Maswali 9 ya Kumuliza Muuzaji Ukiwa Unanunua Gari

  | 3 min read
0
Comments
2101

Haya, umeona Toyota Passo inayouzwa ikitangazwa ZoomTanzania na umeipenda. Kinachofuata ni nini?

Ndio, unampigia simu muuzaji. Ila, sio kwa ajili ya kupanga mkutano naye, hapana, ni kumuliza maswali kuhusu gari hiyo.

Maswali ya kwanza utakayouliza yatakusaidia kuamua kama kweli unataka gari hii.

Kutegemeana na utu wa muuzaji, maongezi yanaweza yakawa magumu, hasa kama hujajiandaa vizuri. Kwa hiyo, kukuandaa ni hili, tuna maswali 9 yakumuliza muuzaji mkiwa mnaongea kwa mara ya kwanza.

1. Kwa nini unauza gari hii?

Namna atakavyo jibu swali hii inaumuhimu sawa na jibu lake kamili. Kama hawi wazi na ajibu kisirisiri, basi kuna kitu muhimu ambayo anakuficha.

2. Imetembea kwa KM ngapi?

Kabla ya kuuliza swali hii, uwe umeshapata ushauri kutoka kwa fundi anayeaminika kuhusu utembeaji wa aina ya gari hiyo. Ila, kama ni zaidi ya 32,000km/mwaka basi gari hiyo imetumika sana na hivyo inaweza ikakuletea matatizo mengi zaidi (pitia ripoti za wateja kwa maelezo zaidi).Vile vile, kama haijetembea sana uliza kwa nini. Labda imepata matatizo mengi mpaka imeshindwa kutembea.

3. Umekuwa nayo kwa muda gani?

Iwapo mwaka wa kutengeneza ni muhimu (isiwe zaidi ya miaka 10), miaka aliyokaa nayo ni muhimu vile vile.

4. Uliinunua ikiwa mpya au ikiwa imetumika?

Kama ilikuwa imetumika, mmiliki wa kabla yake aliiuza kwa sababu gani?

Kama gari imepita kwa wengi kabla yako, hii inaweza ikawa dalili ya kwamba inapata matatizo mara kwa mara.

Kama ilikuwa mpya, imewahi kuombwa irudi kiwandani?

Mara mojamoja, makampuni wataomba aina fulani ya gari irudishwe ili waiboreshe, hasa ikiwa ni swala la usalama.

5. Wewe ndio aliyekuwa akiiendesha mara nyingi?

Ni muhimu kumhoji yule mtu aliyekuwa anaitumia gari hiyo mari nyingi. Mara nyingi jinsi alivyo yeye itaonekana kwenye matunzo na hali ya ujumla ya gari hiyo.

6. Imeshawahi kupata ajali?

Kama gari imewahi kupata ajali ndogo, basi usijipe wasiwasi sana na hali yake. Ila, kama imepata ajali kubwa basi bora usiinunue. Ila, kwa chochote kile, uliza:

  • Ajali ilitokeaje?
  • Gari iliumia kwa kiasi gani?
  • Fundi gani alifanya matengenezo? Pata jina lake au la kampuni yake na namba ya simu.

7. Hali ya gari kwa ujumla ikoje?

Zaidi ya muonekano wake wa juujuu:

  • Ina matatizo yoyote ya kiufundi
  • Muuzaji anapata matatizo yoyote akiiendesha?
  • Inapiga kelele zisizoeleweka
  • Vifaa vyake vyote vina fanya kazi?

8. Kuna chochote kinacho hitaji kutengenezwa?

Majibu ya swali hii yatakusaidia kuamua kama uko tayari kwa gharama zozote za ziada, kama unataka kushusha bei au kama bado unataka kuinunua kabisa.

Kumbuka, redio isiyofanya kazi sio sawa na injini mbovu. Kwa hiyo, kama unataka kushusha bei, tumia matatizo makubwa, sio madogo, kufanya hivyo.

Pia, usijaribu kushusha bei kabla ya kuipeleka kwa fundi.

9. Unaripoti za servisi?

Ripoti za servisi zitakwambia kama muuzaji alikuwa anaijali hiyo gari na kama imetunzwa vizuri. Kawaida, gari inapelekwa servisi kila baada ya kutembea 5000km. Kama ripoti haionyeshi hivi, basi hiyo ni dalili ya kwamba muuzaji alikuwa haitunzi vizuri.

Uliza na utapewa

Wengi wetu hatuulizi maswali ya kutosha. Iwe shuleni, kwenye interview ya kazi au hata ukiwa unanunua nyumba. Kawaida yetu ni kukaa kimya. Ila, tabia hii inaweza ikatufikia pabaya, hasa ukiwa unanunua gari iliyotumika.

Kwa hiyo, tunatumaini kwamba ukianza kutafuta gari kwa kupitia tovuti yetu, maswali tuliyoelezea hapa yatakusaida ukiongea na muuzaji kwa simu.

Iman Lipumba
A digital storyteller, experienced in creating content that improves website visibility on search engines, enhances the user experience, and nurtures brand loyalty. With a background in the social sciences, an expert in researching complex ideas, and communicating them in engaging language to multiple audiences.