Nguo na vifaa vingine vya watoto changa

  | 2 min read
0
Comments
19610

Kwa bahati nzuri hapa Tanzania, wanawake wengi wakiwa wajwazito wanapata msaada kutoka kwa mama zao na wanawake wengine ndani ya familia, pamoja na rafiki zao wa kike. Ila, kujiandaa na kuwa mzazi ni ngumu sana, hasa ikiwa ni mtoto wako wa kwanza.

Ni rahisi sana kununua vitu vingi ambavyo mtoto wako hatahitaji au kufurahia. Ila, ni rahisi sana kusahau vitu muhimu kwake.

Kukusaidia, tumeandaa orodha ya nguo za mtoto changa na vitu vingine utakavyohitaji mtoto akija:

1. Nguo za kila siku

Achana na bukta na gauni, hakikisha unajipatia:

 • Nguo 6 zenye mikono na miguu zikiwa zimeshonwa kwa pamoja. Ziwe za mikono mirefu
 • Fulana 6
 • Pea 4 ya soksi
 • Kofia 2

2. Neppi

Mtoto mchanga atahitaji kubadilisha neppi yake kwa mara 8 au 12 kwa siku. Zaidi ya neppi, utahitaji:

 • Mifuko ya kutupia neppi zilizotumika
 • Tissue za kumpangusa mtoto ukiwa unabadilisha neppi
 • Dawa za neppi – kuua wadudu

3. Vifaa vya kumlisha

Iwapo unaamua kunyonyesha, kutumia chupa au zote mbili, utahitaji:

 • Sidiria za kunyonyesha
 • Pedi za matiti kuzuia mwagiko wa maziwa
 • Pampu ya matiti
 • Chupa za kulisha
 • Burashi za kusafishia chupa
 • Dawa za kuua wadudu kwenye chupa

Pitia vifaa hivi hapa.

4. Vifaa vya kumuogesha:

Utahitaji:

 • Bafu la mtoto mchanga
 • Sponji laini yakumwogesha
 • Taulo za watoto
 • Pamba kusafisha masikio na shingo

5. Vifaa vya kulala

Zaidi ya kula na kunya, watoto wanatumia muda wao mwingi kulala. Hakikisha mtoto wako analala kwa faraja kwa kuwa na:

 • Kitanda cha mtoto yenye godoro na mashuka yake
 • Kikapu cha Moses yenye godoro na mashuka ya kumlazi mtoto akiwa hayupo kitandani.
 • Mito
 • Mtandio wa pamba

6. Vifaa vya kusafiri

Utahitaji:

Pata strolla na pram bora za watoto wachanga hapa

Mwisho wa siku, utafurahia

Kuwa mzazi ni kazi ngumu kuliko zote, ila mwisho wa siku ni kazi inayoleta furaha kuliko yote. Kwa hiyo, furahia maandalizi ya kuwa mzazi na kuwa mzazi kwa ujumla!

Tafuta bidhaa zote utakazohitaji za watoto changa hapa.

Iman Lipumba
A digital storyteller, experienced in creating content that improves website visibility on search engines, enhances the user experience, and nurtures brand loyalty. With a background in the social sciences, an expert in researching complex ideas, and communicating them in engaging language to multiple audiences.