Makosa 10 Yatakayo Sababisha Ukose Ajira

  | 5 min read
0
Comments
2869

Karibia kila nafasi ya kazi inayotangazwa kupitia ZoomTanzania.com zinapata maombi 50 – 100 kwa wiki. Hii inaonyesha kwamba nafasi za kazi ni chache ukizilinganisha na watu wanaoomba ajira.

Zaidi ya hapo, inakuwa ngumu kufanya ombi lako lionekani zaidi ya wengine kwa kuwa:

  • Waajiri hawana muda wa kupitia maombi yote ya kazi wanazopata kwa kiundani.
  • Maombi ya kazi zinapitiwa kwa haraka kwanza na zili zinazoonekana bora huwekwa pembeni kupitiwa kwa kiundani zaidi.

Kwa hiyo, kama wewe unatafuta ajira, kazi yako kubwa ni kufanya ombi lako la kazi liwe nzuri ili utambuliwe kama moja kati ya wagombea wa nafasi hiyo. Ila, ukifanya makosa 10 yafuatayo, utaendelea kukosa ajira.

1. Kuomba kazi wakati huna sifa zinazohitajika

Maelezo ya kazi zinataja sifa, ujuzi na uzoefu unaohitajika kwa kazi hiyo. Kama umekosa sifa hizo, usipoteze muda wako kuomba kazi hiyo!

Badala yake, tumia muda wako kuboresha CV yako pamoja na barua ya kuomba kazi kwa ajili ya nafasi za kazi ambazo ziko ndani ya uwezo wako. Ila, ukiona nafasi ya kazi inayohitaji uzoefu wa kazi wa miaka kadhaa ila unaamini kwamba utaiweza na majukumu yake, basi tuma maombi ya kazi na wapigie kuwauliza zaidi.

2. Kutuma barua moja ya kuomba kazi kwa kazi zote unazoomba

Waajiri wanaweza kujua kama umewatumia barua ya kuomba kazi ambayo umewatumia waajiri wengine. Wakishahisi hivyo, wanaona kwamba hujatumia juhudi yakutosha kuomba kazi na hawatakuchagua.

Watu wanaofanikiwa kutafuta ajira wanaelewa kwamba kutuma maombi mengi ya kazi haikusaidii kupata ajira. Kinachosaidia ni ubora wa ombi lako la ajira pamoja na kama una sifa zinazohitajika. Kila kazi ni tofauti kwa hiyo hakikisha una onyesha jinsi gani uzoefu na ujuzi wako zinaendana na kazi unayoomba.

3. Unaongelea majukumu uliyokuwa nayo badala ya mafanikio

Waajiri wanataka watu wa vitendo. CV inayosema ‘Niliongeza mauzo kwa wastani wa 4% kila baada ya miezo minne’ inaweka uzito zaidi kuliko ‘nilikuwa na jukumu la mauzo”. Popote pale ukiwa na nafasi, taja mafanikio yako zaidi ya majukumu uliyokuwa nayo.

Harvard Business Review nao wanasisitiza umuhimu wakuweka baadhi ya mafanikio yako kwenye CV. Onyesha yale mafanikio yanayoendana na kazi unayoomba.

4. Kutoongelea thamani utakayoleta  kwenye nafasi unayoomba

Kusema kwamba ‘nina uzoefu wa miaka 7’ haionyeshi thamani ya uzoefu huo.

Ila, ukisema ‘nina uzoefu wa miaka 7 na majukumu yangu yaliongezwa kila mwaka. Pia, nina uhusiano mzuri na wadau wa sekta hii” inavutia zaidi ni inasaidia kuonyesha thamani utakoyeleta.

5. Kuonyesha kwamba unashida na hivyo, unahitaji ajira

Mwajiri hajali ni kwa hali gani unahitaji ajira. Kuna mamia ya watu wanaoomba kazi hiyo hiyo. Hakikisha huonekani kwamba unahitaji kazi kwa kuwa unashida.

Badala yake, jiamini na onyesha jinsigani utasaidia kampuni/shirika, na sio jinsi gani kampuni/shirika itakusaidia wewe. Kwa mfano, usiseme ‘Nataka nafasi hii ili nijufunze zaidi kuhusu masoko’. Sema, ‘uwezekano wakuleta uzoefu wangu wa masoko unanipa motisha ya kufanya kazi hii. Pia, nafurahia uwezekano wa kujifunza mengi zaidi kutoka kwa wataalam wako ili kufikisha bidhaa zako kwa watu wengi zaidi”.

6. Kutofanya utafiti ya kampuni/shirika kabla ya kutuma maombi ya kazi

Hakuna kitu kibaya kama kuomba kazi bila kujua lolote kuhusu hiyo kampuni unaloomba kazi.

Kupitia tovuti au kurasa za Facebook, Twitter, LinkedIn n.k inaweza ikakusaidia sana. Inabidi ujue kampuni hiyo inajali nini hasa, kabla ya wewe kuonyesha ni thamani gani utakyoleta kwenye nafasi hiyo.

Waajiri wanfurahishwa wakijua mwomba ajira amefanya utafiti juu ya maadili, malengo na mafanikio ya kampuni. Inawaonyesha kwamba umejitayarisha vya kutosha na huleti mzaha. Itakusaidia kwenye kushindania nafasi hiyo.

7. Makosa ya kuandika

Unapewa nafasi moja tu kuomba kazi. Hakikisha hujakosea kwenye kunadika neno lolote.

Makosa ya kuandika yanamuonyesha mwajiri kwamba hujali kazi yako na kwamba hukuipitia kwa undani uliyo hitajika.

8. Kujilazimisha kuandika wa Kiingereza kwa mara ya kwanza

Watu wengi wanatoka jasho wakitakiwa kuandika barua ya kuomba kazi kwa Kiingereza. Lengo lao linaiishia kuwa kuimaliza badala ya kuiandika kwa ubora.

Ni wewe tu mwenye uwezo wa kuelezea uzoefu na thamani utakayoleta kwenye nafasi unayoomba. Kwa hiyo, ni wewe tu unayeweza kuandika barua ya kuomba kazi na CV.

Kama kiingereza sio lugha yako ya kiasili, andika barua ya kuomba kazi kwa lugha yako ya kiasili alafu mwombe rafiki au ndugu yako aipitie.

9. Kuwasilisha CV na barua ya kuomba kazi ambazo ni ndefu

Barua yako ya kuomba kazi inabidi isizidi ukurasa mmoja na ili ionekane zaidi ya zingine, inabidi iendane kampuni na nafasi ya kazi unayoomba.

Karibia kila mtu anasema kwambe yeye ni mchapa kazi na anauwezo wakufanya kazi mwenye au kwenye kundi. Onyesha ufanisi wako kwa kuonyesha sifa hizi kwa kutumia mafanikio yako.

10. Kupuuzia maelekezo ya kuomba kazi

Usitume vyeti kama umeambiwa utume CV tu. Usitume CV iliyochapishwa kama umeelekezwa kutuma kwa kupitia barua pepe.

Ukipuuzia maelekezo muhimu, unamuonyesha mwajiri kwamba huwezi kufuata maelekezo ya kawaida. Unaweza ukawa na kipaji kikubwa sana ila kama unaonyesha kwamba kufanya kazi na we italeta shida, waajiri hawatakuchagua.

Jifunze kutoka kawa makosa yako

Kama unajikuta kwamba umetuma maombi mengi ya kazi lakini huitwi kwenye interview, inabidi upitie upya mbinu zako za kutafuta kazi ile ujue ni makosa gani unayo ya fanya. Ila, usikate tama. Badala yake, boresha CV na barua yako ya kuomba kazi ili kuongeza ushindani wako kwenye utakazoomba.

Iman Lipumba
A digital storyteller, experienced in creating content that improves website visibility on search engines, enhances the user experience, and nurtures brand loyalty. With a background in the social sciences, an expert in researching complex ideas, and communicating them in engaging language to multiple audiences.