Maisha yaliyo Changamka: Muziki, Sanaa na Utamaduni wa Tanzania

  | 4 min read
0
Comments
1245

Watu

Ingawa kuna zaidi ya kabila 120 na lugha 128 zikitumika, watanzania wameweza kubaki kama walivyo, watanzania. Popote pale mtanzania atakapoenda atajiita mtanzania kwanza. Akiulizwa maswali mengi, anaweza akataja kabila yake. Ila, watanzania ni watanzania kwanza. Ndio utamaduni wao.

Zaidi ya hapo,  ni kidogo watanzania wagawanyike kwa usawa kidini kati ya wakristu na waislam. Zaidi ya hapo, wameishi pamoja vizuri tangu uhuru. Ndio, tofauti zinatokea hapa na pale ila yatasuluhiswa. Sera ya Ujamaa na lugha ya Kiswahili zimechangia sana kwa hii.

Ujamaa ulikuwa sera ya kiuchumi iliyoanzishwa na serikali ya kwanza ya Tanzania yenye msingi wa kusaidiana katika jamii. Ingawa iliishia kuumiza uchumi, uliweka msingi wa nguvu wa umoja nchini baada ya kupata uhuru.

Sasa, kama Ujamaa ulikuwa nyumba ya hisia hii ya umoja, Kiswahili ilisema ‘karibu’ na ikakaribisha hisa hii. Kiswahili, lugha ya taifa, ili waunganisha watanzania wote na kuleta mshikamano wa nguvu.

Kutokana na hisia za kifamilia zilizotoka kwa vizazi vya zamani, watanzania ni wamekuwa watu wa kirafiki sana. Ni kawaida kumwona mtanzania akisalimiana kwanza na mwenye duka, rafiki, mfanyakazi au mtu yoyote yule akimuita ‘kaka’ au ‘dada’, tofauti majirani we tu wa Afrika Mashariki. Kwa hiyo, ingawa inakubalika zaidi siku hizi, kutomsalimia mtu kabla ya kuendelea na mazungumzo mengine bado inachukuliwa kama vile humheshimu huyo mtu.

Kwa ujumla, watanazania ni watu wenye ukarimu na utulivu.

Vyakula na Kula

Vyakula utakavyokuta popote nchini ni wali, ugali na hivi karibuni, chips. Ukialikwa nyumbani kwa mtu, kuna uwezekano mkubwa wa kwamba utakuta moja kati ya vyakula hivi mezania. Aidha, kama umeamua kwenda kwenye mgahawa, pitia menu. Tisa kati ya menu 10 zitakuwa zimeweka kinyota pembeni ya kila mlo na kwa chini kueleza kwamba, kila mlo unakuja na wali/ugali/chips.

Watanzania ni walaji wa nyama. Iwe nyama ya ng’ombe, mbuzi, kuku, nguruwe, samaki , kama nyama ipo italiwa. Kumpata mtu asiyekula nyama kabisa hapa ni kama kumtafuta mtu anayeongea Kiswahili Urusi; itachukua muda saaaaaana, ila, unaweza kubahatika kumpata.

Mlo wa asubuhi Tanzania ina mchanganyiko wa vyakula vitamu na visivyo tamu. Sambusa, chapata, maandazi, supu ya kuku/ng’ombe, mkate, viazi na mengineyo ni vyakula vya asubuhi vya kawaida. Chai na kahawa ndio vinywaji vinavyopendwa asubuhi.

Sanaa

Iwapo sanaa ya kucheza au kuigiza bado inakua nchini, sanaa ya uchoraji na vinyago vimeenea. Uchoraji wa Tingatinga na vinyago vya Wamakonde vinapendwa sana na watalii na wenyeji pia.

Jifunze zaidi kuhusu sanaa ya kitanzania hapa

Muziki

Utamaduni wa muziki Tanzania ni nzito. Kwanza, kila kabila ina muziki asili yake, yenye sauti tofauti. Ila, ngoma ni kitu pekee utakacho kikuta kwenye muziki asili za karibia kabila zote. Na hivyo, muziki wa kitanzania kwa ujumla unaongozwa na ngoma.  Ila, iwe kwa kufuraha au kwenye huzuni, nyimbo, kucheza na muziki kwa ujumla zimekuwa njia ya watanzania kujieleza na kujiburudisha kwa namna moja au nyingine.

Baada ya ukoloni, muziki wa bendi ikisukumwa na aina ya muziki ya Lingala kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, uliingia nchini. Na hadi leo, bado unapendwa na unadunda. Vizaza vya zamani na vya leo zote zinafurahia muziki wa aina hii. Vilevile, Taarab ambayo inaunganisha midundo ya kiarabu na ngoma za pwani, inapendwa sana pwani na pia kwenye maeneo mengine nchini.

Muziki wa kizazi kipya ndio unaovuma siku hizi na ndio utakachosikia ukiwasha redio. Bongo Fleva ndio aina ya muziki maarufu Tanzania hivi sasa. Ikiwa na hisia za hip hop, r&b na pop za Marekani na hivi sasa Nigeria,  inasauti yake ya kipekee ya kitanzania. Umekuwa kwa kasi sana ndani ya miaka 10 zilizopita na kuvuma wasanii wa hadhi ya kimataifa kama AY, Diamond Platnumz Ali Kiba na Vanessa ‘Vee Moneyy’ Mdee.

Tafuta matukio ya muziki Tanzania hapa

Utamaduni uliochangamka lakini ulio tulio vilevile

Rangi, ladha, urafiki na uchangamfu ndio viungo muhimu vya utamaduni wa Tanzania. Iwe chakula, muziki, sanaa ama watu wenyewe, chochote cha kitanzania kitakuwa na moja kati hivi vitu (kama sio vyote). Watanzania wanaweza wakawa na ukarimu kwa wageni zaidi ya wenyeji, ila kwa ujumla ukarimu wao uko sawa kote kote; Lakini, barabarani, hii ni swala lingine tofauti kabisa.

Iman Lipumba
A digital storyteller, experienced in creating content that improves website visibility on search engines, enhances the user experience, and nurtures brand loyalty. With a background in the social sciences, an expert in researching complex ideas, and communicating them in engaging language to multiple audiences.