Laptop 10 Bora za Kununua Kwa Matumizi Binafsi na Kwa Kazi

  | 3 min read
0
Comments
4944

Kuna vitu vingi vya kufikiria ukiwa unanunua Laptop:

Gharama:

Hii itategemea na bajeti na matumizi yako. Kwa hiyo fikiria hivyo vitu viwili kwanza kabla ya kununa laptop; yatakusaidia san kufanya maamuzi.

Urahisi wa kuitumia

Unataka laptop ambayo ni rahisi kutuimia. Hutaki kukerwa nayo.

Betri

Hii itategemea na matumizi yako. Kama utakuwa unaitumia sana, laptop yenye betri inayodumu itakufaa zaidi

Ubebaji

Kama utakuwa unatembea nayo mara kwa mara, laptop nyepesi ndio itakayo kufaa. Ila, kama itakuwa inakaa nyumbani/ofisini kwa karibia muda wote, uzito wake sio swala la kufikiria sana.

Prosesa

Kwa kifupi, laptop zenye bei zaidi ndio zenye prosesa za nguvu zaidi.

Sasa, twende kwenye orodha yetu ya laptop 10 bora za kununua kwa matumizi binafsi na kwa kazi.

1. Dell XPS 13

Hii ina betri ya kudumu, keyboard bora pamoja na trackpad inayofanana na Macbook Air, ila ni bei nafuu zaidi.

Bei yaki ni kati ya $900 – $1200, kutegemea na prosesa yake.

2. Asus ZenBook UX305

Kwa bei safi ya $600 – $750 kutegemea na prosesa yake, ZenBook ni nyepesi, ina betri ya kudumu na ni rahisi kutumia.

3. Macbook Air (Inchi 13)

Hii ni laptop bora ya apple kwa bei yake.

Ni nyepesi, nyembamba na rahisi kutumia.

Bei yake ya kuanzia ni $800 – $1200. Hizi bei ni za chini kwa laptop za Apple.

4. Dell Inspiron 3542

Inagawa ni nzito,hii ni laptop nzuri kwa bei nafuu, urahisi wa kutumia na keyboard safi.

Bei yake ni kati ya $600 – $700.

5. Lenovo Thinkpad T4600 (inchi 14)

Kama betri ya kudumu ndio cha muhimu kwako, nunua laptop hii. Ni nzuri kwa kufanyia kazi kwa kuwa ni rahisi kutumia na inadumu sana. Pia, keyboard yake ni safi sana.

6. Macbook Pro (Retina Display)

Kama bajeti inaruhusu, nunua hii laptop. Ina betri inayodumu kwa masaa 12, prosesa ya maana, ni nyepesi na ina urahisi wa kutumia ya kipekee.

7. Acer Aspire Cloudbook

Hii ni moja kati ya laptop za bei nafuu zenye Windows 10. Betri yake inadumu na unaweza ukaipata kwa hata $200.

8. Microsoft Surface Pro 3

Ingawa hii inaangukia kwenye kipengele cha Tablet, iko kama laptop, na inauzwa kwa bei nzuri. Stendi yake inarahisisha matumizi yake, betri yake ni nzuri na nirahisi kutumia kwa ujumla. Ubaya wake ni kwamba unabidi kununua keyboard peke yake.

Pamoja na keyboard, gharama yake inafikia $1000.

9. HP Spectre X360

Inamuonekano wa kisasa na inaweza ikageuzwa kuwa tablet. Spika zake ni nzuri sana, ina prosesa ya Core i5 na ina nafasi/kumbukumbu nyingi.

Bei yake ni $900

10. Lenovo Yoga 900

Betri yake ni safi na wataalam wanapenda keyboard yake. Uzuri wake mwingine ni kwamba inaweza kukunjwa kwa pembe nyingi, ikiwemo pembe ya kuifanya kama tablet. Wepesi wake inaipa sifa ya kuwa bora kwa ajili ya kazi, kusafiri na matumizi ya binafsi.

Bei yake ni $1020.

Pata laptop yako leo

Kwa kuwa umeshagua laptop nzuri ni zipi, tafuta itakayokufaa wewe hapa.

Iman Lipumba
A digital storyteller, experienced in creating content that improves website visibility on search engines, enhances the user experience, and nurtures brand loyalty. With a background in the social sciences, an expert in researching complex ideas, and communicating them in engaging language to multiple audiences.