Maendeleo ya Uchumi na Viwanda Tanzania

  | 4 min read
0
Comments
1964

Tanzania imebadilika sana ndani ya miaka 50 yaliopita. Ikiwa na kiongozi mpya anaejulikana kama ‘Buldoza’  kwa kuendesha msukumano wa kujenga barabara, uchumi wa Tanzania inaanza kukuza ukuaji wa muda mrefu. Ila, mishtuko ya hapa na pale hujitokeza.

Sekta muhimu zinazochangia uchumi wa Tanzania ni utalii, madini na kilimo. Zote zimeweza kuongeza ushindani mkubwa ndani yao, na hivyo kuboresha huduma.

Kilimo

Kwa muda mrefu, nchi nyingi za Kiafrika zilikuwa zinategemea kilimo kuendeleza uchumi wao. Hii bado inaukweli kijijini. Pia, 30% ya kipato cha nchi inatoka kwenye kilimo wakati 60% za nafasi za kazi zinatoka sekta hii pia.

Kwa mujibu wa Tanzania Invest, mazao makuu yanayouzwa nje ni tumbaku, pamba, mkonge, korosho, kahawa, chai na karafuu. Malengo yamewekwa kwenye mazao haya na matokea yake ni kwamba uzalishaji umeongezeka kwa 44% kutoka 2008 – 2013. Kwa mujibu wa Tanzania Invest, tumbaku ni zao inayouzwa nje kuliko zote ikileta $318m kwenye mwaka 2015, ikifuatiwa na korosho – 201m na kahawa 162m.

Pia kuna vikundi mbalimbali vya kilimo vilivyundwa na serikali ili kuboresha usalama wa chakula na uzalishaji wa kilimo. SAGGOT – Southern Agricultural Growth Corridor of Tanzania na TADB – Tanazania Africulture Development Bank ndio zenye umuhimu kuliko zote.

Nishati

Zaidi ya 80% ya jumla ya nishati ya msingi Tanzania ni kutoka mkaa na kuni. Mafuta ni 9% na umeme ni 4.5%, ila, kugundulika kwa gesi inawaza ikabadilisha takwimu hizi kwa kuwa Tanzania imeanza kujulikana kwa nishati.

Ingawa mkaa unatumika sana Tanzania, ukilinganisha na nchi zingine za kiaafrika kama Afrika Kusini na Zimbabwe, hifadhi za mkaa, ambazo ni 1.9bn, sio kubwa sana. Ila, hii ni 25% tu ya hifadhi zilizogundulika Tanzania. Miradi mingine zilizodhaminiwa na serikali zimeanza kuchunguza hifadhi zingine.

Pia, Tanzania ni muingizaji wa bidhaa za mafuta ya petroli. Imeshaingiza 4.6bn za bidhaa za mafuta ya petroli.

Benki

Mpaka Machi 2015, kulikuwa na benki 56 pamoja na taasisi za fedha. Mwaka 2009, idadi hii ilikuwa 38. Benki kuu ya Tanzania inamatumaini ya kufikia ongezeko la 7.3% kwenye pato la nchi kati ya 2016 – 2017.

Pia, takwimu zilizopatikana na Tanzania Invest zinaonyesha kwamba mali zote za BOT zilifikia gharama ya TZS 19,522.92bn kwa 2013-2014.Takwimu za 2015 – 2016 bado zinakusanywa. Ingawa mfumuko wa bei huwa ni tatizo kwa Tanzania, hii imepungua hivi karibuni kutoka 6.5% mwaka 2013 mpaka 4.3% mwaka 2015.

Nyumba na Makazi

Sekta ya nyumba na makazi imefaidika na nafasi kamili kuundwa kwa ajili ya sekta ya nyumba na makazi. Miradi ya nyumba na makazi za hivi karibuni zimeongeza nafasi ya uwekezaji kutoka nje pamoja na ndani.

Ongezeko kwa mahitaji ya sekta ya nyumba inaletwa na ongezeko mkubwa zaidi wa watu. Idadi ya watu nchini inakaribia 54m. Idadi hii inategemewa kuongezeka kwa mara mbili tukifika mwaka 2050. Mahitaji ya nyumba Tanzania kwa sasa hivi ni 200,000 kwa sasa, kukiwa na pungufu ya nyumba 3m.

Madini

Ndani ya Tanzania, madini inajumuisha metali na madini. Mwaka 2014, iligundulika kwamba madini yalichangia 3.75 ya kipato cha nchi. Hii ililetwa na mahitaji makubwa duniani ya:

  • Almasi
  • Tanzanite
  • Marijani
  • Garnet
  • Chokaa

Kwa mujibu wa mpango wa maendeleo ya Tanzania, madini yanapaswa kuchangia sio chini ya 10% kwenye kipato cha nchi ikifika 2025. Jumla ya mauzo ya nje ya almasi ilifika $61.7m wakati huu ulikuwa jumla ya nishati za viwanda vyote kwa pamoja.

Mzalishaji wanne wa dhahabu duniani ni…Tanzania! Dhahabu inauzwa Afrika Kusini, India, Uswisi na Australia hasa hasa.

Aidha,  amana kubwa za uranium zimegundulik hivi karibuni huko Mkuju. Waziri mkuu wa Urusi, Dennis Manturov, ana matumaini ya kuanza kuendesha mgodi hiyo mwaka 2018.

Utalii

Utalii unachangia kipato cha nchi kwa mara tatu zaidi ya kilimo. Hivi sasa, ni sekta inayoongoza kwa kuchangia kipato cha nchi – ikiingiza $1bn! Kwa kuwa kuna hoteli nyingi Tanzania bara na Zanzibar za kifahari, pamoja na huduma nzuri na amani nchini, haishangazi sana kwamba Tanzania imekuwa nchi inayovutia sana.

Sekta ya Huduma

Mwaka 2015 ilifunuliwa kwamba sekta ya huduma ya Tanzania imeweza kuchangia 49% kwa kipato cha nchi. Hii ilishangaza sana kwa kuwa kawaida, sekta hii haitiliwi uzito sana Afrika. Lakini hii imebadilika.

Kiukweli, utafiti uliofanyiwa na All Africa umeonyesha kwamba 21% ya ajira rasmi iko kwenye sekta ya huduma, na kuna uwezekano mkubwa kwamba idadi hii itakuwa kwa mara mbili kwa sababu ya sekta ya ajira rasmi nchini.

Mambo mazuri yanakuja

Kwa ujumla, uchumi wa Tanzania umekuwa vizuri katika miaka yaliyopita na sekta tofauti zinajiboresha. Ingawa, miundombinu yanaweza kuboreshwa kwa sana, nchi inamuelekeo mzuri kwa ujumla.

Iman Lipumba
A digital storyteller, experienced in creating content that improves website visibility on search engines, enhances the user experience, and nurtures brand loyalty. With a background in the social sciences, an expert in researching complex ideas, and communicating them in engaging language to multiple audiences.