiamini pia. Kwa mfano, kama unawasiwasi na tumbo lako lilivyojitokeza, vaa mkufu au ereni safi zitakazo fanya watu waangalie sura badala ya tumbo yako.

4. Nunua Jinzi safi kwa ajili ya ujauzito

Nunua jinzi zenye uwezo wa kupanuka ndio zitakazokufaa. Zinaweza zikawa za kubana au zenye nafasi zaidi, cha muhimu nikwambai unajisikia vizuri ukizivaa.

5. Nunua gauni ya kufunga (Wrap Dress)

Wrap Dress zinafaa kwa umbo yoyote ile na zinapendeza sana! Pia ni rahisi kuzivaa na kutembea ndani yao ukiwa umezivaa.

6. Nunua nguo zenye rangi kali

Rangi kali kama njano na rangi ya machungwa (orange) zinaonyesha ile mwanga asili ambao wajawazito huwa wanao. Kwa hiyo, kuvaa gauni yenye rangi kali inaweza ikampa mjamzito mng’ao wa kirembo.

Onekana vizuri zaidi ya unavyojisikia

Kuwa mjamzito ni wakati muhimu katika maisha ya mwanamke na kwa kuwa hutajisikia vizuri kila siku ya ujazito wako, unaweza kuendelea kupendeza na kutafuta nguo zitakazoipendza mwili wako.

Tafuta nguo nzuri za ujauzito hapa

Iman Lipumba
A digital storyteller, experienced in creating content that improves website visibility on search engines, enhances the user experience, and nurtures brand loyalty. With a background in the social sciences, an expert in researching complex ideas, and communicating them in engaging language to multiple audiences.