Migahawa Mizuri Vya Kumpeleka Mpendaye

  | 3 min read
0
Comments
2530

Badala ya kwenda kuangalia sinema, ambapo hutaweza kuongea vizuri na mgeni wako au kwenyen mgahawa iliyojaa na watu, chagua sehemu itakayo waruhusu kujuana zaidi.

Kwa kukusaidia, zifuatayo ni migahawa 10 zinazofaa kumpeleka mpendaye kwa mtoko wen wa mara ya kwanza.

Mbalamwezi Beach Club, Mikocheni

Bei $$

TZS 7,000 – TZS 20,000

Hii ni mgahawa maarufu iliyo fukweni . We na mpendaye mnaweza kukaa kwenye mchanga kabis mkiangalia bahari au kwenye viti mkifurahia chakula, vinywaji na upepo wa bahari.

Kama unatafute sehemu iliyo tulia, utapapenda.

Jua zaidi kuhusu Mbalamwezi hapa

News Café, Masaki

Bei $$$

​TZS 15,000 – TZS 45,000

Kama unatafuta sehemu ya kisasa inayovutia, News Café ndiyo penyewe. Chakula na vinywaji vyao vinaendana na bei zao. Pia, huduma yao ni safi.

Jua zaidi kuhusu News Café hapa

Havana Café, Msasani Peninsula

Bei $$$

​TZS 15,000 – TZS 30,000

Hii ni mgahawa inayojulikana, lakini hapa tembelewi sana na watu wengi, kitu ambacho utafurahia ukiwa na mpendaye. Ina mandhari ya kicuba na kumetulia. Wana vyakula na vinywaji vya aina nyingi na huduma yao ni ya kipekee.

Jua zaidi kuhusu Havana Café hapa

Oasis Wine Bar & Coffee House, Masaki

Bei $$

​TZS 15,000 – TZS 30,000

Kumepambwa na picha na uchoraji wa kiafrika, zinazochangia kuweka mandhanri ya kinyumbani nay a kukaribisha. Zaidi ya kufurahia huduma yao kwa ujumla, chakula chao ni kizuri sana na wana mvino na whiskey za aina nyingi. Pia, mmiliki na meneja ni mchangamfu sana. Kwa kifupi, Oasis iko poa sana.

Jua zaidi kuhusu Oasis hapa

Msumbi, Masaki

Bei $$

TZS 5,000 – TZS 15,000​

Kama unatafuta sehemu ya kwenda mchana, basi mpeleke mpenday Msumbi. Mtafurahia kahawa na chai yao, pamoja na chakula chao cha mchana. Pia, kuna stuli, viti na makocha zinazoongeza faraja pale.

Jua zaidi kuhusu Msumbi hapa

Velisa’s Jamaican Restaurant, Kawe

Bei $$

TZS 20,000 – TZS 35,000

Ikiwa na mtazamo mzuri wa bahari na pwani, Velisas ni moja kati ya migahawa yaliyo na mandhari ya kimapenzi. Chakula chao ni kizuri ni tofauti, kwa kuwa ni cha kijamaika. Pia, wanaweza wakakuandalia meza fukweni, ukala pale na mpendaye mkiangalia nyota angani.

Jua zaidi kuhusu Velisas hapa

Addis in Dar

Bei $$$

TZS 15,000 – TZS 25,000

Kama unataka kufanya cha ziada, mpeleke mpendaye Addis In Dar kula chakula cha kiethiopia. Chakula chao ni ya aina yake na utafurahia huduma yao.

Jua zaidi kuhusu Addis In Dar hapa

High Spirit, City Center

Bei $$$

TZS 18,000 – TZS 40,000

Inagawa kuna changamka kati ya Ijuma na Jumapili, ukija hapa siku yoyote kabla, utafurahia muziki wao na hasa mtazamo wa mji wa Dar es Salaam.

Jua zaidi kuhusu High Spiti hapa

Coffeesha, Barabara ya Ali Hassan Mwinyi

Bei $

TZS 5,000 to TZS 15,000

Kama wewe na mpendaye mnapenda sehemu iliyotulia yenye kahawa na vitafunio vizuri, Coffeesha kutawafaa.

Jua zaidi kuhusu Coffeesha hapa

Rudy’s Farm, Bahari Beach

Bei $$

TZS 7,000 – TZS, 15,000

Rudy’s Farm ni sehemu tulivu yenye nyama ya kuchoma ya kipekee na vinywaji kwa bei nzuri. Hii ni sehemu ya kwenda na mpendaye mburudike bila shida, ambapo mtaweza kujuana vizuri zaidi.

Jua zaidi kuhusu Rudy’s hapa

Vitu tunavyofanya kwa ajili ya mapenzi

Kutafuta sehemu nzuri ya kumpeleka mpendaye ni kazi ngumu, ila sababu za kufanya zinathamani.

Tafuta migahawa mingine kupita orodha yetu ya biashara

Iman Lipumba
A digital storyteller, experienced in creating content that improves website visibility on search engines, enhances the user experience, and nurtures brand loyalty. With a background in the social sciences, an expert in researching complex ideas, and communicating them in engaging language to multiple audiences.