Miji – Unachohitaji kujua kuhusu Arusha

  | 2 min read
0
Comments
644

Ukiwauliza watuwengi kusema chochote wanachokijua kuhusu Arusha, sana sana watasema kwamba ni nyumbani kwa mbuga za wanyama maarufu.

Ila, kuna mengine yakujua kuhusu Arusha.

1. ‘Chimbuko la Binadamu’

Fuvu ya binadamu ya zamani kuliko zote ilipatikana Olduvai Gorge, iliyopo Arusha Tanzania.

2. Senta ya Urithi wa Utamaduni

Ikiwa nje na mjini, senta hii inamwezesha mtu kuangalia sanaa na utamaduni wa zamani na wasasa hivi.

Pia inajulikana kwa usanifu wake wa ajabu.

3. Ni nyumbani kwa ICTR

Kwa zaidi ya miaka 10, Arusha imekuwa nyumbani kwa ICTR. Kazi ya mahakama haya ni kuwajibisha wote walihusika na mauaji Rwanda mwaka 1994.

4. Katikati ya Afrika

Mnara wa saa ulio mjini ilijengwa hapo ilipo kwa kuwa ni katikati ya Cairo na Capetown.

5. Hollywood inapapenda Arusha

Sinema ya ‘Hatari’ iliyo ongozwa na Howard Hawks ili rekodiwa Arusha. Nyota ya filamu hii alikuwa John Wayne, na alilala kwenye hoteli ya Safari Hotel (inaitwa New Safari Hotel siku hizi). Hotel hiyo imekuwepo tangu 1935.

6. Mbuga inayojulikana duniani

Huffington Post iliitambua Mbuga ya Kilimanjaro katika mbuga za wanyama 35 bora duniani.

7. Mlima Kilimanjaro

Ni ngumu sana kutaja Mbuga ya Wanyama ya Kilimanjaro bila kutaja mlima yenyewe. Watu 35,000 wanajaribu kuipanda kila mwaka ila chini ya nusu yao wanafanikiwa

8. Nyumbani kwa Tanzanite

Kito johari ya Tanzanite inapatikana Arusha, Tanzania tu! Ni kati ya vito johari 3 duniani zinazopatikana ndani ya nchi moja tu.

9. Past meets present

Makumbusho ya taifa yaliyopo Arusha ilikuwa ngome iliyojengwa na wajerumani kwenye miaka ya mwanzo ya 1900.

10. Shanga Shanga

Shanga Shanga ni kati ya miradi ya kwanzai zinazojaribu kuongeza uelewa wa vilema Tanzania, na pia kuwapa nafasi za kazi.

Nia yao ni kuwa na biashara ya haki na endelevu.

Haya, hizo ni ukweli 10 za kihistoria na kitamaduni kuhusu Arusha. Kawa hujawahi kufika huko, huna sababu ya kutokwenda sasa!

Pitia hoteli hizi safi zenye bei nzuri.

Iman Lipumba
A digital storyteller, experienced in creating content that improves website visibility on search engines, enhances the user experience, and nurtures brand loyalty. With a background in the social sciences, an expert in researching complex ideas, and communicating them in engaging language to multiple audiences.