Miji – Vitu 10 usivyojua kuhusu Mwanza

  | 2 min read
0
Comments
2239

Mwanza, au ‘Rock City’ kwa mujibu wa wenyeji, inajulikana kwa kuwa njiani kwenda Serengeti. Ila mji inayoizunguka Ziwa Victoria lina mengi zaidi. Kwa mfano:

1.

Mwanza ni mji unaokuwa kwa kasi zaidi Afrika Mashariki na ni ya pili kati miji mikubwa Tanzania.

2.

Mwanza inajulikana kama ‘Rock City’ kwa kuwa kuna sehemu nyinge mikusanyo ya mawe makubwa kwenye mji huu; zikiongozwa na Bismarck Rock.

Kujua zaidi, pitia tovuti ya Living Water.

3.

Wasukuma, ambayo ni kabila kuu Mwanza, ni kabila kubwa kuliko zote Tanzania.

4.

Kirumba, soko kubwa zaidi la samaki katika Afrika Mashariki na Kati, iko Mwanza.

5.

Mti maarufu iitwayo ‘The Hangman Tree’ ambapo wafungwa na wahalifu walikuwa wanyongwa, ni vutio kubwa kwa watalii.

6.

Ongezeko la utalii umetokea kwa kuwa Mwanza ina mandhari mazuri na iko karibu mbuga za wanyama (Serengeti ikiwa ya kwanza).

7.

Mahinda, muhogo na viazi ni 71% ya mazao ya chakula zinazopandwa huko.

8.

Kisiwa cha Ukerere, uliopo Mwanza, ni nyumbani kwa ‘dancing rocks’ (miamba yanayocheza). Ila kiutamaduni, wanaume tu ndio wanaruhusiwa kuzitembelea.

9.

Kipande cha Ziwa Viktoria, ya pili kwa ukubwa duniani, inapita Mwanza.

10.

Mji huu ulijulikana duniani baada ya dokumentari inayoitwa Darwins Nightmare ilionyesha jinis gani samaki ya Nile Perch (sangara) ilikuwa inaathiri maisha asili ya baharini Mwanza.

Mji umekuwa kwa kasi sana kulingana na miji mingine Afrika. Inagawa haipati sifa kama Dar au Arusha, ina vitu vingi vya kujivunia.

Iman Lipumba
A digital storyteller, experienced in creating content that improves website visibility on search engines, enhances the user experience, and nurtures brand loyalty. With a background in the social sciences, an expert in researching complex ideas, and communicating them in engaging language to multiple audiences.