Miji – Vitu vya kujua kuhusu Dar es Salaam

  | 3 min read
0
Comments
721

‘Nyumba ya amani’, au Dar es Salaam, ni mji mkubwa kuliko vyote Tanzania na mji mkuu wa kibiashara wa Tanzania. Ilianza kuwa senta muhimu ya kifedha na kiuchumi kabla na hasa baada ya Vita Kuu 1. Baada ya vita hiyo, Dar kuliendelea kuwa mji mkuu wa kibiashara, hadhi iliyonayo hadi leo hii.

Hivi sasa, Dar ni mji ulichangamka na unao nawiri. Ina idadi ya watu zaidi ya 4m na mji wa tatu yenye ukuaji wa kasi zaidi Africa, na wa tisa duniani. Bandari laki ni ya pili Afrika Mashariki kwa utumiaji na utakshika nafasi ya kwanza hivi karibuni. Kwa kifupi, uwezo wa mji unaonekana kwa wote.

Pia, Dar imekuwa ikitembelewa na watalii kwa wingi zaidi hivi karibuni. Kwa nini? Sababu zifuatayo zimechangia:

  1. Fukwe zenye mvutio – hasa kaskazini na kusini mwa mji
  2. Visiwa – unaweza kutembelea visiwa vya Mbudya na Bongoyo vyenye urembo wa aina yake kiurahisi (na kwa bei chee)
  3. Hali ya hewa – Kwa kifupi, jua lina waka karibia siku zote na hainyesha mvua sana kwa mwaka
  4. Zanzibar iko karibu – Zanzibar ni masaa mawili kwa boti au daka 20 kwa ndege kutoka Dar. Kwa hiyo, ukitaka kwenda sehemu yenye utulivu zaidi, unaweza kufanya hivyo kiurahisi.

Pia kuna sababu zingine za kupatembelea Dar, sababu ambazo si za kawaida, kama zifuatayo:

Kupanda Daladala

Daladala ni basi ya umma na nyingi zinatumika na watu wengi Dar. Ni usafiri wa umma ulioenea zaidi mjini na ni bei chee. Sasa, madereva wa daladala wanajulikana kwa uendeshaji wao wa aina yake. Ila, ijaribu mara moja angalau. Nadhani utakuwa na stori moja au mbili za kuwaambia marafiki zako.

Chakula cha kitanzania na cha mtaani

Ugali, ndizi, nyama choma au chipps mayai? Hizi vyakula nne utakazo zikuta popote Dar. Kuna vyakula vingine vingi vya nyumbani kama makande, makange, muhogo na kiti moto – ila hizo nne zilizotajwa kwanza ndio zenyewe!

Pitia migahawa ya Kitanzania hapa

Angalia bendi

Kuna bendi nyingi sana Tanzania, na nyingi zimejitokeza ndani ya miaka mitano ya yaliopita. Huwa zinapiga kwenye baa kubwa kwenye siku za wikiendi. Kwa sasa hivi Skylight Band ndio bendi inayoongoza nchini.

Kunywa Konyagi

Tanzania ina pombe safi zinazouzwa kote nchini, hasa bia. Ila, pombe kali ya Konyagi inayotengenzwa kwa miwa na huitwa ‘roho ya taifa’, ni ya aina yake. Na huwezi kuja Dar, huwezi kuja Tanzania bila kuijaribu. Ni kali na inanyweka vizuri na toniki na barafu.

Nenda kwenye Send-Off

Ukibahatika kupata nafasi ya kwenda kwenye send-off, nenda! Ni sherehe ya kiharusi ambayo familia ya bibi harusi inamumuaga. Ni sherehe iliyo Tanzania pekee kwa hiyo, lazima itakuwa tofauti kwako.

Angalia mechi ya mpira wa miguu kati ya Yanga na Simba

Yanga na Simba ni timu za mpira wa miguu kubwa Tanzania. Zote zinatoka Dar es Salaam na zina upinzani mkubwa  sana. Kwa hiyo, wakikutana huwa na siku ya kukumbuka kwa mashabaki yao na wa mpira wa kitanzania. Pia, kwa mgeni, na mpenzi wa mpira kwa ujumla, itakuwa siku ya kukumbuka kuanzia kwenye mpira wenyewe hadi kwenye matani kati ya mashabiki wao kabla, wakati na baada ya mechi.

Burudani na wakati mzuri zinakusubiri Dar. Iwe ufukweni, visiwani, kwenye baa na migahawa, kokote kule utapata sehemu za burudani na starehe. Ni mji uliochangamka na unaoendelea kuchangamka!

Jua zaidi kuhusu historia na utamaduni wa Dar hapa

Iman Lipumba
A digital storyteller, experienced in creating content that improves website visibility on search engines, enhances the user experience, and nurtures brand loyalty. With a background in the social sciences, an expert in researching complex ideas, and communicating them in engaging language to multiple audiences.