Mbinu 3 za Kutafuta Ajira ambazo Mtafuta Ajira Inabidi Azijue

  | 4 min read
0
Comments
3919

Hivi, ni kwa nini kutafuta ajira Tanzania ni kazi ngumu sana?

Ukweli ni kwamba kuna watu wengi zaidi ya kazi zilizopo.

Kwa wastani, kwa kila nafasi moja ya kazi inayotangazwa, zaidi ya maombi mia yanatumwa. Zaidi ya hapo, ukosefu wa ajira ni zaidi ya 10% na ukosefu wa ajira kwa vijana ulikuwa 13.7% mwaka 2014. Kwa hiyo, mtu anaweza kukatishwa tamaa kiurahisi.

Ila, wale wanaopata ajira na vyeo vizuri kwenye makampuni mbalimbali, huwa wana sifa moja ambao watafuta ajira wengine hawana – kujituma.

Hawa wenye mafanikio haya hawataki kuchaguliwa kutoka kwenye kundi la watafuta ajira wengi. Badala yake wanajitahidi kujipa nafasi ya kuonekana zaidi kwenye mchakato wote wa kutafuta ajira. Uzuri ni kwamba wote tunaweza kujifunza na kujuizoesha kujituma.

Zaidi ya kutumia njia za kawaida kutafuta kazi, kwa mfano:

Kuingia ZoomTanzania > Kupitia kazi zilizopo > Kutuma maombi > Kusubiria jibu

Kuna hatua zingine unazoweza kuchukua ili kugundua nafasi zingine za kazi, na hivyo kuweza kutuma maombi mengi zaidi.

Kwa hiyo, kama unatafuta ajira kuna vidokezo 3 ambazo unapaswa kutumia ili kuajiriwa kwa haraka zaidi.

 1. LinkedIn

Ingawa mitandao ya kijamii na intaneti kwa ujumla ni rasilimali nzuri kutafuta ajira, LinkedIn hasa ni chombo muhimu kwa mtu yoyote anayetafuta ajira. Mpaka sasa, LinkedIn haitumiwi inavyopaswa kutumiwa Tanzania.Watu wengi wanaitumia kama Facebook, kama njia ya kujiunganisha na wafanyakazi wanaovutia na kuongelea shughuli zao za kila siku.

Badala yake, wafanyakazi wanpaswa kutumia LinkedIn kama CV yao. Watumie vipengele vya utafutaji na ‘groups’ kutafuta na kuwasiliana na wafanyakazi wengine kwenye sekta yao.

Zaidi ya hapo, makampuni mengi zaidi yanatumia LinkedIn kutafuta wafanyakazi. Kwa hiyo, hakikisha ukurasa yako ya LinkedIn imekamilika. Itawasaidia waajiri kukutafuta

Vidokezo vya LinkedIn ni:

 • Kamilisha ukurasa wako
 • Weka picha inayokuonyesha vizuri
 • Ukitaka kuunganishwa na mtu usiyemjua, mwandikia ujumbe wa kujitambulisha.
 • Jenga tabia ya kupost habari za kazi au sekta yako mara mbili kwa wiki na pia, toa maoni juu ya post za watu wengine
 • Kama unajaribu kujijengea jina, jaribu kuandika na kuchapisha makal ya LinkedIn angalau mara moja kwa mwezi (hakikisha zina husika na kazi na sekta ya kazi uliopo)
 1. Boresha Ujuzi Wako

Ukikuta kwamba kwa nafasi za kazi unazozitaka, unakosa ujuzi wa kutosha kwa 25% labda maa 3 mfululizo, utafanyaje?

Watafuta ajira wanaojituma watatumia muda wao kujifunza hiyo 25% wanayokosa.

Watafuta ajira wengia wanaweka malengo yao yote kwenye kutafuta ajira, mpaka wanasahau kuboresha ujuzi wao. Kufuatilia blog za sekta husika, kusoma pamoja na kufanya kozi za zinazo onyeesha mwelekeo upya, zitakuongezea nafasi ya kupata ajira.

Sehemu moja watafuta ajira wa kitanzania wanapohitaji kujiboresha ni kwenye kuongea na kuandika Kiingereza. Kujiongezea ujuzi hapa kutakusaidia kuwania nafasi za kazi ambazo usingeweza kuwania kabla.

Na kama utafanikiwa kuitwa kwenye interview, waambie waajiri kwamba umejifunza. Hii itaonyesha kwamba unajituma pamoja na kwamba kweli unaitaka hiyo kazi.

Pia, kusoma kitu kinachohusika na kazi unayoitaka pamoja na kupata vyeti itak=fanya uonekane zaidi kwa mwajiri. Kwa mfano, AMCAT ni mtihani inayojulikana kimataifa ya kuwasaidia watafuta ajira kwa kuonyesha thamani yako kwa waajiri. Ina pima:

 • Ujuzi wa Kiingereza na mawasiliano
 • Kiwango wa kuchambua, wa mantiki na wa kufikiri
 • Utaalamu wa sekta/kazi unayoomba
 • Utu wako kuendana na mahitaji ya kazi unayoomba na maadali ya kampuni

Kwa hiyo, ukijitahidi kwenye mtihani wa AMCAT, itawaonyesha waajira kwamba wewe una sifa zinazohitajika.

Fanya mtihani wa AMCAT na ongeza nafasi yako kuajiriwa

 1. Tumia mtandao wako, sio upendeleo

80% za nafasi za kazi hazitangazwi.

Sasa, hizo nafasi zinajazwaje? Kwa mapendekezo.

Ila, hii sio sababu ya kuwapendelea ndugu zako. Badala yake, tumia marafiki, familia, na wengine kuwa ‘wapiga debe’ wako ili kama nafasi ya kazi inajitokeza na unasifa za kuijaza, we ndio unayetafutwa kuijaza.

 • Wataarifu marafiki, ndugu, watu uliosoma nao na wengine kwamba unatafuta ajira, aina ya ajira unayotafuta na sifa zako za kazi.
 • Kama unamjua mtu kwenye kampuni fulani, mtumie CV yako na umwombe akutaarifu kama nafasi ya aina itakayo kufaa itajitokeza
 • Jitolee kufanya kazi kwenye kampuni alafu mwombe mmiliki/mkurugenzi mtendaji akuongelee kwa waajiri wenzake.

Kujituma kutakufikisha mbali kwenye kutafuta kazi

Wengi wetu tunajua ugumu wakutafuta kazi Tanzani. Ingawa kutafuta kazi kwa njia ya kawaida inawatosha watu wengine, wale wanaojituma zaidi ndio wanaopata kazi wanaotaka, na sio kazi tu yakuwapatia mshaara.

Kwa hiyo, pumzika kidogo kwenye kuomba kazi alafu jiulize: Nifanyeje kuongeza uwezo wangu wakuajiriwa? Je, nimefanya kila ninachoweza kupata ajira hii? Nifanye nini kuwa mgombea bora wa kazi hii?

Ukishafikiria vyote, fikiria kufanya mtihani wa AMCAT na boresha nafasi yako ya kuajiriwa kwa kiasi kikubwa.

Iman Lipumba
A digital storyteller, experienced in creating content that improves website visibility on search engines, enhances the user experience, and nurtures brand loyalty. With a background in the social sciences, an expert in researching complex ideas, and communicating them in engaging language to multiple audiences.