Mwongozo Kuu wa Kuajiri Wafanyakazi Bora

  | 5 min read
0
Comments
3143

Changamoto moja kubwa kinachopunguza kasi ya ukuwaji wa kibiashara ni ukosefu wa rasilimali watu wenye utaalam na motisha. Kwa kifupi, makampuni yanapata shida kutafuta wafanyakazi wazuri.

Ingawa mfumo wa elimu Tanzania ina wafundisha wanafunzi vitu vingi, haikuzi umuhimu wa kufikiri na kuchambua – sifa ambazo sinatiliwa umuhimu na waajiri.

Biashara yako haiwezi kubadilisha mfumo wa elimu Tanzania, ila unaweza ukachukua hatua mbali mbali kwenye mchakato wa kuajiri ili kuwa na nafasi kubwa zaidi ya kupata wafanyakazi bora. Hatua 8 zitakazo kuhakikishia kwamba utakuwa na wafanyakazi bora ni:

1. Fikiria ni mtu wa aina gani anyehitajika

Kabla ya kuandika maelezo ya kazi, tumia muda kufikiria mfanyakazi unayemwajiri awe na sifa zipi. Zaidi ya ujuzi inayohitajika kujaza nafasi hiyo, sifa gani zingine na ujuzi zitakuwa na umuhimu kwa kampuni na kwake? Tuna tafuta mtu mwenye utu gani?

Kwa mfano, nafasi hii ya kazi inahitaji mtu mwenye motisha, anayefikiria namna ya kukuza biashara yako pamoja na kufanya kazi zinazohitajika na kuongoza wenzake? Au unamtafuta mchapakazi haswa anayeweza kufuata maelekezo kwa kiundani?

Pamoja na hayo, usisahau kufikiria hizi pia:

 • Inabidi mfanyakazi awe na hamu ya kupandishwa cheo na kuwa na majukumu mengi zaidi?

Kama kazi iliyotangazwa inaonyesha njia ya kupandishwa cheo, basi wafanyakazi wanaotaka kujiendeleza na walio tayari kufanya kazi ili wafanikiwe, ni muhimu. Ila kama kazi haionyeshi nafasi ya kupandishwa cheo basi mfanyakazi atakayefaa kazi hiyo inabidi asiwe mtu ambaye anatafuta kupandishwa cheo kwa kuwa ataboreka haraka.

 • Mfanyakazi wako inabidi awe na sifa gani?

Kujisikia vizuri ofisini huchangia kuridhishwa kwa wafanyakazi. Kwa hiyo ni muhimu kuelewa utamaduni wa kampuni ukoje.

Pia, ni muhimu kutafuta mtu mwenye sifa binafsi (utu) inayolingana na nafasi ya kazi iliyotangazwa. Kwa mfano, kazi ya kuuza haitakiwi kwenda kwa mtu anayeona aibu au mwenye fujo sana.

2. Andika maelezo ya kazi mazuri

Ukishaelewa na aina gani ya mfanyakazi unayemhitaji, utakuwa tayari kuandika maelezo ya kazi.

Kawaida, maelezo ya kazi yanaongelea mahitaji ya kazi, elimu pamoja na miaka ya uzoefu wa kazi yanayohitajika. Kwa kuongelea haya tu, mwajiri anaweza akakosa wafanyakazi wazuri wasio na shahada au uzoefuwa kazi (kwenye sekta hiyo) unayohitaji.

Kwa mfano, mtu ambaye amejifunza Graphics hatakuwa na shahada ila ataonyesha kwamba anajituma kwa sana nad hivyo, amejipatia uzoefu pia. Kwenye dunia inayobadilika kila siku, waajiri wa hapa Tanzania inabidi watambue kwamba kwa kuwa mtu mwenye shahada ndiye anayestahili kupewa kazi kuliko mtu mwingine.

Pia, hii nijia mbovu ya kujitangaza kwa kuwa wafanyakaziwenye uwezo wanatuma maombi ya kazi kwa zile nafasi ambazowanaweza wakapata. Hawpotezi muda kuomba kazi kama wanajua kwamba hawawezi kuipata au hawana sifa zinazohitajika.

Kwa hiyo, ukiwa unaandika maelezo ya kazi, jaribu kutumia maneno yatakayomkaribisha watu walijiendeleza kielimu na watu wenye uzoefu nje ya elimu. Njia moja ya kufanya hivi ni kusema ‘Uzoefu na _________ inapendekezwa ila sio lazima, kama unaweza kuonyesha kwamba _________”. Hii itawasaidia waomba kazi kutarajia mahitaji ya kazi hiyo. Hii itawavutia wale ambao wanatafuta kazi ya aina hiyo.

3. Majaribio ya ujuzi

Hapa Tanzania, waajiri wanapokea zaidi ya maombi ya kazi 100 kwa nafasi moja ya kazi! Hii inaongeza ugumu kuwatambua wafanyakazi wazuri.

Suluhisho kwa hili kuwapa waombakazi wote mitihani kwenye ujuzi muhimu na baada, kuangalia CV na barua za kuomba kazi za wale waliojitahidi kwenye mtihani.

Chombo bora kwa ajili hii ni mitihani ya AMCAT. AMCAT ina mitihani ya:

 • Uwezo wa kuongea na kuandika kiingereza, na ujuz wakuwasiliana.
 • Mantiki
 • Uwezo wa kuchambua
 • Ujuzi wa kazi maalum: Kwa mfano, kama unataka kumajiri meneja masoko, kuna mtihani wa masoko.

Jifunze zaidi kuhusu AMCAT hapa

4. Tangaza kwenye sehemu mbalimbali

Zaidi ya kutangaza kwenye tovuti ya kampuni na kwenye ukuruasa zenu kwenye mitandao ya kijamii, pia tumia:

ZoomTanzania ina shirika la kuajiri na inatoa huduma na suluhisho zote zitakazo kusaidia kupata wafanyakazi bora! Wasiliana na recruitment@zoomtanzania.com kuanza.

5. Fanya ukaguzi wa waombakazi

Udanganyifu wa waomba kazi si jambo la kushangaza. Na hapa Tanzania, waajiri huwa hawafanyi ukaguzi wa wafanyakazi na hivyo, wanasaidia hawa wadanganyifu wasigundulike.

Kwa hiyo, kabla ya kumwita mgombea kwenye interview, fanya ukaguzi ukizingatia:

 • Historia ya uhalifu
 • Ukurasa zake za mitandao ya kijamii
 • Wapigie wafanyakazi zake wa zamani
 • Wasiliana na referee zake
 • Andika jina la kwenye Google alafu anagalia majibu gani yanatokea

6. Uliza maswali ya kawaida yaliyosahihi

Pitia orodha hii ya maswali ya kawaida ya kuuliza kwenye interview kujua ni maswali gani unayopaswa kuuliza.

7. Fanya interview na wafanyakazi wenzako

Kuna uwezekano mkubwa wa kwamba mfanyakazi wako mpya atafanyakazi na kundi la watu ndani ya hiyo kampuni. Kwa hiyo, wahusishe wale watakao fanya kazi naye kwenye interview.

Wanaweza wakawa na maswali maalum yanayohusika na jinsi au mazingira gani mfanyakazi huyo anapenda kufanya kazi, utu wake pamoja na mengina ambayo wewe labda hukufikiria. Pia, wataweza kuhisi kwa ubora zaidi kama wataweza kufanya kazi pamoja. Ni muhimu kuhakikisha kwamba mfanyakazi wako mpya ataiweza kazi hiyo na kuendana na maadili ya kampuni.

8. Waonyeshe kwamba unajali

Ukiamua ni mfanyakazi wa aina gani unayemtaka, ni kazi yako kuwashawishi kukubali kuchuua nafasi hiyo. Kwa hiyo hakikisha:

 • Unawalipa vizuri (kulingana na ujuzi wao, uzoefu wao na majukumu ya kazi)
 • Wanapata mahitaji yao ya msingi (bima ya afya, pensheni, mapumziko n.k)
 • Kuna faida za ziada kama mafunzo, nafasi za kuongeza kipato n.k

Wafanyakazi wako watajenga biashara yako

Waswahili wanasema, “chombo hakiendi ikiwa kila mtu anapiga makasia yake.”Biashara yoyote ile, bila kujali ubora wa bidhaa au huduma inayotoa, haiwezi kufanikiwa bila wafanyakazi bora.

Kwa hiyo ni muhimu kwamba unawaajiri wafanyakazi bora ndani ya bajeti yako ili biashara yako ifanikiwe zaidi.

Bahati nzuri, shirika letu la kuajiri, ZoomTalent, inaweza kusaidia na hili! Wasiliana na: recruitment@zoomtanzania.com kwa maelezo zaidi.

 

Iman Lipumba
A digital storyteller, experienced in creating content that improves website visibility on search engines, enhances the user experience, and nurtures brand loyalty. With a background in the social sciences, an expert in researching complex ideas, and communicating them in engaging language to multiple audiences.