Kwenda Kambini Tanzania: Wapi pakwenda

  | 4 min read
0
Comments
496

Watu wanaoenda kambini Tanzania huwa ni wasafiri wanaotaka kubana matumizi na hivyo wanapendelea malazi ya gharama nafuu wakiwa wanatembelea nchi na kwenda kwenye mbuga za wanyama. Watanazania wengi hawaoni kwamba kwenda kambini ni burudani ya kufurahia na familia, huwa wanapendelea kwenda ufukweni au kwenye mji/kijiji kingine.

Ndio, kuwa fukweni ukiwa na kinywaji baridi inaridhisha sana. Ila, kama una nia yoyote ya kupata uzoefu na mazingira ya nje, fikiria kwenda kambini.

Kambi ni nafasi ya kujiweka ndani ya mazingira ya asili. Una lala nje kwenye aridhi, unapata upepo wa kiasili, na unasikiliza ndege wakiimba, matawi ya miti yakicheza na wanyamapori wakipita.

Kwa bahati nzuri, Tanzania ina sehemu nyingi nzuri za kwenda kambini ndani ya mbuga za wanyama, misituni na hata ufukweni. Kukuanzisha, pitia orodha yetu hii ya sehemu kumi za kwenda kambini Tanzania:

1. Udzungwa Forest Camp, Dodoma

Udzungwa Forest Tented Camp iko kwenye mpaka wa Udzungwa Mountains National Park. Wakazi wa pale wameipa hoteli hii jina la Hondo Hondo, kwa kuwa ndege hizi zimejaa huko.

Kambi ya Udzungwa Forest ina aina 3 za malazi: vyumba vya mahema, vibanda na malazi ya nje. Pia, wanaweza kuandaa sehemu maalum ya kuweka kambi ndani ya Udzungwe Mountains National Park.

Vifaa vya kambi vilivyopo ni:

 • Mahema, godoro na mito ya kukodi
 • Bafu zenye maji ya moto
 • Vyoo vya kisasa
 • Sehemu ya kupikia
 • Sinki kubwa ya kuoshea vyomba
 • Sehemu mbili za kuchoma nyama kwa mkaa
 • Sehemu ya kuota moto yenye mtazamoa wa milima ya Udzungwa na Bonde la Kilombero

2. Masai Camp, Arusha

Masai Camp ni sehemu ya kawaida na ya gharama nafuu. Ikoo kilometa 3 kutoka Arusha mjini na ina sehemu ya kambi, vyumba vya mtu mmoja au watu wawili na banda za kimasai.

Pamoja na mandhari mazuri yaliyopo, unaweza ukajituliza hapo kambini kwenye baa, ukiwa una sikiliza muziki mzuri laivu na kucheza pool.

Pia, wanjivunia kuwa na Enchilada bora Afrika Mashariki.

Soma maoni mengine kupitia Tripadvisor.

3. Lilac  Lake Manyara Budget & Luxury Campsite, Arusha

Lilac Lake Manyara Budget and Luxury Campsite ina kambi zenye mahema pamoja na eneo linigine la kambi ambayo ni ya gharama nafuu zaidi.

Kujua zaidi, tembelea tovuti yao

4. Chawaba Camping Village, Kigamboni – Dar es Salaam

Chawaba Camping Village iko kwenye eneo ya Kigamboni inayoitwa South Beach. Chawaba Camping Village inatazama fukwe ya aina yake na maji masafi mno.

Chawaba Camping Village ina aina mbili za malazi:

Vibanda vyenye:

 1. Godoro
 2. Vyandarua
 3. Chumba cha kuoga

Sehemu ya mahema (uje na tent yako) yenye:

 1. Usalama wa masaa 24
 2. Sehemu ya kufua
 3. Vifaa vya kuchoma nyama na vyombo vyake.

Kujua zaidi tembelea tovuti yao.

5. Ikoma Bush Camp, Serengeti

Ikoma Bush Camp iko kwenye kichaka cha miti ya Acacia na ina mtazamo mzuri sana wa savannah na anga. Jina lake lingine ni Serengeti Tented Camp. Iko kwenye mpaka wa Serengeti, kwenye njia inyotumiwa na Nyumbu kutembea kati ya Kenya na Tanzania.

Kambi hii in mahema yenye:

 • Choo
 • Fenicha vya kisasa
 • Kibaraza

 

Mgahawa na baa kuu zina sehemu kubwa ya kuota moto – hii ni sehemu nzuri ya   kujipumzisha baada ya siku ndefu ya kuwa kwenye mbuga za wanyama.

Soma maoni ya watu kupitia TripAdvisor.

6. The Lakeshore Lodge and Campsite, Rukwa

Lakeshore Lodge and Campsite iko mwisho wa Ziwa Tanganyika, karibu na kijiji ya Kipili, Tanzania Magharibi kwenye mkoa wa Rukwa. Ina malazi mbalimbali yakiwemo:

 • Kuweka kambi chini ya miti ya maembe yenye miaka 80.
 • Banda za gharama nafuu zenye vyumba vya faraja kwenye bustani na mtazamo mzuri wa ziwa.
 • Banda za kifahari zilizopo ufukweni zenye upatikanaji wa fukwe za kibinafsi.

Pia, ina vitu vingine vya kufanya kama:

 • Scuba diving
 • Snorkeling
 • Kayaking
 • Quad bikes
 • Baisikeli za kupandia milima
 • Safari za kwenda Katavi National Park
 • Fly camping on private beaches

7. Lua Cheia, Kisiwa ya Mafia

Kama unataka kwenda kwenye kambi ya kifahari, nenda Lua Cheia Camp iliyopo kwenye kisiwa ya Mafia.

Iko Ras Bweni, kaskazini mwa Mafia kwenye fukwe binafsi ya urefu wa 2km.

Tembelea tovuti yao kujua zaidi.

8. Simbamwenni, Morogoro.

Simbamwenni Lodge iko karibu na soko la mjini Morogoro na ni sehemu nzuri ya kufika kama una penda kwenda kambini.

Weka kamba yako kwenye eneo lao la kambi. Utaweza kupata:

 • Bafu zenye maji ya moto
 • Vyumba vya kujisaidia
 • Chakula (ukihitaji)
 • Eneo ya kula
 • Table Tennis
 • Sebule

9. Kipepeo Beach Camp, Mjimwema – Dar es Salaam

Kipepeo Campsite ina wahudumia wasafiri wa aina yoyote na wapenzi wa fukwa. Eneo lao la  kambi ina usalama, vyoo, bafu na bar iliyopo fukweni. Pia, kuna mgahawa na sehemu ya nyama.

Kwa wale wasiotaka kulala kwenye hema, wana vibanda vya gharama nafuu zenye vitanda viwili na vyandarua.

Soma maoni ya Kipepeo Beach Camp kupitia TripAdvisor.

Tafuta sehemu bora la kwenda kambini

Ukiwa unataka kambi la kifahari au ya kawaida, kuna kambi zingine nyingi zitakazofaa mahitji yako.

Zipitie hapa!

Iman Lipumba
A digital storyteller, experienced in creating content that improves website visibility on search engines, enhances the user experience, and nurtures brand loyalty. With a background in the social sciences, an expert in researching complex ideas, and communicating them in engaging language to multiple audiences.