Mbuga ya wanyama ya Ruaha: Ukweli, Makala na Zaidi

  | 2 min read
0
Comments
1649

Mbuga ya wanyama ya Ruaha inafikiwa kirahisi kwa kuwa iko katikati ya nchi. Wanyama watano kuu wote wanaonekana hapa. Katika msimu wa kiangazi, wanyama wanaotafuta maji wanakutana na mhasimu. Katika msimu wa Masika, ndege na mimeo vinajitokeza kwa wingi.

Mbuga ya wanyama ya Ruaha: Ukweli, Makala na Zaidi
Features

Size: 
10,300 sq km (3,980 sq maili). Inashika nafasi ya pili Tanzania kwa ukubwa kati ya mbuga zote.

 

Iko katikati ya Tanzania, 128km (80 maili) magharibi ya Iringa.

 

Getting to: 
Inaweza ikachukua masaa 10 kwa gari au lisaa limoja na nusu kwa ndege kutoka Dar.

 

Best time to visit: 
Kwa mahasimu na mamalia wakubwa, Mei mpaka Desemba. Kwa kuangalia ndege, kutazama mandhari na mimea zenye urembo wa kipekee, January mpaka Aprili.

 

Accomodation & Services

 

Kwa nini upatembelee?

Kumepanuliwa hivi karibuni ili iwe mbuga ya wanyama kubwa Afrika  Mashariki. Pia, ni nyumbani kwa wingi usiofikiwa wa tembo.

Mto mkubwa wa Ruaha iliyo mashariki mwa mbuga hii ndio chanzo cha  maisha cha wanyama wengi ndani ya mbuga hii. Katika msimu wa Kiangazi,  pundamlia, nyati, swala na wengine wanatembea kwenda mtoni ila wanashambuliwa na mahasimu kama simba, chui, fisi na duma.

Ruaha ni maarufu pia kwa kuwa ina swala nyingi tofauti  pamoja na aina 450 ya ndege.

Sasa unasubiri nini? Anza kupanga safari yako sasa hivi!

Iman Lipumba
A digital storyteller, experienced in creating content that improves website visibility on search engines, enhances the user experience, and nurtures brand loyalty. With a background in the social sciences, an expert in researching complex ideas, and communicating them in engaging language to multiple audiences.