Mbuga ya wanyama ya Selous – Ukweli, Makala na Zaidi

  | 2 min read
0
Comments
4984

Selous ni mbuga ya wanyama kubwa kuliko zote Tanzania na ni nyumbani kwa tembo nyingi, vifaru vyeusi, viboko na aina mbalimbali za ndege. Ikiwa imegawanywa na Mto wa Rufiji, ni pazuri kwa kuangalia wanyama wanaokaa kwenye maji. Hapajajaa kama mbuga nyingi za kaskazini na hivyo, imehifadhi nyika zake zaidi.

Mbuga ya wanyama ya Selous – Ukweli, Makala na Zaidi
Features

Size: 
54,600 sq km (21,100 sq miali).

 

Iko kusini mwa Tanzania, mashariki wa kisiwa cha Mafia kwenye Mto wa Rufiji.

 

Getting to: 
Kwa gari aina ya 4WD, kwa safari ya ndege ya lisaa limoja kutoka Dar au kwa treni kutoka Kisaki.

Accomodation & Services

 

Kwa nini upatembelee Selous?

Mwaka 1982, mbuga ya Selous ilipewa taji ya kuwa World Heritage Site ya UNESCO kwa kuwa ina wanyama wengi tofauti na mazingira yakiwa yamehifadhiwa vizuri. Uingiaji na utokaji wa watu unadhibitiwa na idara ya Wanyamapori wa Wizara ya Maliasili na Utalii ya Tanzania.

Tembo, viboko, nyati aina ya cape na mambo yapo hapo kwa wingi zaidi kuliko mbuga yoyote nyingine Afrika.

Inagawa idadi ya wanyamapori ni kubwa, hakuna msongamano wa wanyama kwa kuwa eneo yenyewe ni kubwa.

Sehemu za kutembelea ndani ya mbuga hii ni Mto wa Rufiji, linalo kutana na Bahari ya India, ikiangaliana na Kisiwa cha Mafia na Stieger Gorge, ambayo ni korongo inayokwenda chini kwa 100m na yenye upana wa 100m. Mazingira ya asili yaliopo ni pamoja na nyika, Acacia Savanna ya kawaida, maeneo ya oevu na misitu ya Miombo.

Sasa unasubiri nini? Anza kupanga safari yako sasa hivi!

Iman Lipumba
A digital storyteller, experienced in creating content that improves website visibility on search engines, enhances the user experience, and nurtures brand loyalty. With a background in the social sciences, an expert in researching complex ideas, and communicating them in engaging language to multiple audiences.