Matumizi ya Mafuta – Siri za kupunguza gharama za mafuta

  | 2 min read
0
Comments
2776

Matumizi ya mafuta ni gharama ya kila wiki unayobidi kulipa. Hasa ukizingatia foleni. Pia, usafiri wa umma bado ni tatizo kubwa.  Ila, sio lazima gharama hii ya mafuta iwe kubwa sana.

Kuna njia tofauti ya kupunguza gharama hii:

1. Kuendesha kwa kasi inaongeza gharama

Madereva wengi Tanzania wanpenda kuendesha kwa kasi na kupita magari mengine hata kama haihitajiki. Pia kuendesha kwa kasi na kwisha kubreak ghafla ni matumizi mabaya ya mafuta. Kadri unavyokanyaga kichapuzi, mafuti mengi zaidi yanatumika.

Ni bora uongeze mwendo pole pole, na hivyo kupunguza matumizi ya mafuta.

2. Zima gari yako na kuiwasha ukiwa tayari kuitumia

Iwapo unamsubiri mtu kwenye parking au unasubiri chakula barabarani, madereva wengi wa Tanzania wanapenda kuacha gari ikiwa imewashwa bila sababu.

Kwa kifupi, kama umepaki na unasubiria kitu, zima injini na okoa mafuta. Kwa kuwa gari yako haitembei haimaanishi kwamba mafuta hayatumiki.

3. Zima AC

Sasa, hii inaleta changamoto kidogo kwa kuwa Tanzania ni nchi yenye joto sana, hasa pwani. Ila, utafiti uliofanywa na Wizara ya Nishati Marekani iligundua kwamba AC inaweza ikatumia 25% ya mafuta yako. Sasa, hiyo ilikuwa marekani. Tanzania je?

Shusha vioo hizo!

4. Cheki presha ya matairi

Kama tulivyosema kwenye vidokezo vya kudumisha gari yako, kuhakikisha kwamba matairi yako yana presha ya kutosha itapunguza uzito wa gari lako na hivyo, utaokoa matumizi ya mafuta. Kwa hiyo hakikisha unacheki presha ya matairi kila mwezi.

5. Jitahidi kuifanya  iwe nyepesi

Wengi wetu tunageuza gari yetu kuwa nyumba yetu ya pili. Ila, gari yako ikiwa nyepesi haihitaji nguvu nyingi kuongeza kasi, na hivyo inatumia mafuta machache zaidi.

Kwa hiyo, usiijaze na vitu bila sababu maalum.

6. Usinunue mafuta mengi sana

Baadhi ya watu wanaamini kwamba ni bora kuweka mafuta mengi kwa wakati mmojo badala ya kuongeza kidogokidogo. Tatizo linalokuja ni kwamba Kwa kujaza gari yako na mafuta, unaongeza uzito wake. Kwa hiyo, usiijaze mpaka mwisho na vile vile usitemebee na robo tenki. Kuweka nusu tenki ya mafuta ndio bora.

Dokezo nyongeza: Kununua gari yenye matumizi mazuri ya mafuta (link) ndio suluhisho bora kuliko zote. Pia, huwa magari haya sio ghali.

Kila shilingi inahesabika

Gharama za gari hazipungui baada ya kuinunua. Kwa hiyo, ni muhimu sanaa kupunguza gharama pale unapoweza. Ingawa kuokoa TZS 100 au TZS 1000 kila unapoweka mafuta inaonekana kuwa ndogo kwa sasa hivi, baada ya miezi na miaka utakuwa umeokoa pesa nyingi. Kwa hiyo, ni matumaini yetu kwamba vidokezo vitasaidia kukupunguzia gharama ya kuwa na gari.

Iman Lipumba
A digital storyteller, experienced in creating content that improves website visibility on search engines, enhances the user experience, and nurtures brand loyalty. With a background in the social sciences, an expert in researching complex ideas, and communicating them in engaging language to multiple audiences.