Magari 5 Yasiotumia Mafuta Mengi Tanzania

  | 2 min read
0
Comments
77586

Zaidi ya kuwa bugudha, foleni inaongeza matumizi ya mafuta, hasa kwenye miji ya watu wengi kama Arusha, Mwanza na Dar.

Iwapo, kuwa tabia za kubana matumizi ya mafuta kama kudumisha gari lako, kuzima AC na kuendesha kwa spidi ya kawaida yatasaidia, bora uwe na gari isiyotumia mafuta mengi.

Uzuri wa magari yasiotumia mafuta mengi ni kwamba si lazima yawe ghali. Na tumeziorodhesha hapa.

1. Toyota IST

IST ni gari ambayo wanunuzi wake ndio mara yao ya kwanza kuwa na gari au watu wenye bajeti ya kawaida wanaotaka gari la kila siku ambayo ni rahisi kuidumisha.

Kutegemeana na mwaka na hali yake kwa ujumla, zinaweza zikakugharmia TZS 8m – TZS 12m.

Pitia IST zinazouzwa hapa.

2. Toyota Vitz

Vitz inafanana na IST kwenye utendaji ila ni ndogo zaidi na nafuu zaidi. Ila, injini yake ina nguvu yakutosha.

Kutegemeana na mwaka na hali yake kwa ujumla, zinaweza zikakugharmia TZS 6m – TZS 9m.

Pitia Vitz zinazouzwa hapa

3. Toyota Passo

Kwa swala la ubunifu, Passo ni kubwa zaidi ya Vitz ila ikijia kwenye maswala ya utendaji, yanatofautiana kidogo sana. Watu watano wanatosha kwenye gari hii pamoja na mizigo na pia, gari linaweza kutembea 100km kwa lita 7.

Kutegemeana na mwaka na hali yake kwa ujumla, zinaweza zikakugharmia TZS 6m – TZS 8.5m.

Pitia Passo zinazouzwa hapa.

4. Nissan March

Ingawa inaonekana ndogo, ndani kuna nafasi ya kutosha kabisa kwa sababu ya jinsi matairi yalipowekwa pamoja na uwezo wa viti vya nyuma kuvunjwa. Pia, udogo wake inaiwezesha kupenya barabarani.

Kutegemeana na mwaka na hali yake kwa ujumla, zinaweza zikakugharmia TZS 4m – TZS 6m.

Pitia Nissan March zinazouzwa hapa

5. Honda Fit

Ubunifu wa Honda Fir ndio kinachoiwezesha kuwa na matumizi mazuri ya mafuta. Badala ya kuifanya iwe kubwa zaidi, na hivyo kuongeza uzito wake, Honda waliamua kwamba wataongeza nafasi kwa kuweka tenki la mafuta chini ya viti vya mbele na kupandisha viti vya nyuma. Hii imewezesha gara hii kutembea 100km kwa 7.1L.

Kutegemeana na mwaka na hali yake kwa ujumla, zinaweza zikakugharmia TZS 8m – TZS 14m.

Pitia Honda zinazouzwa hapa

Faida haziishi

Kuwa na gari yenye matumizi mazuri ya mafuta itakupunguzia gharama ya uendeshaji sana! Sasa kwa kuwa una chaguo za magari yasiotumia mafuta mengi, pitia magari yanayouzwa kupitia ZoomTanzania.

Iman Lipumba
A digital storyteller, experienced in creating content that improves website visibility on search engines, enhances the user experience, and nurtures brand loyalty. With a background in the social sciences, an expert in researching complex ideas, and communicating them in engaging language to multiple audiences.