Matengenezo Matatu ya Magari Ambayo Kila Mwenye Gari Anapaswa Kujua

  | 3 min read
0
Comments
24058

Kila mtu mwenye gari hafurahii akiwa barabarani na kutambua kwamba gari haliko sawa. Inakuwa mbaya zaidi ukiwa huna hakika kwamba tatizo ni nini.

Ila, matatizo ya yanayotokea huwa yana husisha vitu vitatu. Na bahati nzuri, huhitaji kuwa mtaalam wa magari kuzitengeneza.

1. Betri Iliyokwisha

Gari yako ikikataa kuwaka, kuna uwezekano mkubwa kwamba betri imekufa. Kuna sababu nyingi ya hii kutokea, zikiwemo:

 • Uliacha taa zikiwaka kwa muda mrefu
 • Nguvu ya betri haiendani na nguvu gari
 • Betri imeingia maji
 • Betri ni ya muda mrefu na imechoka

Licha ya sababu, unaweza kuwasha gari lako kwa muda mdogo kwa kufanya yafuatayo:

 • Tafuta gari lingine
 • Zime magari yote mawili
 • Fungua boneti
 • Angalia betri ilipo
 • Angalia sehemu za kukonekti nyaya
 • Toa nyaya zako za kubusti gari
 • Ambatisha upande mwekundu (positive) kwenye terminal ya positive ya betri. Ambatisha upande nyeusi/bluu (negative) kwenye terminal ya negative ya betri.
 • Washa gari la pili kwa daka 5
 • Washa gari lililo kataa kuwakaka. Ikiwaka, iache kwa daka 5
 • Toa nyaya za kubusti.
 • Endesha gari lako na kama tatizo hii itatokea tena, tembelea duka la betri ili ununue betri mpya.

2. Fyuzi Iliyoungua

Ukikuta kwamba redio, indiketa au kifaa kingine linalotumia umeme haiwaki, kunauwezekano mkubwa kwamba fyuzi imeungua. Bahati nzuri tatizo linaweza kushughulikiwa haraka:

 • Fungua boneti, utakuwa boksi ya fyuzi kwenye bay ya injini au steering wheel. Kama huioni, itafute kwenye mwongozo ya gari.
 • Toa funiko ya boksi ya fyuzi. Utaona namba tofauti na rangi kuonyesha nguvu ya kila fyuzi.
 • Tafuta alafu toa fyuzi iliyoungua
 • Unapaswa kuwa na fyuzi ya akiba kwenye gari lako. Kama huna jaribu yafuatayo:
  • Kutumia fyuzi nyingine ya nguvu hiyohiyo kutoka kwenye sehemu nyinge ya gari (kwa mfano redio), au
  • Iache gari yako mpaka utakapo kwenda gereji au kwenye duka la spea za magari ambapo unaweza kununua fyuzi unayohitaji.
 • Jaribu kuwasha gari yako kuona kama tatizo limetatuliwa.
 • Kama fyuzi ikiungua tena, ipele kwa fundi wako.

3. Pancha:

Gari yako itapata pancha mara moja au nyingine. Bahati nzuri, sio tatizo kubwa na wala haihitaji fundi.

 • Washa taa zako za dharura alafu paki gari lako kwenye eneo yenye usalama.
 • Toa vifaa vifuatayo:
  • Jeki
  • Bisibisi
  • Lug Wrench (ya kufungua tairi)
 • Toa tairi yako ya spea kutoka kwenye buti.
 • Tumia Lug Wrench kufungua gurudumu za tairi yenye pancha
 • Weka jeki chini ya gari alafu anza kuipandisha
 • Fungua tairi
 • Weka tairi ya spea alafu hakikisha unaikaza sana
 • Shusha jeki
 • Tumia lug wrench kukaza gurudumu za matairi zaidi
 • Rudisha kila kitu kwenye gari na endelea na safari yako.

Kuna wauzaji wengi wa matairi mazuri kwa ajili ya aina mbalimbali za magari.

Unaweza!

Kujifunza kuhusu gari yako na namna gani ya kufanya matengenezo madogomadogo ni muhimu sana. Kwanza hakikisha spea zote za magari unazo. Hii itakusaidia kujiamini zaidi barabarani na pia itakuokolea muda na gharama ukipata tatizo lingine ndogo.

Iman Lipumba
A digital storyteller, experienced in creating content that improves website visibility on search engines, enhances the user experience, and nurtures brand loyalty. With a background in the social sciences, an expert in researching complex ideas, and communicating them in engaging language to multiple audiences.